CHIEF MP
JF-Expert Member
- Jul 6, 2011
- 1,559
- 680
KAMA NI NJIA NZURI NAWE ICHUKUE IFANYIE KAZI!!
Mama yangu aliwahi kunyanyaswa sana, aliwahi
kudharauliwa sana .wakasema maneno mabaya
juu yake .wakamsemea familia yake.
Waliomsema walitegemea kuwa atawajibu, au
ataanza kulia na kutangaza kwa watu kuwa
anaonewa lakini la hakuwahi kulalamika.
Lakini alipojifungia ndani akiwa nami mtoto wake
alilia sana yaani alikuwa analia kweli kweli.
Siku moja nilimuuliza.
Mama mbona ukiwa nje unacheka tu na watu,
kila mara una tabasamu? Ukifika ndani unalia
usiku kucha?
Mama akalazimisha tabasamu kisha akanijibu.
Najilazimisha kufurahi ili adui yangu atambue
kuwa kero zake haziniumizi, maneno yake ni bure
kwangu hayaniathiri hata kidogo ..kwa kufanya
hivyo mimi nakuwa mshindi na mwisho adui
anakosa mbinu za kuniumiza zaidi .NALIA mbele
yako maana wewe unanifahamu, na hapa uelewe
kuwa naumia kweli kweli maneno yao ni makali
sana zaidi ya miiba, yananipondaponda moyo na
kunikatisha tamaa lakini sitaki wajue. Wakijua
watakutana kupongezana ..sikiliza
mwanangu ..USIJE UKAMPA NAFASI ADUI
AKAGUNDUA UDHAIFU WAKO .KAMWE USILIE
MBELE YA ADUI
Kwa miaka ile sikumuelewa .ilipita miaka
kadhaa nikaingia katika mahusiano ya
kimapenzi baada ya muda mpenzi wangu wa
kwanza kabisa tangu nijitambue aliniacha kisa
siwezi
kumuhudumia..na kweli sikuwa naweza
kumuhudumia .nilikuwa maskini wa kipato na
hakuwa tayari kunivumilia akaamua kuniacha
na kuwa na mtu mwingine ..nikayakumbuka
maneno ya mama enzi zile .
Kila siku nikawa mtu wa kutabasamu kila
nilipoonana nae akiwa na furaha na mpenzi wake
mpya, furaha ikazidi, alijaribu kunionyesha mambo
mengi na mpenzi wake mpya lakini sikuonyesha
kushtuka wala kuumia mbele yake.
Kitanda changu na godoro langu pekee vilitambua
ni jinsi gani nilikuwa nalia usiku, nililia bila mtu
yeyote kuona.
Moyo ulipondeka nikayachukia mapenzi lakini haya
yote adui yangu hakuyajua
Mwisho akajiona mjinga .akaacha madharau.
Na hatimaye waliachana na bwana yule mwenye
mbwembwe.
Aliporejea kwangu, moyo wangu ulikuwa umekufa
ganzi tayari ..sikumpa nafasi ..sikumpa nafasi
kamwe.
Ile hali ya yeye kunibembeleza kila siku, moyo nao
ukaanza kupona ..
HAKUWAHI KUJUA KAMA NILIWAHI KUMLILIA
AKAWA MJINGA AKANILILIA HADHARANI.
Nilifurahi na kumsikitikia, natamani angeyajua
maneno yale matamu ya mama yangu huenda
angeyashinda maumivu yake.
NAKUKUMBUKA SANA MAMA.
NB: Kama ni njia sahihi kukabiliana na adui
yako ..ichukue na mshirikishe mwenzako!!"