Nanaa
JF-Expert Member
- Dec 26, 2012
- 5,893
- 3,711
Umesema ukweli, mimi nina ushuhuda wa kaka yangu wa damu;
Kaka yangu alifeli vibaya mtihani wake wa kidato cha sita, kwa alama alizopata asingeweza kuchaguliwa kujiunga na elimu ya juu, alisoma Combination ya PCB. Kila mtu alijua kwamba ndoto yake ya kuwa daktari imeishia pale.
Lakini hakukata tamaa, aliomba Chuo kwa kutumia vyeti vya kidato cha nne na kwa kuwa alikuwa na matokeo mazuri alipata chuo na akasoma Clinical Officer.
Wakati yuko mwaka wa pili chuo Baba akafariki, maisha yakabadilika, no support kutoka kwa ndugu yoyote na kaka angu ndo mkubwa.
Mungu akajaalia akamaliza chuo na akaanza kusupport familia, tukasahau machungu, akawa ndo baba wa familia.
Sasa kuna wakati huwa najiuliza, hivi angefaulu, angepata chuo Muhimbili, miaka mitano angeweza kweli kumaliza chuo? Nawaza labda angedisco kwa stress za familia na boom.
Lakini yeye alitafuta alternative and he is a doctor now na ana mshahara mzuri kuliko mimi niliyeunga elimu ya juu moja kwa moja.
Kuanzia hapo nimejifunza kila linalokufika lina sababu. Tumshukuru Mungu kwa yote.