Jifunze Kiswahili cha Kongo Mashariki

.......... Muendelezo wa somo letu la jana

Yulu............ juu mfano uikae kule yulu maana kaa kule juu
Mbegete----- Ndoo
Chungu ------sufuria
kopo-----------Kikombe
Kilauri----------Bilauri
Zamu ---------mlinzi
Siku ya posho-----Jumamosi
Siku ya Mungu----Jumapili
Siku ya kwanza---Jumatatu
Siku ya pili----------Jumanne
siku ya tatu--------Jumatano
Siku ta ine--- Alhamisi
Siku ya Tano-------Ijumaa
Utalungula----------utaungua
Mapapa-------------ndala au kandambili
Mkaba---------------Mkanda
Shemizi--------------shati
Jipe------skirt
shapo------Kofia
Kiwelewele---hamnazo au mwehu
Wazanga------hamnazo au mapepe
Maziba---------matiti
Shushu--------maziwa fresh
maziwa/kivuguto----mtindi
Makumi mbili----ishirini , nakuendelea mpaka mia moya ndio mia moja
Petrole ----mafuta ya taa
Mazutu--dieasel
Petrol--essense
mayi----maji




Sentesi fupi fupi

-Chef umwe mimi niko na makosa kama njo vile basi unikilie uruma nilizani nimenyangula bien kumbe nimekosea... nisikilie uruma papa
- Si ukuye kunyumba niko na lazima na weye-----si uje nyumbani ninakuhitaji
-sa mbona unanipita kama unijue-kuya karibu kuna chenye nataka kukuambia au unazani nataka kulomba kitu
-nawewe ukatale wewe kila kitu dako tu---nawewe ukatae kila kiitu yes tu?
-jana nimekunya sana pombe
-kesho ulete mavi na mkoyo---hawana tafsida ni kavukavu tu
-koyola niende busiku bunaingia---?????? hapo mtajaza wenyewe
 
Kutomboka=kuongea

Kwahiyo Ukitaka Kusema Naongea Na Serunkuma Ajiunge Na Lubolo Utasemaje Mkuu? Naomba Unijibu Haraka Sasa Hivi Kwani Nataka Nimuunganishe Huyo Mchezaji Na Wakala Wa Kikongo. Nitashukuru!
 
masasi=risasi
mbo (bon)= eeeh...., sasa....
kuya uku= njoo huku
usipime!=usijaribu!
makumi mamoya, makumi na bili, makumi mawili, makumi manne, makumi manane= 11, 12, 20,40,80
 
Solola bye=angalia vizuri
Toseka moke=Tucheke kidogo
Fasi ya kuwesee=Kiungo cha kutolea haja kubwa
 
Kutambuka. = kuvuka
Magharibi =kuanzia saasita na kuendelea mpaka jioni
Kutambuka ni neno la kawaida tu, yaani kupita juu ya kitu. Mfano tambuka reli maana yake pita juu ya reli.

Mi nikiona Wakongo napenda sana kusikiliza coz wanaongea kile Kibantu chenyewe hasa kama Kiswahili cha zamani ambacho hufanana kwa karibu na lugha ya kabila letu ukanda wa Pwani.
 
Hahaha hiyo mwanzo umeniacha ila zingine zote nimeng'amua. Lugha inafanana na kilugha chetu.

Koyola niende busiku bunaingia.....kojoa niondoke (niende) usiku unaingia
 
Munyama mukwenda akili mukuya

-Mnyama akiondoka ndipo akili inakurejea.

Yaani: Tumia fursa kadiri inavokujia, ili usijute baada ya fursa hiyo kutoweka.
 
Wacongo Wakitaka Kumuuliza Kama Mtu Ameshiba Chakula Wanasema Umeenea? Mbaraga/malaya Kurumbata/kuwinda Milomo/midomo Licho/jicho Mugulu/mguu Mulibo/koo.Koromeo Liziba/ziwa(titi) Udongo/bulongo Uji/buyi Uongo/bongo Mkaa/makala Kiatu/kiatu Naishia Kwa Pale Banduku Tukutane Kumangaribi Tutaongea Bya Mingi
 
Chunga mbele - Subiri au ngoja kidogo ;Mangharibini - Hutumika kama salamu ikimaanisha Habari za jioni; Kusim - kupiga simu ;Umeteswa weye - Una shida wewe.
 

Batoo - meli

yulu - juu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…