Jifunze namna ya kupokea matukio

Jifunze namna ya kupokea matukio

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Posts
8,809
Reaction score
15,438
images

Kwa kawaida tukio lolote likishatokea katu hatuwezi kulibadilisha, hiyo ni moja, lakini la pili ni kwamba tukio likishatokea ni sawa na mzoga, sidhani kama kuna mtu kati yetu anaweza kukesha usiku kucha kujaribu kuufufua mzoga, ni kujisumbua bure na kujiweka katika wakati mgumu zaidi kwa kutaka kujaribu kitu kisichowezekana.

Tunachotakiwa kufahamu ni kwamba, matukio ni sehemu ya maisha, matukio ni maisha, bila matukio maisha yatapoteza ladha, yatakosa maana.

Ukweli ni kwamba, hatuna uwezo wa kukataa matukio kwani kwa kufanya hivyo tunakataa maisha na hivyo kupelekea maisha yetu kuwa magumu sana. Matokeo yake tunajikuta hatuna furaha, hatuna amani na hatuna ridhiko. Tukio lolote linapokuja kwako, ina maana kwamba suluhu yake unayo, kama huna haliwezi kuja.

Unachotakiwa ni kuachana na mazoea uliyoambiwa na wazazi wako, jamii na marafiki kwamba, kuna matukio mabaya na mazuri. Ukweli ni kwamba matukio yote ni ya kawaida au mazuri. Mfano uliambiwa na wewe ukaamini kwamba -kuibiwa ni kubaya, kufeli mtihani ni kubaya, kufukuzwa kazi ni kubaya n.k. Lakini ubaya wa matukio haya ni upi?

Katika hali halisi ni kwamba, kila tukio lina pande mbili, tatizo ni kwamba upande wa pili huujui, unajua upande mmoja tu ambao ni mbaya. Mfano, unapofukuzwa kazi, kwanza kubali kwamba umefukuzwa, unastahili kufukuzwa, usiseme umeonewa kwani kila tukio lina sababu njema kwako hata kama kwa mazoea ni tukio baya, kiuhalisia hakuna tukio baya, tatizo liko kwenye tafsiri uliyowekewa, uliyopewa na kufundishwa na wazazi au jamii.

Mawazo yako yote yaweke kwenye kupata kazi, jiambie kwamba, sasa utapata kazi nzuri, yenye mshahara mkubwa zaidi, na yenye marupurupu mengi zaidi. Au jiambie sasa umepata muda wa kutosha kufuatilia mambo yako mengine zikiwemo biashara zako.

Achana na kuwaza upande wa pili kwani huuhitaji, lakini watu ndivyo wanavyoishi, inapotokea amefukuzwa kazi, akili yake na mawazo yake yanatawaliwa na mambo yafuatayo- nitaishije hapa mjini, nitakula nini, watoto wangu watakula nini, mke wangu ataniacha, mwenye nyumba atanifukuza, watu watanidharau… kwa kuwa unatumia nguvu nyingi kuwaza haya, mwisho wa siku yote yatatokea.
 
Umesema sahihi kabisa shem.......
Kupokea tukio ni one step ya suluhisho (kama ni "baya", au la kawaida kama ulivyoliita)
 
Ukianguka KOSA lao, ukishindwa kunyanyuka ni kosa LAKO!
Ukiwa na baba mzazi maskini hiyo ni kazi ya mungu, ukiwa na baba mkwe maskini huo ni uzembe wk!
 
Kweli mkuu Mtambuzi bado tunarudi kule kule kua akili yetu inatengeneza matukio yajayo
 
Last edited by a moderator:
images

Kwa kawaida tukio lolote likishatokea katu hatuwezi kulibadilisha, hiyo ni moja, lakini la pili ni kwamba tukio likishatokea ni sawa na mzoga, sidhani kama kuna mtu kati yetu anaweza kukesha usiku kucha kujaribu kuufufua mzoga, ni kujisumbua bure na kujiweka katika wakati mgumu zaidi kwa kutaka kujaribu kitu kisichowezekana.

Tunachotakiwa kufahamu ni kwamba, matukio ni sehemu ya maisha, matukio ni maisha, bila matukio maisha yatapoteza ladha, yatakosa maana.

Ukweli ni kwamba, hatuna uwezo wa kukataa matukio kwani kwa kufanya hivyo tunakataa maisha na hivyo kupelekea maisha yetu kuwa magumu sana. Matokeo yake tunajikuta hatuna furaha, hatuna amani na hatuna ridhiko. Tukio lolote linapokuja kwako, ina maana kwamba suluhu yake unayo, kama huna haliwezi kuja.

Unachotakiwa ni kuachana na mazoea uliyoambiwa na wazazi wako, jamii na marafiki kwamba, kuna matukio mabaya na mazuri. Ukweli ni kwamba matukio yote ni ya kawaida au mazuri. Mfano uliambiwa na wewe ukaamini kwamba -kuibiwa ni kubaya, kufeli mtihani ni kubaya, kufukuzwa kazi ni kubaya n.k. Lakini ubaya wa matukio haya ni upi?

Katika hali halisi ni kwamba, kila tukio lina pande mbili, tatizo ni kwamba upande wa pili huujui, unajua upande mmoja tu ambao ni mbaya. Mfano, unapofukuzwa kazi, kwanza kubali kwamba umefukuzwa, unastahili kufukuzwa, usiseme umeonewa kwani kila tukio lina sababu njema kwako hata kama kwa mazoea ni tukio baya, kiuhalisia hakuna tukio baya, tatizo liko kwenye tafsiri uliyowekewa, uliyopewa na kufundishwa na wazazi au jamii.

Mawazo yako yote yaweke kwenye kupata kazi, jiambie kwamba, sasa utapata kazi nzuri, yenye mshahara mkubwa zaidi, na yenye marupurupu mengi zaidi. Au jiambie sasa umepata muda wa kutosha kufuatilia mambo yako mengine zikiwemo biashara zako.

Achana na kuwaza upande wa pili kwani huuhitaji, lakini watu ndivyo wanavyoishi, inapotokea amefukuzwa kazi, akili yake na mawazo yake yanatawaliwa na mambo yafuatayo- nitaishije hapa mjini, nitakula nini, watoto wangu watakula nini, mke wangu ataniacha, mwenye nyumba atanifukuza, watu watanidharau… kwa kuwa unatumia nguvu nyingi kuwaza haya, mwisho wa siku yote yatatokea.

excellent lesson!

Huyu mwenye ID ya
SUPU YA MAWE, asipojifunza kitu hapa, ameisha.

Sijui kwa mganga ameshapeleka yule kuku mweusi!!!!!!!!!!!!!
 
mtambuzi tunarudi palepale kwenye soma la meditation.....!!!kama ulivyo oleza kiundani katika lile soma nadhani jamii tukiishi hapo wengi wetu hatuta kuwa na hofu ya kesho...
 
somo zuri mtambuzi tangu nijifunze kutoka kwako jinsi ya kuwa positive mahali ambapo mtu alitarajia niact negative maisha yangu ni simple
huwaga sikurupuki kabisaaaaa sitabiriki from now yaani hii kanuni ni nzuri sana
 
Back
Top Bottom