Jiepushe na mtego huu katika familia

Jiepushe na mtego huu katika familia

Billionaire wa Betting

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2022
Posts
1,104
Reaction score
2,208
Wakuu,

Kumekuwa na utaratibu hasa kwa familia zinoishi mijini na zenye uchumi mzuri , kukusanya nguo zilizovaliwa na wanafamilia kwa kigezo kwamba hawazihitaji tena na baadae kuwapelekea baadhi ya ndugu vijijini. Huu kwa baadhi ya familia ni mtego mkubwa sana kiroho.

Sio Kila ndugu anafurahia mafanikio ya ndugu mwingine na sio Kila familia inafurahia mafanikio ya familia nyingine katika ukoo.

Jiepushe sana na hili kwani kuna baadhi ya ndugu wanaweza kutumia nafasi hiyo kuzifunga familia nyingine kiroho(roho wa Giza) yaani mnawapelekea nguo ambazo mlikuwa mnazivaa na nguo hizo hizo znatumiwa na ndugu wenye wivu, chuki nk kufanya vifungo vya kiroho ambavyo vinaweza kuja kuleta mabalaa ndani ya familia.

Pia jiepusha na tabia ya kuvaliana nguo, sio Kila unayevaliana naye nguo ni mtu safi.

Kama ni zawadi mnapeleka vijijini sio mbaya mkanunua kwani nguo za mtumba sio gharama sana .

Niwatakie likizo njema
 
True bora ukazigawe kanisani, au kwenye NGo wasiokujua, japo kama ndugu mchawi akikutaka hakukosi sababu mshare mzimu mmoja kupitia family tree labda tu uwe na elimu ya kutosha kuhusu kuziblock nguvu za giza zisikuattack.
 
True bora ukazigawe kanisani, au kwenye NGo wasiokujua, japo kama ndugu mchawi akikutaka hakukosi sababu mshare mzimu mmoja kupitia family tree labda tu uwe na elimu ya kutosha kuhusu kuziblock nguvu za giza zisikuattack.
Duuh kuna mzimu wa Familiy tree [emoji268] tena!??
 
Waroge tu hakuna namna, mama akija anafunga zote ambazo sivai anapeleka kijijini, watoto wa ndugu almost wa ukoo mzima hakuna ambae hajawahi vaa nguo zangu. Sana sana wale wanaomsaidia kazi kufua, usafi wote anawapaga hizo.

Uko sahihi ila ndo hivyo tena kama kuroga washaroga sana
 
Back
Top Bottom