Loveeness78
JF-Expert Member
- Oct 9, 2016
- 280
- 294
Tazama mungu alivyo mwema amewapa uzima hadi sasa!
Toka nimekuwa katika mahusiano nimejifuza kuwa kupenda haitoshi kuwa na hisia kali na kuthamini unaempenda tu!
Nimejifunza kwamba unapodenda unaanza kuingia ulimwengu wa elimu, yaani kuanza kumsoma yule umpendae.
Katika hatua za awali utaangalia vitu vichache ambavyo vitakulidhisha kuingia lasmi katika mahusiano na huyo unaempenda.
Tunapo kosea.
Tukumbuke sisi binadamu sio static twaweza kubadilika kila mara kutokana na mambo mbalimbali. Unaweza kunifahamu kuwa Loveness hapendi kelele ila kesho ukanikuta sehemu nipo kwenye kelele tena mie ndio mpiga kelele maarufu mahari hapo!
Kusema hivyo nataka kumaanisha kuwa yawezekana mapenzi hayana formula!
Mimi nimejifunza kuwa ili tudumu pamoja na tuwapendao inabidi mimi nijifunze kuishi vitu ambavyo unapenda na wewe pia ujifunze kuishi vitu ambayo napenda. Sasa utakuta mmoja wetu yeye anataka umadapt yeye tu, lakini yeye hataki kukuadapt! Kila siku anakulaumu " ina maana miaka yote hiyo tuko wote hunijui tu mwanamke/ mwanamme gani hujui kujiongeza?"
Pia tujifunze kuwarahisishia wenzetu kutujua, na hata unapokuwa tofauti utoe nafasi ya kusomeka, ili mwenzio anaekusoma kila siku aweze kukuelewa kuwa leo hesabu zimebadilika ili nae aweze kucheza ngoma yako kwa siku hiyo.
Katika yote tukiweza kuvumiliana tunafika mbali, maana kujifunza kuishi na mtu aliepitia mengi kabla hamjakutana ni ngumu, tusipende kuona kuwa tunao wapenda ndio wajifunze kuishi nasi tu ila nasi tujifunze kuishi nao kwa uvumilivu.
Kila siku mwenzio yuko tofauti na jana, pia yuko tofauti na mwingine uliewahi kumjua kabla!
Note:
Kila siku ni mpya na ushauri wa leo unaweza usifanye mabadiliko kama uliyofanya jana, au ukafanya kwa rafiki yako ila kwako usibadilishe chochote, na ndio maana hatuwezi kuandika kanuni za mahusiano na kuzibandika ukutani mwa vyumba vyetu.
Daima jifunze kuishi vitu avipendavyo mwenzio na yeye ajifunze kuishi vitu uvipendavyo. Pia rahisisha maisha, hakuna apendae mtu mwenye misimamo mikali isio na maana.