Jifunze practical electronics Comparators(viling anishi)- part I

Jifunze practical electronics Comparators(viling anishi)- part I

Transistor

JF-Expert Member
Joined
Aug 8, 2013
Posts
1,061
Reaction score
1,640
COMPERATORS (VILINGANISHI)
Comparator ni nini?

Kama jina lake linavyo jieleza comparators(vilinganishi) ni tendo la ulinganish linalofanywa na vifaa vya vya kielectronic vinavyoitwa OPAMP.

Vifaa hivi vinafanya kazi ya kulinganisha kati ya voltage rejea(voltage isiyo badilika badilika) na voltage inayo badilika (variable voltage).
Mfano:-

Kwa kuwa katika Electronics tunajihusisha na viwango tofauti tofauti vya voltage na current Ambavyo viwango hivi vinabadilika badilika kutokana na Sababu mbalimbali hivyo Comparators zimekuwa muhimu sana kwetu wabunifu na wana-electronics kwa ujumla pale tunapotaka kulinganisha voltage mbili tofauti ili tuunde tendo fulani linaloakisi mabadilikohayo.

OPAMP zipo nyingi za aina tofauti tofauti.Lakini mimi nitajaribu kuielezea IC LM741 Kwa kuwa inapatikana kwa wingi hapa kwetu Tanzania,hivyo hata kama utataka kufanya practical itakuwa rahisi kwako kuipata.



Hii ni OpAmp IC ambayo unaweza kuitumia kama comparator Kama tutataka kuitizama graphically with pin out LM 741 itaonekana hivi;-

Tuitambue miguu ya IC hii kazi zake na connection zake:-
Mguu namba 7
Huu ni mguu ambao ni Chanya( + ) unaungwa moja kwa moja kwenye chanzo chako cha umeme kati ya volt 5vdc hadi 15vdc upande wa chanya.


Mguu namba 4
Huu ni mguu ambao ni Hasi( - ) unaungwa moja kwa moja kwenye chanzo chako cha umeme kati ya volt 5vdc hadi 15vdc upande wa hasi.


NB LM 741 inahitaji nguvu ya umeme ili ifanye kazi inayokusudiwa,hivyo mguu wa 7 na 4 nikwa ajili ya kuiwasha IC ili ianze kufanya kazi.Katika IC hii unaweza kuingiza voltage kati ya 5VDC hadi 15VDC.


Mguu namba 2 na Mguu namba 3
Hii ni miguu inayofaya majukumu makubwa mawili kwa kubadilishana.
Ninamaanisha kuwa mguu namba 2 unaweza ukatumia kuingiza voltage rejea au kuingiza voltage inayo badilika vivyo hivyo kwa mguu namba 3.


JINSI YA KUPATA VOLTAGE REJEA

1. Ili kuipata voltage rejea(voltage isiyo badilika) tunahitaji kuwa na sakiti itakayo tutengenezea aina hiyo ya Voltage.Sakiti hii inaitwa VOLTAGE DIVIDER.

Kazi ya voltage divider ni kugawanya voltage inayozalishwa na chanzo cha umeme kwa 2.

Mfano chanzo chako cha umeme kina volt 12VDC ukigawa kwa 2 utapata 6VDC. Hii 6VDC ndiyo itakuwa Voltage rejea. Ili voltage divider igawe Voltage katika kiwango cha nusu huhitaji RESISTORS mbili (fixed resistors) zenye ukinzani sawa ambazo huungwa series na kuunganishwa parallel na chanzo cha umeme.

Katika muungo wa hizo resistor mbili ndiyo utapata nusu voltage ya power supply.
Mfano wa Voltage Divider ni kama ufuatao;-


ITAENDELEA..................

Kwa elimu zaidi ya electronics bonyeza HAPA
 
Back
Top Bottom