Jifunze silaha kuu tano (5) za ulimwengu wa kiroho ili upate ushindi kwenye kila jambo

MAOMBI YA MFUNGO.
Kufunga ni kufanya ibada ambayo unajisogeza karibu na Mungu wako,unafunga ili kufungua vifungo vikubwa vilivyoko juu yako viweze kuondoka.

Unafunga huku ukitarajia kulegeza nira ulizofungwa na shetani ziweze kukuachia na wewe uwe huru.

Unafunga ili kuutiisha mwili usiwake tamaa ya kutenda dhambi na kujikuta umemuasi mola wako.Maandiko yanasema roho i radhi ila mwili ni dhaifu.

Roho yako inatamani kutenda mema lakini mwili unakusuma kutenda dhambi, na huwezi kuishinda dhambi kama huna nguvu za kuishinda dhambi.

Dhambi ni uasi. Roho yako haitaki kutenda dhambi lakini mwili unaisukuma roho yako itende dhambi ili uharibu kiroho chako.

Mwili ukiharibika,na Roho wa Mungu hakai ndani yako.Mwili ni nyumba ya Roho Mtakatifu, kwasababu mwili wa mtu anayeamini katika Kristo ni hekalu la Roho Mtakatifu.

Kwahiyo mambo mengine hayawezekani kukuachia isipokuwa kwa kufunga na kuomba. Ukiutiisha mwili kwa kufunga maan yake unaunyong'onyesha na unakosa nguvu za kutenda dhambi.

Mara nyingi dhambi hapa ya kwanza inayotakiwa kuishiwa nguvu ni UZINZI kwasbabu hii inafanyika katika mwili na huvuruga sana kiroho cha mtu na kuharibu mfumo mzima wa Mungu ndani yako.

Unapofunga mwili wako unakuwa hauna nguvu ya kukuongoza kutenda dhambi bali roho yako ndio inakuwa na nguvu ya kufanya maamuzi katika njia za haki.

Kwasababu gani!?

Kwasababu, mwili unabaki hapa duniani hauna makao huko mbinguni wakati roho ya mtu inabidi iende mahali palipo salama.

Sasa Biblia inavyosema roho i radhi ila mwili ni dhaifu, maana yake ni kwamba roho iko tayari kabisa kumcha mola wake aliyeiumba kwasababu inatakiwa baada ya kuishi ndani ya mwili wa mtu irudi ilikotoka, lakini inashindwa na mwili unaoitaka ibaki duniani, yaani udongoni, kwasababu mwili uliumbwa kwa udongo,wakati roho ilitokana na sehemu ya pumzi ya BWANA.

Mwili na udongo ni asili moja,kwakuwa mwili ulifinyangwa kwa udongo. Roho na Mungu ni sehemu moja. Kwahiyo hapa lazima kuwe na msuguano. Huwezi kuushinda mwili usikupotoshe kama huna nguvu za kuuchosha ili usikuletee tamaa za uzinifu na uasherati.

Mwili unapenda uuvishe vizuri, uishi mahali pazuri, ulale mahali pazuri, ule vizuri ili unawiri, utumie mafuta mazuri na manukato mazuri mazuri, mwili unapenda umiliki vitu vizuri. Mwili bwana unapenda umiliki pisi kali zote za mtaa (kwa wanaume lakini).

Wenyewe unakushauri,unaonaje ukiwa na hiki,au ukiwa na kile? Unakwambia vitu ambavyo huna uwezo navyo wala huna njia za haki za kuvipata. Hapo ndipo unawaka tamaa kwamba lazima nivipate kwa njia yoyote ile.

Utasema mbona mawazo yanaanzia rohoni,sasa iweje iwe tena mwilini. Ni sahihi.

Tamaa ya mwili huichochea nafsi yako ili ikubaliane na ushauri wa mwili wako. Roho yako haitaki ila mwili unaishinda nguvu na kuamua kufanya maamuzi yasiyo sahihi.

Unakuta mtu anasema kama kuomba nimeomba sana,sadaka nimetoa sana,mafuta nimepakwa sana,chumvi nimetumia sana,damu ya Yesu nimeimwaga sana.Lakini yote ni kama ninatwanga maji kwenye kinu, sipati upenyo kabisa,sijui ninakosea wapi, mbona,mbona, wenzangu wanapata miujiza na shuhuda kibao?

Mtu mpaka anasema mimi Mungu hanisikilizi maombi yangu maana "sijibiwagi ".Usikate tamaa ndugu yangu.Nguvu yako iko kidogo na mambo mengine hayawezekaniki isipokuwa kwa sala na kufunga.

TUSOME.MATHAYO MTAKATIFU 17:14-21.
Nao walipoufikia mkutano, mtu mmoja akamjia, akampigia magoti,akisema,

15.Bwana,umrehemu mwanangu ,kwa kuwa ana kifafa, na kuteswa vibaya;maana mara nyingi huanguka motoni, na mara nyingi majini.

16.Nikamleta kwa wanafunzi wako ,wasiweze kumponya. 17.Yesu akajibu, akasema,Enyi kizazi kisichoamini, kilichopotoka, nitakaa pamoja nanyi hata lini? Nitachukuliana nanyi hata lini? Mleteni huku kwangu.

18.Yesu akamkemea pepo, naye akamtoka;yule kijana akapona tangu saa ile.

19.Kisha wale wanafunzi wakamwendea Yesu kwa faragha wakasema Mbona sisi hatukuweza kumtoa?

20.Yesu akaambia, Kwasababu ya upungufu wa imani yenu.Kwa maana ,amini,nawaambia,Mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali mtauambia mlima huu,Ondoka hapa uende kule;nao utaondoka;wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu.

21.[Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga. ]

Mmeona hapo watoto wa Mungu. Yesu mwenyewe anasema mambo mengine hayawezekani isipokuwa kwa kusali na kufunga. Au kwa maombi ya mfungo.

Nipunguze maswali. Mlima huwa ni sehemu ya nchi yenye kupanda, kama huna nguvu huwezi kupanda mlima,Kama unaumwa huwezi kupanda mlima. Mlima ni sehemu iliyoinuka.

Ukiutazama mlima ni sehemu ya nchi iliyoinuka na kubwa halafu huonekana hata ukiwa mbali.Mlima ni kikwazo. Biblia ni maneno yenye mafumbo yanayotumia lugha ya picha na tamathali za semi.

Biblia inatumia ufundi wa Lugha katika kuwasilisha ujumbe wake,Yesu alipenda sana kutumia mafumbo.Mungu aliamua kutupa mafumbo ili aone ni kwa jinsi gani tutatumia muda mwingi kumtafuta na kuyafumbua mafumbo yake.

Hapa ndipo huwa tunaomba ili tuweze kujibiwa maombi yetu. Kwahiyo mlima huu ng'oka na ukatupwe kule ni kitu chochote kigumu,kikubwa, jaribu, dhambi,pepo,mizimu na jambo gumu lililo katika maisha yako,unaweza kuliamuru litoke ili uwe huru. LAKINI HALITOKI PASIPO KUOMBA NA KUFUNGA.

Ndugu zangu na wazazi wenzangu someni Biblia na muwanunulie watoto wenu Biblia huku mkiwafundisha na kuwafafanulia maandiko,maana kuna vijana wengi siku hizi wanatukana watumishi wa Mungu kwamba ni wa uongo wakati yote wanayoyafanya yameandikwa katika maandiko.

Shida siyo wao ni wazazi wao,kanisa la Mungu,baadhi ya madhehebu na baadhi ya watumishi kutosisitiza watoto wetu wasome maandiko.Wazazi tuko busy na mitandao na maisha,hatuna muda wa kufanya ibada za nyumbani tukiwa na watoto wetu.Tutadaiwa siku ya mwisho. Tuombe sana tumalize salama.Yesu anakaribia kurudi,ni vizuri tujiandae ili akifika twende wote Mbinguni, itapendeza sana kuliko uende wewe halafu uwaache wanao wakiteseka na kutaabishwa na mpinga Kristo.

MTU ANATAKIWA KUFUNGA SIKU NGAPI?

Maombi ya kufunga huwa ni siri kati yako na Mungu wako,au kati yenu na Mungu wenu.Unafunga kwa ajili ya kuomba msaada wa Mungu ukusaidie kuondoa milima iliyo ndani yako ambayo wewe mwenyewe umeshindwa kuiondoa.

Siyo vizuri kusema sema kwa watu kwamba mimi nimefunga, usifanye hiki kwa kuwa nimefunga, usile mbele yangu kwasababu nimefunga.

Ufungaji wako usiwaharibie watu wengine starehe zao;unayoyapitia wewe ,wao hawayajui wala hayawahusu. Huwezi kumzuia mtu asile eti anakuharibia swaumu kwa kuwa yeye hajafunga na wewe umefunga.

Huu ni wivu, kama ulikuwa huwezi kufunga pasipo watu wengine kujua kwanini ufunge, acha kusumbua watu,na huu ni unafiki, kwani unafunga kwa ajili ya watu au mola wako?

Na msipende kuomba kwa kupiga kelele hadi watu wengine wanajua kile mnachokiomba,hasa muwapo sehemu inayohitaji faragha. Mfano nyumbani penye watu wengi,mtaani,shuleni, ofisini, nyumba za kupanga, bwenini. Omba kwa utulivu,hata kimoyo moyo Mungu anakusikia maana Yeye haangalii mwili anaangalia moyo wako unawaza nini mbele zake.

Unapokuwa umefunga mtu asiyejua kama umefunga hatakiwi kujua chochote kinachohusiana na mfungo wako.

YESU ALIZUIA HII MAANA ANAJUA KUNA WATU WABAYA WATAKUHARIBIA MFUNGO WAKO.

Kuweni makini sana.Dunia imeshachafukwa.

TUSOME.MATHAYO MT.6:5
Tena msalipo, msiwe kama wanafiki;kwa maana wao wapenda kusali hali wamesimama katika masinagogi na katika pembe za njia,ili waonekane na watu,.Amini,nawaambia,Wamekwisha kupata thawabu yao.

6.Bali wewe usalipo,ingia katika chumba chako cha ndani ,na ukiisha kufunga mlango wako,usali mbele za Baba yako aliye sirini;na Baba yako aonaye sirini atakujazi.

7.Nanyi mkiwa katika kusali ,msipayuke payuke, kama watu wa mataifa;maana wao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu ya maneno yao kuwa mengi.

8.Basi msifanane na hao;maana Baba yenu anajua mnayohitaji kabla ninyi hamjamwomba.

Chumba cha ndani ni ndani ya moyo wako,usali kile kilichoko ndani ya moyo wako,mahitaji yako ambayo huwezi hata kumsimulia mtu mwingine.

Baba herufi "b"kubwa ni Mungu.

Kufunga mlango ni kuacha mawazo yote ya nje ya mwili na kufumba macho kwa ajili ya kuyaona ya rohoni. Ukiwa unaomba huku umefumba macho huwezi kuona vishawishi vya kukufanya uache kumakinika na maombi yako.

Mtu anauliza ulimwengu wa roho ukoje au ni wapi.

Fumba macho halafu uanze kutafakari uone utaona vitu gani,kiwango chako cha kuona ndicho kitakachokupeleka kuona ya mbali au karibu. Ila kama huna ulinzi angalia usije ukaona vitu vya kukutia uchizi. Kuwa makini.Ni vizuri uingie rohoni ukiwa katika ulimwengu wa roho wa NURUNI maana huku unaelekezwa wapi uishie na uone nini.

TUANGALIE UKIWA KATIKA SWAUMU UFANYEJE.

SOMA.MATHAYO MT.6:16-18.
Tena mfungapo, msiwe kama wanafiki wenye uso wa kukunjamana;maana hujiumbia nyuso zao,ili waonekane na watu kuwa wanafunga. Amini,nawaambia, wamekwisha kupata thawabu yao.

17.Bali wewe ufungapo, jipake mafuta kichwani, unawe uso;

18.ili usionekane na watu kuwa unafunga, ila na Baba yako aliye sirini;na Baba yako aonaye sirini atakujazi.

Hapa niiweke sawa.Siyo lazima kupaka mafuta kichwani au mdomoni kama midomo yako haijapauka,au kujinyong'onyesha wakati huna swaumu kiivyo.

Kiujumla usijionyeshe. Ndio maana watu husema eti Wakristo huwa hawafungi. Siyo kweli kwasababu huwezi kuwajua kama wamefunga maana haitakiwi kujionyesha.

Kuna mahali nimesoma eti kuna abiria alizuia ndege isiondoke kwasababu anataka kufanya ibada. Ndege ikabidi ichelewe maana kulitokea ubishi.

Mwingine tuko stendi ya mabasi anamwambia konda zima tv ya gari mimi ninataka kuomba. Hii yote ni ya nini. Kwani wengine tulitoka nyumbani pasipo kuomba au yeye anaona maombi yake ndio sahihi kuliko ya kwetu?

Huu ni unafiki tu,utakuta huyo ni mchawi na mwanga mkubwa sasa pale anajikosha ili aonekane ni mtu mwema.

Mtu aliye na Mungu utamjua kwa matendo yake,na wala siyo ajitangaze eti yeye ni mtu wa ibada sana,anaomba sana,anasali sana.

Kuna wachawi wengine huenda ibadani kwa kupaa ili wawahi seat zao wakiwa wa kwanza ,na hawakosi ibadani. Ole wako ukae seat yake ,cha moto utakipata nakwambia.

Eti nao wanasali.Jamani!!!

Siku moja bwana nilienda kanisani muda kidogo ndio nimeanza maombi,nikakaa sehemu yangu kama kawaida,pembeni yangu akaja mbibi wa makamo akaketi karibu yangu.

Akaniomba mistari ambayo walishafundisha ili anakiri. Nikampatia, ibada ikaendelea. Wakati wa maombi mwendesha maombi akasema tuombe maombi ya mnyororo.

Haya ni maombi ya kushikana mikono kanisa zima,yaani unamshika mtu aliyeko mkono wako wa kushoto na kulia. Huyu bibi yangu alikuwa kulia kwangu,na ni mkono wenye nguvu.

Katikati ya maombi nikasikia kelele kama mtu ananivuta mkono wangu kama anataka nimuachie fulani hivi, mimi sijui ninahisi upako umemkolea anaomba kwa nguvu,kwahiyo na mimi ninakaza mkono.

Baadaye ninasikia weweeee nimesema niachie mkono wangu kwanini unaniumizaaa!?

Nikafumbua macho,ninakuta katoa macho yamekuwa mekundu hayaelezeki. Nikasema sawa. Huku kanisa zima bado linaendelea na maombi. Nikamshika tena akawa anakimbiza mkono,akiuleta karibu anaukimbiza tena,nikujua kumbe huyu yupo hapa kwa kazi maalumu.

Maombi yalipoisha tukakaa kwenye viti.Hakutulia ninakuta ananiangalia kwa macho mabaya na ya mshangao. Na mimi sikumuacha nikawa ninamuangalia kwa macho ya kumzodoa, kwamba kumbe ulizoea vya kunyonga,sasa leo Roho Mtakatifu amekupatia uonje vya kuchinja.

Akawa anajibalaguza kucheza, ninamuangalia kwa kumwambia acha unafiki. Hakukaa, hata sijui aliondoka saa ngapi.

Kwahiyo nilitaka niwaonyeshe, usimuamini mtu,usimshirikishe mtu mambo yako kama humuamini. Watu wengi huwa wanaulizwa hivi umefunga kwa ajili ya nini?

Mtu naye anajibu utafikiri yuko kwenye usahili wa kazi.

Mimi pamoja na kuyafundisha haya ndugu zangu hawajui kama ninayajua haya. Hawajawahi kuniona nikienda kanisani wala msikitini. Huwa wananiambia siku nikifa nitazikwaje na akina nani.NINAWAAMBIA MANISPAA,KWANI MLIWAHI KUONA MAITI AKITEMBEA KWASABABU AMEKOSWA KUZIKWA ETI ALIKUWA HAENDI IBADANI?

Of course ninajua sitakufa maana Yesu karibu arudi nitaenda mbinguni na Unyakuo wa kanisa.Vipi wewe uko tayari twende wote Mbinguni siku hiyo ya UNYAKUO WA KANISA?

Karibu tujifunze neno la Mungu. Yesu ndiye njia ya kweli na Uzima, kila ajaye kwake hatapotea.

MTU AFUNGE SIKU NGAPI?

Kila mtu hufunga na kuomba kwa kiwango cha imani yake.
1.Wengine wanafunga kuanzia saa 12 alfajiri hadi saa nne asubuhi,wengine saa sita mchana, wengine saa 12 jioni.

2.Wengine kuanzia kuanzia saa 12 asubuhi mpaka kesho yake saa 12 jioni. (24hrs).

3.Wengine masaa 36,wengine 48,wengine 72.

4.Wengine siku tatu kavu,au siku 7 kavu.

5.Wengine siku 14,hadi 30,au 40.Yaani anafunga kavu moja moja hadi siku 40.

Ninavyosema kavu,ukila saa 12 jioni tarehe 31,ni mpaka kesho yake tarehe 1 saa 12 jioni.

Kiwango cha mtu cha kufunga kiendane na kiwango chake cha imani. Imani ndio nguvu ya Mungu iliyoko ndani yako.

Usijing'ang'anize kufunga siku nyingi wakati uwezo wako ni mdogo,utajikuta unaharibu afya ya mwili wako,midomo kupasuka, mwili kuishiwa maji,kukosa nguvu,vidonda vya tumbo n.k.

Kama ukijisikia unaishiwa nguvu unaweza kunywa chai,juisi, matunda ,hasa kwa mtu anayeanza ambaye bado hajakuwa na nguvu kubwa, au kwa mtu anayefunga siku nyingi.

Ukiwa umefunga na ukasikia kizunguzungu hata ukahisi kufa tumbo kuvuruga, kichefuchefu hata kutapika. Kula chakula cha kutosha ili upate nguvu.

Hali hiyo huwa inasababishwa na nguvu za Mungu kuingia ndani yako na kutoa nguvu za shetani kwahiyo lazima ujisikie vibaya. Sasa unapokula chakula zile nguvu za Mungu zilizoingia zinapata support au usaidizi wa chakula na kuanza kutengeneza roho yako iwe hai na kukupa nguvu za Mungu ,za kiroho na kimwili.

MTU AKIWA AMEFUNGA ANAFUNGUAJE?

Kama nilivyosema huko juu ikiwa ni mfungo wa matunda muda ukifika kama ni mchana au jioni ,unafungua kwa kula matunda tu na maji au juisi kwa muda wa hizo siku ulizofunga au utakazojaaliwa kufunga.

Kama ni mfungo wa chakula kigumu utaratibu ni ule ule kula saa nne asubuhi kula kama kawaida,saa sita mchana kama kawaida,jioni saa kumi na mbili jioni, kama kawaida.

Ila kwa anayefunga katika matunda na chakula ambaye hajazaoea mfungo anaruhusiwa kunywa maji na juisi katikati ya mfungo ili mwili upate nguvu ya kuendelea na maombi ya kufunga.

Ikiwa umefunga na ukajibiwa maombi YAKO unaweza kufungua ikiwa hujisikii mzigo ndani yako wa kufunga.

MTU ATAJUAJE KAMA ANATAKIWA KUFUNGA?
1.Unakosa hamu ya kula chakula na tumbo kujaa pasipo mtu kuhisi njaa.

2.Mambo yako hayaendi;hivyo unaona unahitaji nguvu za Mungu ili zikusaidie kukuvusha.

3.Unahisi kichefuchefu kila ukitaka kula na wakati mwingine unatapika kabisa wakati huumwi.

4.Dalili zake ni sawa na mwanaume ambaye mimba ya mke wake imehamia kwake.Kama hujawahi kupatwa na hili waulize waliowahi kukumbana nalo.

5.Unakuwa unaona kabisa hapa bila mfungo sitoboi wala sitajibiwa. Mungu anakupa ujumbe wako kupitia kufunga kwasababu wakati wa mfungo unakuwa na utulivu wa kutosha na sauti nyingi unaanza kuzitofautisha.

Hizo ni dalili baadhi kwa mtu anayeanza kufunga, nyingine ziko juu zaidi.Tuanze na hizi kwanza.

MFUNGO UNA FAIDA GANI KWA MTU?
1.Kiroho unaongezeka katika imani na nguvu za Mungu zinakuwa juu.

2.Unajibiwa maombi yako.

3.Unakutenga na vishawishi maana unakuwa ni dhaifu, vichocheo vya mwili vinakuwa chini sana.Ila kwa watu waliooa mwili unakuwa na nguvu katika tendo la ndoa, hasa kwa wanaume maana unapunguza mafuta mwilini kwa hiyo damu inatembea vizuri kwenye mishipa hadi chini. (Hii inasababishwa na mapepo ,kwahiyo yakiondoka yanakuacha na urijali wako).Ila ukimaliza ujue njaa utakayoisikia siyo ndogo yakupasa unywe maji mengi maana mwili unaishiwa nguvu,lakini baada ya muda zinarudi. Ukiendekeza unaharibu mfungo. Jifunze kujizuia mtu wa Mungu.

4.Unarejesha afya ya mwili,unakata kitambi, manyama uzembe, tumbo linakuwa huru sana.

5.Unakupa mfumo mzuri wa upumuaji maana mafuta mengi yanakuwa yameondoka.

6.Mfungo unafanya Ngozi yako kuwa nzuri hasa kwa watu wa rohoni. Msome Danieli sina muda wa kuandika kila andiko.

7.Afya yako kwa ujumla inaimarika,unapunguza uzito wa mwili na unakuwa mwepesi pasipo kufanya mazoezi ya viungo. Kiujumla unaimarika Kiroho na Kimwili.

MTU AFANYEJE KABLA HAJAANZA KUFUNGA NA KUOMBA.

Omba sala ya toba na rehema ili upate kibali cha Mungu kwa ajili ya kuondoa vifungo vyote vikubwa na vigumu vilivyokuwa juu yako.

Hakikisha una dhamira ndani ya moyo wako,unafunga kwa ajili ya kitu gani,unataka Mungu akutendee nini!

Usiache kutoa sadaka katika maombi yako.Sadaka isemeshe ndani ya moyo wako kwamba unataka Mungu akutendee nini.

Udhamirie kuacha kutenda dhambi.Usiwe kama ndugu zangu Waislamu na Wakristo. Wakiwa kwenye Ramadhani au Kwaresma, utakuta guest house zimeandikwa vyumba viko wazi.

Sasa ngoja watoke siku hiyo ya sikukuu unakuta vibao VYUMBA VIMEJAA,uliza wageni ni akina nani?

Ni John na Rukia. Au Abdallah na Rose(Ni mfano wa majina sijamlenga mtu yeyote hapa).Wote hawa wanasali na kufunga. Sasa niwaulize swali mlifunga kwa ajili ya nini?

Ndio maana Yesu amenituma akwenu nyinyi nyote mnatakiwa kutubu na kuacha dhambi,yeye hana dini ,ila nyinyi mlitenganishwa kwa dini ili msimjue Yeye wala kuzijua siri za Mungu na za Mbinguni.

Mmefichwa maksudi ili mpotee. Mimi sitaki mpotee maana nimeambiwa niwaambie kweli yote niijuayo. Mrudieni Mungu mpate kuurithi uzima wa milele. Jehanamu ni kubaya sana ndugu zangu,kuna mateso makali,mbaya zaidi hayana mwisho milele na milele ni moto tu.

MUNGU AWABARIKI SANA WATOTO WA MUNGU.

Kila nikitaka kuandika maombi au jinsi ya kuomba ninazuiwa. Ninaona tujifunze kwanza neno la Mungu halafu maombi yatakuja baadaye.Roho Mtakatifu hajanipa kibali.Ila uwapo katika mafungo yako.SOMA SANA NENO,SOMA MAANDIKO YATAKUPA NGUVU ZA KUISHINDA DHAMBI NDANI YAKO

JE,WANADAMU NDIO WANAOFUNGA TU?

Hapana,hata mizimu na majini huwa yanafunga ili yapate nguvu za kumshinda mwanadamu.

Wachawi hufunga pia ili wapate nguvu zaidi za kuwashinda wanadamu walio katika nuru, wengine hupikwa huko kuzimu kwa siku na majuma wakija juu duniani wanakuja na nguvu mpya ili wasimike utawala wao.

Mtu wa Mungu funga ili upate nguvu za kuwashinda maadui zako.

JE,KUFUNGA NI SAWA NA KUSHINDA NJAA?

Hapana,KUFUNGA ni dhamiri ya kweli ndani ya moyo wako ili uwe karibu na Mungu akupatie nguvu mpya za kuweza kulishinda jaribu.

Kufunga ni tofauti na kushinda njaa kwasababu, unashinda na njaa kwa kuwa huna jinsi ya kula,ila kufunga unakuwa na hamu ya kula na chakula unacho lakini unajinyima ili kuongeza kiwango chako cha imani.

Jinsi unavyojinyima kula chakula chako kitamu ndivyo unavyomuonyesha Mungu wako jinsi umpendavyo na kumtii.

JE,KUFUNGA PASIPO KUAMBIWA UFUNGE NI KAZI BURE.?

Ndiyo! Ndio maana nikasema unafunga kwa maelekezo ,na ukifunga kwa maelekezo huwezi kusikia njaa ya hovyo hovyo. Ila kama hujaambiwa kufunga, acha,maana utakuwa unajitaabisha bure kwa kujishindisha njaa na kuishia kukonda hata kuharibu mwili wako.

JE,WATOTO WANATAKIWA KUFUNGA?

Watoto hawatakiwi kufunga kwasababu hawajui walitendalo. Kufunga hakulazimishwi, ni hiyari ya mtu na maelekezo ya Roho Mtakatifu ili ampe nguvu za kulivuka hilo jaribu.

JE,NINAWEZA KUMUIGA MTU KATIKA KUFUNGA?

Usimuige mtu katika mambo ya kiroho kwa kiwango kizidicho imani yako.Msikilize Roho Mtakatifu anakuambia nini,kama atakupa mtu wa kukuelekeza katika mambo ya Mungu msikilize, ila ukiona unaelekezwa nje ya uwezo wa imani yako na moyo wako unasita usimfuate. Subiri kwanza huenda adui ameshamtembelea, omba muongozo wa Roho Mtakatifu naye atakusaidia.

Kama utagundua alikosea, usimlaani, usimseme kwa watu ili kuifichua aibu yake,usimcheke na kumdharau, usimpondee kwa watu wengine.Usimtuhumu. Yeye naye ni mtu tu kama wewe ana madhaifu yake.

Tena Kumbuka aliyokufundisha ni mangapi, aliyokuombea ni mangapi, aliyokusaidia kiroho na kimwili ni mangapi.

Kuweni na moyo wa shukrani na kuthamini uwepo wa kila mtu aliyekutendea mema maishani mwako.

Umemshauri hataki kubadilika. Jitenge naye na ukae kimya huku ukimuombea. Ipo siku neema ya Kristo itamsaidia na kuinuka tena.USIMSEME VIBAYA KUMBUKA ALIKOKUTOA.

HERI YA MWAKA MPYA.2024.

Sema ninavuka nikiwa mpya ,mambo yangu yawe mapya, kiroho changu kiwe kipya. Nilipoishia mwaka 2023,ndipo ninapoanzia mwaka 2024,sitarudi nyuma mpaka nikamilishe mipango yangu na kufanikiwa kusudio langu katika Jina la Yesu Kristo aliye hai.

Niwe mpya katika kazi,niwe mpya katika ndoa,niwe mpya katika elimu,niwe mpya katika biashara, nivuke vikwazo vyote nilivyokuwa nimewekewa na wachawi, niwe bora na siyo hafifu. Niwe na afya mpya kuliko mwaka jana,sitaki kuwa chini bali niwe juu kama jinsi ulivyo Wewe Mungu wangu wa mbinguni.

Sitaki kubaki nyuma,sitaki dharau,sitaki kunyanyaswa, sitaki, kuwa mpweke. Ninavuka kama ilivyoamriwa na mamlaka za mbinguni maana giza halina nafasi tena kwangu katika Jina la Yesu Kristo aliye hai.

Sema,ninajivua vazi lolote chafu nililokuwa nimevikwa na wachawi,ninalitakasa vazi jipya nililopewa na Yesu kwa damu yake ili liwe safi jeupe kama theluji, ili linipatie kibali kwa watu.

Watu wengi mmechafuliwa mavazi yenu ndio maana mkienda mahali mnaonekana hamjapendeza wala hamvutii hadi mnakosa fursa. Yatakaseni kwa damu ya Yesu hayo mavazi yenu ili yawe mapya na mpate kibali kwa watu.

Takaseni nyayo zenu zisiingie na uchawi wa mwaka jana kwenda kufanyika antenna mwaka kesho. Wengine mmefungwa miguuni antenna ili kila muendako muwe mnajulikana. Kateni hizo nira zote kwa upanga wa Yesu na muwe huru.

Jifunzeni kujitamkia baraka maana wachawi huwa wanawatamkia mikosi na nuksi na inawashika. Msiache kujibarikia maisha mazuri mwaka 2024.

Ingieni kwa kishindo kikuu maana kuanzia mwaka 2024 ni mwaka ambao Mungu anakwenda kuwapiga maadui zenu kwa mapigo ya mfululizo pasipo kukoma,watahangaika kuutafuta msaada lakini hawatafanikiwa maana watakuchukiwa na kila mtu.

Walichokitegemea hakipo tena.Sasa hivi ni KIPIGO TU.

Nami ,ninaachilia upako wa mwaka mpya uwafikie popote mlipo na baraka za Mungu zijae ndani yenu kwa wingi hadi muwabariki na wengine katika Jina la Yesu Kristo aliye hai.

HAPPY NEW YEAR,2024.
 
Am

Udhamirie kuacha kutenda dhambi.Usiwe kama ndugu zangu Waislamu na Wakristo. Wakiwa kwenye Ramadhani au kwa Resma, utakuta guest house zimeandikwa vyumba viko wazi.

Amen Mtumishi, ninapokea Upako wa wa mwaka mpya kwa Jina la YESU Kristo, barikiwa sana uzidi kutulisha chakula cha roho na maji ya uzima mwaka 2024. Happy New Year
 
Amen! Amen!Ahsante sana,Mungu akubariki pia katika mwaka mpya unaoanza kesho uwe mkuu kuliko maadui zako wote katika Jina la Yesu Kristo aliye hai.
 
Shalom! Matunda hutofautiana kati ya mtu na mtu,ila embe, parachichi, ndizi mbivu,mapapai, matikiti maji,korosho na karanga ni nzuri sana kwenye mfungo. Usile nanasi maana huwa linafanya "digestion" kwa haraka sana na linaweza kukusabishia gesi tumboni japo lina sukari ya kukupa nguvu mwilini. (DIGESTION,MMENG'ENYO WA CHAKULA TUMBONI).

Machungwa na machenza hapana,usile yana gesi.

Asali nayo ni nzuri, miwa ni mizuri haina gesi,hapa zingatia vyakula visivyo na jamii ya damu damu,na visivyopikwa. Isipokuwa karanga na korosho unaweza kula havina shida.

Maji ya vugu vugu unaweza kutumia asali badala ya sukari ya kiwandani na majani ya chai ili usipate kichefuchefu,na mwili uwe na nguvu ya kutosha.(Jitahidi iwe siku 7 utaona mwenyewe).Hii itakusaidia kunywa maji mengi zaidi kwa mtu ambaye hajazoea.

Ila kwa mzoefu wa kufunga,hii si kitu kabisa kwake. Mafungo yaendane na kiwango cha mtu cha imani yake,mtu akiweza kufunga siku moja sawa,mbili sawa,tatu na kuendelea ni sawa maana Mungu atamhesabia haki kwa kuwa anazo nguvu kidogo, na hatutakiwi kuwacheka wale wasioweza kufunga bali tuwaombee na kuwatia nguvu ili nao waweze kufunga kama sisi.Amen.
Mfungo unanguvu sana na unaupa mwili upako wa ajabu toka Kwa Mungu.....

Mimi mifungo mingi nilivyofanya nimepata majibu kabla haijaisha

Yani mfungo wa siku 7 unakuta siku ya 2 au 3 tayari nimefunuliwa...

Pia mwishoni mwa mwaka hapa nikasema nafunga siku 14 kwaajili ya mahusiano na maisha kiujumla....ajabu siku ya 6 nikapata maono yangu kidogo alafu roho mtakatifu akasema nifungue.... Nikafungua mwez wa 12 tarehe 1 nikapata picha halisi kuna kitu roho mtakatifu alinionesha na nikambishia akafunua kwangu kilakitu na kuniasa nisimdoubt Mungu wangu anaona ambavyo mimi sioni.

Sasa hapa naomba na wote tujue, kuna shida,matatizo, changamoto ambazo tupo nazo either tunazijua au bado Yesu kupitia roho mtakatifu huwa anaweza uzito moyoni au mwilini kuhusu Jambo husika inatakiwa uamini ile sauti au ule mguso na kuufanyia kazi.... Kuomba na kusoma neno ni muhimu ili kumruhusu zaidi roho mtakatifu aguse maisha yako na abadilishe pale penye kasoro..

Kuna mambo mengine atarekebisha bila hata yawewe kujua..

Kuna sisi ambao bado hatujaoa unakuta unampenda sana binti na unaenenda kwenye mstari lakini ghafla mnagombana au ghafla binti anakuwa anakukwepa basi... unaweza umia sana na kulaani unamkosi bila kujua Yesu anakuepusha na nini...

Kuna binti nilimpenda sana na nilikuwa kila nikipata muda naenda mlimani naomba Mungu "nisaidie Mungu huyu awe mke wangu, nitatulia nae Mungu, nitakurudishia sadaka na utukufu wako" ila ajabu sikuwahi pata viashiria vyovyote.

Nikaanza kuongea na Mungu kwa kuweka kama makubaliano "Mungu wa Mbinguni ukinipa huyu binti sitafanya hiki na nitafanya hiki na hiki" bado sikuona chochote..

basi kuna kipindi wiki 3 mbele nilikuwa nahisi tu binti anamtu wake huyu ila uhakika sina... kumbe bwana binti anamtu mwingine.. kunasiku huyo kijana akanitafuta na tukapanga kuonana siku ya kwanza akanielekeza pale akaomba kesho yake tukutane na huyo binti wote 3...

Basi kesho yake nimewahi kutoka kazini ilibidi tuonane saa 11.. nikaenda karibu na kanisa kusubiri muda nasubiri anitafute kuna roho ikasema nenda ingia kanisani...basi nikaingia kanisani nilivyofika nikakuta kuna neno na maombi... Kwanza tu kuomba nikapata uchungu sana,nikalia sana nikaumia sana nikaoneshwa sikuhiyo ugomvi ungezuka na roho ya mauti ilikuwa Kati yangu na binti Yani ni either kwenye ugomvi mimi ningepoteza uhai au binti angeweza dhurika na kupoteza uhai...

Nimekuja toka saa 1 akanitafuta kijana roho mtakatifu akanielekeza namna ya kumjibu yakaisha....Ila pia roho mtakatifu akasema namimi anajua naumia atanipa amani basi usiku nililala na maumivu ila asubuhi niliamka mtu mpya hamna maumivu wala mawazo kuhusu binti..

Yeye anasema kwenye Isaya 43:19 "Tazama, nitatenda neno jipya; sasa litachipuka; je! Hamtalijua sasa? Nitafanya njia hata jangwani, na mito ya maji nyikani"

Pia tutulie yeye anatujua na anajua hatima zetu ndio maana akasema kwenye Yeremia 1;5

"Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa"

Huu mstari huwa unanipa nguvu kuna muda kuna vitu au watu wanaondoka si kwasababu haufai au haustahili ila ni kwasababu Mungu anawaondoa kwa usalama wako mwenyewe.
 
Baraka ni kubwa iliyopo ndani yako mtumishi....nitoe ushuhuda kwako....kunasiku nilikuelezea ndoto flani ya kuota najificha chini ya maji tukajadili pia ukanielekeza maagano ya ukoo na jinsi ya kuomba basi usiku wa siku ile ile nikaota ndoto kuna mtu kama zombie nimemuudhi na amesimama na ndugu mkubwa wa upande wa Baba....

Nashukuru Mungu nazidi kua sana kiroho 7seven
 
Pia Mungu haangalii ubora wa kupangilia maneno katika kumuomba maana wengi wetu hatujui kusali...

Ila anaangalia nia na utayari wa mioyo yetu kumpokea ndio maana wengi huwa wanapokea nguvu ya roho mtakatifu na kuanza kunena baada ya kumkiri Yesu na kusema ASANTE YESU. AU NAKUHITAJI YESU

Pia tusiache kumtafuta madam anapatikana hawa hawa kina 7seven wanaweza kuwa sababu ya sisi kuingia mbinguni..

Nilipewa kitabu cha Good morning Holly Spirit cha Benny Hinn ushuhuda wangu kupitia kitabu kile nimejifunza vingi ila kitu kipya roho mtakatifu amezidi jaa ndani yangu

Kwasasa naweza kupiga magoti na kuinua mikono juu bila kusema chochote ila nikimtafakari Mungu and guess what baada ya muda roho mtakatifu anajaa kiasi ambacho najikuta naanza kunena kwa lugha kutoka ndani zaidi...

Pia nikiwa nanena kwa lugha naelewa vizuri sana na najua ninachosema wakati huo
 
Ushuhuda mzuri sana huu unajenga imani ya mtu kwa kiasi kikubwa. Bila shaka watu wengine wanabarikiwa. Huu mwaka utakuwa wa shuhuda kubwa kubwa kwa watoto wa Mungu kama jinsi tulivyoanza nazo.

Baraka za Mungu ziwe juu yako usiku na mchana, usipungukiwe katika maombi yako kwa kile ukiombacho katika Jina la Yesu Kristo aliye hai.

Yeyote asomaye ushuhuda huu naye akatendewe kama ulivyotendewa wewe katika Jina la Yesu Kristo. Amen.
 
Baraka ni kubwa iliyopo ndani yako mtumishi....nitoe ushuhuda kwako....kunasiku nilikuelezea ndoto flani ya kuota najificha chini ya maji tukajadili pia ukanielekeza maagano ya ukoo na jinsi ya kuomba basi usiku wa siku ile ile nikaota ndoto kuna mtu kama zombie nimemuudhi na amesimama na ndugu mkubwa wa upande wa Baba....

Nashukuru Mungu nazidi kua sana kiroho 7seven
Amen.Huyo huyo ndiye alikuwa adui yako katika roho.Ninadhani ulishamalizana naye.Mwaka wa shuhuda huu,Mungu azidi kukubariki kila uchao. Amen.
 
Asante Sana ndio mwaka wa ushuhuda huu nitaleta shuhuda nyingi maana nimejipanga kwenye vingi
Karibu sana.Shuhuda zinajenga sana imani ya mtu maana ndizo huwa zinamdhihirisha Mungu kwamba yupo,miujiza, uponyaji,ishara na maajabu,shetani, uchawi,asili ya uumbaji (nature) vyote hivi vinamdhihirisha Mungu kwa wanadamu.

Katika hayo yote ndipo tunapopata shuhuda kutoka kwa watu kama wewe hivyo unavyofanya na ulivyoahidi kutuletea shuhuda. Ubarikiwe sana.
 
Pia Mungu haangalii ubora wa kupangilia maneno katika kumuomba maana wengi wetu hatujui kusali...

Ila anaangalia nia na utayari wa mioyo yetu kumpokea ndio maana wengi huwa wanapokea nguvu ya roho mtakatifu na kuanza kunena baada ya kumkiri Yesu na kusema ASANTE YESU. AU NAKUHITAJI YESU

Pia tusiache kumtafuta madam anapatikana hawa hawa kina 7seven wanaweza kuwa sababu ya sisi kuingia mbinguni..

Nilipewa kitabu cha Good morning Holly Spirit cha Benny Hinn ushuhuda wangu kupitia kitabu kile nimejifunza vingi ila kitu kipya roho mtakatifu amezidi jaa ndani yangu

Kwasasa naweza kupiga magoti na kuinua mikono juu bila kusema chochote ila nikimtafakari Mungu and guess what baada ya muda roho mtakatifu anajaa kiasi ambacho najikuta naanza kunena kwa lugha kutoka ndani zaidi...

Pia nikiwa nanena kwa lugha naelewa vizuri sana na najua ninachosema wakati huo
Sawa sawa kabisa. Roho Mtakatifu anakuja ndani ya mtu kwa jinsi ambavyo Yeye hupenda. Ila kila mtu ana wakati wake wa kunena na njia zake za kumfanya anene kwa lugha.

Siku tukipata kibali tutakuja kuzungumzia somo la kunena kwa lugha kama jinsi ambavyo Roho Mtakatifu atapenda kutufundisha, maana kuna lugha ya Mungu ya mbinguni na kuna lugha ya kunena ya kuzimu ya shetani.

Watu wawe makini sana katika kunena kwa lugha wasije wakajikuta wananena lugha ya mapepo.

Ila kwa jinsi wewe unavyoiongelea ni Lugha ya kweli kabisa maana njia unazozizungumzia ndizo hizo hizo walio nazo wanenao kwa imani iliyo thabiti.

Halafu katika Lugha ya kweli kuna aina mbili za Lugha za kunena.

1.Lugha kutoka Mbinguni kabisa ambazo shetani hazijui wala hawezi kujua unaongea nini na Mungu.Hizi huwa zinaenda moja kwa moja kwa Mungu na unaongea naye mambo ya sirini.

2.Kuna kunena Lugha za hapa hapa duniani. Yaani mfano sisi Watanzania tunaojua Kiswahili tu,sasa katika kuomba unaweza kushangaa unaanza kuomba kwa Kiispaniola, Kijerumani,Kiarabu,Kigiriki, Kiebrania, Kifaransa,Kizulu n.k

Ukishamaliza kuomba unakuta huwezi kuongea neno hata moja la hiyo lugha ambayo ulikuwa ukinena.

Halafu ninaona una karama ya maombi ya toba na rehema ndio maana unaomba huku ukiwa umepiga magoti na kuinua mikono juu,wengine huwa hawawezi, wataomba huku wakitembea tembea, wamelala (hawa ni waombolezaji),umesimama huku umekuja ngumi au kushika upanga katika imani(hawa ni wa vita).wengine wameweka mikono vifuani (wanaganga mioyo iliyojeruhiwa).

Pia unapenda watu watubu maana ndio huduma yako kuzungumzia Unyakuo, maana mtu hataenda mbinguni bila kuwa na toba ya kweli.Ni huduma nzuri ya Kristo iko ndani yako.Mungu akubariki sana.

KUNENA KWA LUGHA NI KIPAWA CHA ROHO MTAKATIFU KAMA VILIVYO VIPAWA VINGINE VYA ROHO MTAKATIFU.
 
mfumo wa maisha yetu, umekushape uamini hivo, unachokiona changamoto ni illusion sio uhalisia wa maisha yetu, maisha unayoahidiwa kuyaishi heaven ktk maandiko, ndo maisha halisi unapaswa kuyaishi sasa. Endelea kujifunza soon utakua bora zaidi.
This can't be possible unless uweke facts zinazojitosheleza na sio hisia binafsi
 
Back
Top Bottom