Jifunze kwa kuangalia ndoa zilizofanikiwa

Omela Odongo

Member
Mar 26, 2021
47
66
Salamu Wana jukwaa.

Niende kwenye maada moja kwa moja,kama unavyojua kwa wale tuliozaliwa vijijini mwanzoni mwa miaka ya sabini mpaka mwanzoni mwa miaka ya themanini.Shule za sekondari zilikuwa chache kwa hiyo waliochaguliwa kutoka shule za msingi kwenda sekondari walikuwa wachache mno wengine wote ilikuwa kurudi nyumbani.

Na kwa kijana wa kiume na hata wa like kama hukuchaguliwa kujiunga na elimu ya sekondari kilichobaki kwa maisha ya kijijini ni kuoa au kuolewa.Sasa Mimi baada ya kurudi kijijini sikuoa maana sikuona ndoa ambayo ilikuwa kielelezo cha kunifanya nioe mapema,maana ndoa nyingi zilizokuwa karibu yangu yalikuwa ni majanga tupu,kwa hiyo nimekaa miaka mingi bila kuoa.

Nakumbuka ndoa moja jirani yetu ilikuwa ni ugomvi kila siku Wala wanandoa ilikuwa ni kabila moja kutoka Kanda ya ziwa ambao ni wataalamu wa kutumia upanga kama silaha ya kujihami,

Sasa ilikuwa mwanaume akiwahi upanga mapema siku hiyo mwanamke atapigwa vibaya sana,lakini siku ambayo mwanamke atawahi upanga Basi siku hiyo ni kipigo kwa mwanaume kiukweli ndoa hiyo ilinifanya wazo la kuoa nilisogeze mbele kama vijana wengi Leo wanavyojiapiza kuwa hawataoa baada ya kushuhudia changamoto nyingi kwenye ndoa za Leo.

Kwa nyakati za Leo kijana anaweza akaishi bila kuoa kwa sababu kama unaweza kupata maziwa bila kufuga ng'ombe sasa unafuga ng'ombe wa nini?Enzi zetu bila kufuga ng'ombe maziwa yalikuwa hayapatikani kabisa.

Sasa baada ya kuona changamoto nyingi katika ndoa chache zilizokuwa karibu yangu nilidhani ndoa zote dunia ziko hivo,lakini baada ya kuanza kutembea huko na huko nilianza kukutana na wanandoa wanaoishi kwa amani kabisa kuna ndoa moja ambayo ilinisababisha nibadili mawazo kuhusu kuoa.Wanandoa hao waliishi kwa amani sana na sikuwa nimewahi kuona maana kuanzia kwa wazazi ilikuwa ni shida tupa,mpaka siku moja niliwauliza wanandoa hao ni nini Siri ya kuwa na ndoa nzuri Tena yenye amani? Walinieleza mambo mengi lakini kubwa zaidi waliniambia kuwa kuwa na ndoa nzuri na imara inategemeana na msingi wa ndoa yenyewe.

Ndoa za vijana wengi Leo ni changamoto kwa sababu hata misingi yake ni mibovu,Leo vijana wengi wanafanya uasherati wakiwa wamejificha kwenye kichaka kinachoitwa mahusiano unategemea kupata ndoa imara hapo! Kumbuka ndoa iliyoanzia baa,disco,Chuo n.k itaishia huko ilikoanzia.lakini pia ni mugumu kujifunza kupitia ndoa ZILIZOFANIKIWA ndoa za namna hiyo zipo kamwe tusiangalie ndo zilizoshindwa.

Nimeona niwashirkishe uzoefu wangu kidogo katika ndoa Mimi mhenga nikiwa ninatimiza miaka ishirini kwenye ndoa asikwambie mtu ndoa no nzuri sijawahi kujuta tangu nioe mke wangu ni zaidi ya rafiki.Samahani kwa uandishi wa kihenga lakini hata hivyo kuna la kujifunza.

Nawasilisha.
 
Bora ulivyojitetea huko mwisho maana umejua kubandanisha Mzee

Sawa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom