Jifunze kukaa kimya

RuwaIkunda

Senior Member
Nov 2, 2017
156
279
USIITANGAZIE DUNIA MATATIZO YAKO"

Unapokuwa na matatizo kila mtu hutaka kujua unatatizo gani akiwa na lengo lake moyoni. Je huwa tunajipa muda wa kutafakari aina ya watu amabao tnawasimulia matatizo yetu? Tambua kwamba :- -

1. Kuna ambaye anataka kujua ili akupe msaada.

2. Kuna ambaye anataka kujua ili akasimulie wengine.

3. Kuna ambaye anataka kujua ili akucheke.
Kuna mwingine anataka kujua ili tu asikitike na kuhuzunika.

4. Jifunze kuficha matatizo yako , siyo kila mti unapaswa kumsimulia matatizo yako. Kumbuka kila mtu ana matatizo hapa duniani hata kama awe tajiri vipi lazima atakuwa naatatizo, hata awe mlokole naye pia ana matatizo. Kuweka juhudi za kumsimulia kila mtu haitakufanya utatue matatizo yako badala yake inaweza kukufanya uaibike katika jamii.

Chagua mtu ambae unahisi anaweza kukusaidia kukupa suluhisho la matatizo yako na siyo lazima awe rafiki yako anaweza kuwa mtu mgeni kabisa kwako na akakupa ushauri mzuri wa kujenga. Jifunze kukaa kimya , ongea inapobidi.

NAWATAKIA SIKU NJEMA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom