Nikufundishe kutunga hadithi? Ili kutunga hadithi unatakiwa uwe na kisa, uwe na wahusika pia uwe na mandhari na lugha. Sasa hapo unaanza kutunga matukio muhimu. Mfano Musa atazaliwa kwenye familia ya wafugaji, atapata vikwazo vya kwenda shule, Musa atafanikiwa kwenda kusomea uhandisi Ufaransa, Musa atarudi nchini na kuwa kiongozi mkubwa wizarani. Musa atageuka kuwa fisadi. Musa atafungwa jela miaka mitano. Mwalimu atamchapa viboko vitano wakati anaingia, na vitano wakati anatoka.
Ukishapata kisa unaanza sasa kujazia nyama.
Mfano, ilikuwa ni jumapili iliyojawa na misukosuko wakati basi la Twende kazi lilipowasili dare s salaam. Basi hilo liliwahi kufika kidogo kutokana na uwepo wa mapolisi wachache barabarani. Misuko suko ya jumapili hii ilisababishwa na watu wengi waliokuwa kwenye mizunguko yao huku wakijitahidi kumaliza siku na kuwahi usafiri ambao pia ni wa kusumbua. Usafiri unasumbua kutokana na kuchangiwa na foleni…
Unaona. Yani unaaza kuielezea jumapili, unakatisha kidogo, unaanza kulielezea basi alilokuja nalo Musa, mara uanrudi kwenye jumapili tena, unaikatisha unaanza kuielezea foleni… Kwa mtiririko huu, unaweza hata kuandika kurasa mia za hadithi bila hata kufikia mwisho wa tukio…