Jifunze Kiswahili cha Kongo Mashariki

msumeno

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2009
Posts
2,826
Reaction score
1,738
Tunaanza bila kuchelewa

Kukoropa---------- Kupiga deki
Kunya---------------Kunywa
Mbele----------------Kabla
Kugoma-------------Kunyoosha nguo au kupiga pasi
Kinono---------------Kongolo
Sombe----------------Kisamvu
Lengalenga-----------Mchicha
Kunyamba-----------kwenda haja kubwa
Fufu-------------------Ugali
Kuya------------------Kuja
Kupiga-----------------Kupika
Koyola----------------Kojoa
Mbio-------------------Upesi
Tosha-----------------Toa
Nyangula-------------Nyenyua
makaku---------------Kima/nyani
Soso-------------------Kuku/hii pia ni lingala
Kunyumba------------Nyumbani
Fungula----------------Fungua
Njo vile-----------------ndio hivyo
Nisiikilie huruma-------nisamehe
Pika---------------------piga
Njala---------------------njaa
Ndazi-------------------andazi
Kasamunyu-----------Ndizi za kupika
Ndizi-------------------ndizi kisukari
Bitika-------------------Ndizi mbivu
Tate-------------------bibi au babu
Mloko yangu---------mdogo wangu
Malofu------------------pombe/ulabu
Kanyanga-------------gongo

kesho maneno mengine kibaaao
Chanzo: Wikipedia
 
Last edited by a moderator:
Mkuu asante kwa thread ya kufurahisha. Mimi ni mmoja ya watu wanaofurahishwa sana na kiswahili cha Kongo. Naomba kama una nafasi utuandikie wanavyoongea... kwa sentensi ndefu na maana zake kwa kiswahili. Kwa mfano nilisikia wanaambizana ''nakwenda kunyama''. Wakiwa na maana ''nakwenda kununua nyama''.
Cheers!
 
batu = watu
fasi = mahala

Sentensi:
Batu ba Tanzania banasema kiswahili kila fasi.

Ni mimi yule yule anyeongea kiswahili kikenya.Nawasilisha.
 
Nimecheka sana hio ya "Njo Vile...."
 
Kutomboka ni kukasirika
 

Kununua wansema kuuza... mfano niuzie bia hapa anakua anasema ninunulie bia
 
Siyo kunyamba ni Kuyamba
 
Nini maana ya....... Ekotite?
okoti te maana yake haijatoka.... kota toka okoti imetoka te ni negative form ya kila kitu mfano nalingi yo te maana yake sikupendi nalingi yo maana yake nakupenda.... sasa kwenye ule wimbo inamaanisha picha haijatoka
 
"Nguvu ya mamba kumayi" Nguvu ta mamba majini.

Nzambe na bomoyi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…