Jielimishe kuhusu Israel na vita zinazomzunguka

4,000-3,000 KK Enzi ya Mawe-Shaba: kuibuka kwa tamaduni za kikanda.

Maendeleo ya tamaduni za kikanda nchini Palestina kwa kuzingatia maisha ya ufugaji sambamba na uzalishaji wa bidhaa za kilimo;

Upatikanaji wa shaba(copper), pamoja uwepo wa tamaduni kubwa zaidi za sanaa na ibada.
 
3,000-1,250 KK Enzi ya Bronze/Shaba: Mji wa Kanaani unatawaliwa na milki ya kale ya Misri.

Kuibuka kwa maisha ya mijini na kuanzishwa kwa miji ya kwanza yenye ngome chini ya utawala wa Misri;

Wakanaani, kundi la watu wa Kisemiti, walikaa Palestina/Kanaani na kando ya pwani ya Syria-Palestina. Walianzisha majimbo nusu-huru kama inavyoonyeshwa katika Barua za Tell al-Amarna;

Walidumisha biashara ya baharini na nchi kavu kati yao na Mediterania ya mashariki, Misri na Mesopotamia;

Walivumbua uandishi wa alfabeti;

Walianzisha dini ya miungu mingi iliyofanana na watu wa Kisemiti wa Mashariki ya Karibu ya kale;

Walitengeneza zana za shaba;

Uasi wa mara kwa mara wa majimbo ya mji wa Kanaani ulichochea kampeni za kijeshi za Misri huko Palestina.
 
1250-721 KK Enzi ya Chuma: Falme za kikanda

Uhamiaji mkubwa wa idadi ya watu ulisababisha kuanzishwa kwa falme za kikanda huko Palestina:

Wafoinike (Phoenicians), ambao ni uzao na warithi wa Wakanaani, ambao walikuwa wasafiri wa baharini na , ambao walianzia kwenye majimbo yao ya miji kando kando ya pwani ya Syria-Palestina, makoloni ya bahari kwenye mwambao wa kusini wa bonde la Mediterania. ;

Wafilisti ambao ndiyo jina la Palestina lilipoanzia, walihama kutoka bonde la Mediterania, wakaanzisha shirikisho la majimbo ya miji kwenye pwani ya kusini ya Palestina, na kutengeneza silaha na zana za chuma;

Waebrania au Waisraeli, watu wa Semitic waliohamahama, walikaa katika milima ya kati ya Palestina; walikuwa wameathiriwa kiutamaduni na Wakanaani, na walikuwa wakipigana na Wafilisti.
 
Wayahudi, idadi yao ni ndogo sana, japo kuna wakati walikuwa wengi kidogo. Mwaka 1939, kabla ya vita kuu ya Dunia, idadi ya Wayahudi ilifikia 15.3 million Hitler aliwaua Wayahudi wapatao milioni 6. Wayahudi waliprudi Mashariki ya kati na kuanzisha Taifa la Israel mwaka 1948 walikuwa 0.806 milioni. Ifahamike kuwa mwaka 1933, idadi ya Watanganyika inakadiriwa kuwa watu milioni 5 tu, yaani Wayahudi walikuwa wengi mara 3 ya Watanganyika.

Kabla ya Wayahudi kuvamia na kutwaa eneo la Caanan ambalo ndiyo ardhi asilia ya Wayahudi, lilikuwa na ukubwa wa 50,000 kilometa za mraba. Israel ya leo ina ukubwa wa mita za kilometa za mraba 22,145.

Lakini hata kabla ya haya yaliyowapata baada ya Kristo, kabla yake walipitia madhira mengi kama vile kutengwa na Mungu (walipotenda kinyume na maagano), kuuawa na kutiwa utumwani mara kadhaa. Hivyo, kwa Wayahudi, kuuawa, kupigana vita na kushinda na hata kushindwa, kuishi kwa kumpendeza Mungu, kumkana, na kutenda kinyume cha mapenzi ya Mungu, imekuwa ndiyo mfumo wao wa maisha wakati wote. Na kiimani, tunaamini kuwa hayo yote ndivyo mpango wa Mungu ulivyo dhidi ya Israel na Ulimwengu mzima.

Israel imewahi kudhulumiwa na Wamisri, Wamaleki, Wafilisti, Wapersia, Wababiloni, Warumi, na nchi na makabila mengine mengi.

Kwa nini yote haya yanawatokea Waisrael?
Kwa kadiri ya biblia, ni kwa sababu, Mungu ana mpango na Taifa la Israel, na shetani yupo kwa sababu ya kuharibu mpango wa Mungu. Hivyo ni shetani anawatumia majirani zake, kuiangamiza Israel.

Kiimani, ni kwamba sijui awe ni Hitler, Iran, Wasyria, Hamas au Hizibollah, Wabogoni (Russia), hakuna aliyeweza au atakayeweza kuwaangamiza na kuwapoteza Waisrael. Maangamizi ya Waisrael yatakuja na kutoweka, na wala maangamizi hayo hayamaanishi kuwa tunaelekea siku za mwisho kama baadhi ya watu wanavyotaka kutuaminisha.

Nyakati hizi za mahangaiko ya Wayahudi inatajwa kuwa tribulation (Yeremia 30:7).

Lakini kuhusu siku za mwisho, kuhusiana na Israel, biblia inasema kuwa, makundi makubwa ya Wayahudi yatarejea kwenye ardhi ya Israel (Kumbukumbu la Torati 30:3; Isaya 43:6; Ezekiel 34:11-13; 36:24; 37:1-14). Ifahamike mpaka sasa hivi, Wayahudi wanaoishi Israel ni milioni 9 tu. Wayahudi wapatao 18 milioni wanaishi nje ya Israel, kwenye mataifa mbalimbali.

Kisha mpinga Kristo atafanya mkataba wa amani wa miaka 7 na Waisrael (Isaya 28:18; Daniel 9:27).

Hekalu lililovunjwa (bila shaka kutokana na vita) litajengwa upya mjini Yerusalem (Daniel 9:27; Matayo 24:15; 2 Watesolonike; 2:3-4; Ufunuo 11:1).

Mpinga Kristo atavunja mkataba wa amani uliosainiwa, na mauaji makubwa ya Wayahudi yatafanyika (Daniel 9:27; 12:1, 11; Zacharia 11:16; Matayo 24:15, 21; Ufunuo 12:13). Israel itavamiwa (Ezekiel 38-39).

Kisha Wayahudi watamtambua na kumkiri Yesu kuwa ndiye Masiha (Zacharia 12:10). Baada ya kumkiri Kristo, Israel mpya itazaliwa, itahuishwa, na itaungamishwa kama ilivyokuwa kale (Yeremia 33:8; Ezekiel 11:17; Warumi 11:26).

Andiko hili ni kwaajili ya wanaotaka kujifunza, wasio na nia hiyo, wasihangaishwe nalo.
Mathanzua ...
 
721-332 KK Tawala(hegemony) ya Mesopotamia

Palestina iliwekwa chini ya himaya ya Mesopotamia; ilishindwa mwaka wa 721 KWK na Waashuru(Assyrians), na mwaka wa 586 KWK na Wababiloni, ambao waliwapeleka uhamishoni watu wengi.

Wakati huu, jina la Palestina kwa namna ya "Plistu", linalotokana na Wafilisti, lilionekana kwa mara ya kwanza katika nyaraka za Ashuru.(Assyrians).

Mfalme Koreshi wa Uajemi (Persian emperor Cyrus), aliichukuwa na kuimiliki Palestina na kuruhusu Wayuda warudi kutoka uhamishoni;

Asilimia kubwa ya mawazo, tabia na taasisi, ikiwa ni pamoja na neno Wayahudi, viliibuka wakati huu;

Sehemu kubwa ya Biblia ya Kiebrania iliandikwa upya na kukamilishwa.

Jina "Palestina", lilitajwa na mwanahistoria wa Kigiriki wa karne ya 5 KK Herodotus, lilionekana baadaye katika Agano la Kale kwa namna ya Kiebrania ya "Pleshet", inayotokana na neno "Pleshteem" (Wafilisti).
 
332-63 KK Kipindi cha Ugiriki

Alexander the Great aliichukuwa na kui tawala Palestina mnamo 332, akiiweka chini ya ushawishi wa utamaduni wa Hellenistic, (under influence of Hellenistic culture), ambao uliathiri nyanja zote za maisha, sanaa na usanifu, falsafa na dini.

Baada ya kifo cha Alexander, Dola yake ya Mashariki ya Kati iligawanywa kati ya majenerali wake wawili: Shamu ambayo ndiyo Syria na Palestina ziliwekwa chini ya Waseleucide, na Misri chini ya Ptolemy;

Wayahudi, wakiongozwa na Wamakabayo,(Maccabees), walipingana dhidi ya uenezaji uliolazimishwa wa “hellistic”, wakaasi na hapo kuibuka ufalme huru wa Wahasmonean (Hasmonean Kingdom), ambao ulianzishwa mwaka wa 129 KK.

Wahasmonea waliwalazmisha kwa nguvu Waidumea (Waarabu wa awali wa Palestina ya kusini), kuwaingiza kwenye Uyahudi(Judaism)
 
63 KK-325 BK Kipindi cha Warumi

Kufuatia kuchukuliwa na kutawaliwa kwa Palestina na Warumi mnamo 63 KK, mchakato wa Urumi (Romanization) ulianza;

Kuanzishwa kwa miji, ya Kirumi katika kama vile Yerusalemu, Kaisaria, Sabatiya, Beisan;

Mfalme kibaraka, Herode Mkuu (Mwarabu wa Idumea kwa asili) aliteuliwa kuwa mtawala wa Uyahudi mwaka wa 37 KK;

Wakati huo, makabila ya nchi yalijumuisha Wayahudi, Wasamaria, Waidumea na Waarabu wa Nabatean, Wagiriki na Wafoinike;

Kuzaliwa kwa Yesu Kristo na kuenea kwa Ukristo kulingana na mafundisho yake, na uandishi wa Agano Jipya;

Maasi makubwa mawili ya Wayahudi dhidi ya Warumi yalizimwa, moja katika 70 CE lilisababisha uharibifu wa Hekalu la Wayahudi huko Yerusalemu;

Jaribio la pili la uasi la wayahudi la Bar Kochba mwaka wa 135 WK, lilipelekea Yerusalemu kuharibiwa kabisa na kusambararishwa.

Likajengwa koloni la Kiroma, Aelia Capitolina, kama mbadala.
 
325-640 Kipindi cha Byzantine

Palestina ikawa chini ya utawala wa Milki ya Byzantine;

Mfalme Constantine alihalalisha Ukristo na kuutangaza kuwa dini rasmi ya serikali.

Palestina polepole ikawa ya Kikristo; makanisa mengi na nyumba za watawa zilijengwa kote nchini katika maeneo ya kitamaduni yanayohusiana na maisha ya Kristo, kati ya haya, Kanisa la Ufufuo huko Yerusalemu na Kanisa la Kuzaliwa kwa Yesu huko Beth Lehemu.

Mahujaji wengi walitembelea maeneo matakatifu.
 
640-1099 Kipindi cha awali cha Uislam

Waarabu Waislamu waliteka Palestina kutoka kwa waByzantines na baadaye kuwwabadili wenyeji kuwa waislam(kuwasilimisha).

Bani Umayya wa Damascus (661–750) waliigeuza Yerusalemu, ambayo ilikuja kuwa jiji la tatu takatifu la Kiislamu, na kujenga Haram al-Sharif, ikijumuisha Kuba la Mwamba(Dome of the rock), na Msikiti wa Al Aqsa.

Waliijenga Ramala na kuufanya kuwa mji mkuu wa Palestina.

Chini ya Bani Abbass huko Baghdad (750-969), Fatimids huko Cairo (969-1073), na Saljuqs huko Damascus (1073-1098), Palestina iliendelea kustawi na Yerusalemu ilikuwa kituo cha Hija na mafunzo ya Kiislamu
 
1099-1291 Kipindi cha Crusader(wapigania ukristo)

The Crusaders (Franks) ambao walikuwa wakiupigania ukristo, waliiteka Palestina mwaka 1099, na kufuatiwa na mchakato wa ukoloni;

Yerusalem iliharibiwa na wakazi wake kuuawa;

Ufalme wa Kilatini wa Yerusalemu ulianzishwa, pamoja na amri za kijeshi za kuulinda;

Crusaders(Franks), walianzisha miji mingi, makazi ya vijijini, majumba, makanisa, nyumba za watawa na mitambo ya viwandani
 
1187-1250 Kipindi cha Ayyubid

Waayyubid, wakiwafuata watangulizi wao Wazangid, walipigana ‘vita vitakatifu’ dhidi ya majimbo ya Crusader katika Levant.

Baada ya Salah al-Din kuwashinda Wapiganaji wa Msalaba(Crusaders) kwenye vita vya Hittin mwaka 1187. Salah al-Din aliirejesha Palestina na Jerusalem, akarudisha na kuweka wakfu maeneo matakatifu ya Kiislamu huko Jerusalem, na kufufua sanaa na usanifu wa Kiislamu.

Jerusalem ilijisalimisha(surrender) kwa Wanajeshi wa Msalaba(crusaders) na al-Kamil aliyefanya mapatano ya amani mwaka wa 1229.

Lakini Ilitekwa tena na Wakhawarizmian mwaka 1244
 
1260-1517 Kipindi cha Mamluk

Mamluk, waliwapindua Ayyubid na kutawala Palestina kutoka Cairo.

Mnamo mwaka wa 1260 waliwashinda Wamongolia kwenye mapigano makali ‘Ain Jalut [karibu na Nazareti].

Kufikia wakati wa kifo cha Baybars mnamo mwaka 1277, alikuwa ameteka tena sehemu kubwa ya Palestina kutoka kwa Wanajeshi.

Wamamluk walikuwa walinzi wakubwa wa sanaa na walifadhili idadi kubwa ya majengo ya kidini na ya kilimwengu, yaliyojengwa kwa mtindo wa kipekee.

Pia walianzisha mtandao mpana wa khans (caravanserais) na vituo vya posta, vilivyounganishwa na mtandao wa barabara na madaraja. Jerusalem ilithibitishwa zaidi kama kitovu cha Hija na masomo ya Waislamu
 
1516-1917 Kipindi cha Ottoman

Sultani wa Kituruki wa Ottoman Selim I, aliiteka Palestina mnamo 1516 na kuiingiza katika Milki ya Ottoman.

Chini ya Sultan Suleiman Mtukufu mpango mpana wa kazi ulifanywa, ikiwa ni pamoja na kujenga upya kuta za Yerusalemu na kurejesha Jumba la Mwamba na Msikiti wa Al Aqsa.

Palestina iligawanywa na Waottoman katika wilaya (sanjaks) za Jerusalem, Nablus, na Acre.

Utozaji ushuru mkubwa na hatua za ukandamizaji za mamlaka ya Ottoman zilisababisha maasi kadhaa, huku viongozi wa eneo hilo wakitangaza utawala wa 'uhuru', kama vile Zahir al-'Umar kaskazini mwa Palestina na mji wake mkuu huko Acre.

Mnamo mwaka 1801, uvamizi wa kijeshi wa Ufaransa huko Misri na Palestina ukiongozwa na Napoleon ulipigwa na kufukuzwa kule Acre na Ahmad Pasha al-Jazzar.

Muhammad ‘Ali alitangaza uhuru huko Misri na kuikalia kwa mabavu Palestina (1831-1840). Jaffa ilikua bandari muhimu zaidi huko Palestina.

Wimbi la kwanza la uhamiaji wa Kiyahudi kwenda Palestina lilianza mnamo 1881. Lengo la kuanzisha makazi ya Wayahudi huko Palestina lilitangazwa na Herzl katika kongamano la kwanza la Wazayuni huko Basel mnamo 1897.

Mnamo 1916, Uingereza na Ufaransa zilikubaliana kwa siri kuyagawa majimbo ya Kiarabu ya Dola ya Ottoman kati yao.
 
1917-1920 Utawala wa Kijeshi wa Uingereza wa Palestina

Mwaka 1917 Jerusalem ilitekwa na majeshi ya Uingereza yakiongozwa na Jenerali Allenby.

Katika mwaka huo huo Serikali ya Uingereza ilitangaza katika Azimio la Balfour, uungaji mkono wake wa kuanzishwa kwa makao ya kitaifa ya watu wa Kiyahudi huko Palestina.
 
1920-1948 Mamlaka ya Uingereza

Uingereza ‘ilitunukiwa’ Mamlaka ya Palestina mwaka 1920; kuongezeka kwa uhamiaji na makazi ya Wayahudi, kwa msaada wa Uingereza;

Uasi wa Wapalestina wa 1936, ambao ulidumu kwa miaka mitatu, ulikuwa dhidi ya mamlaka ya Uingereza na uhamiaji wa Wayahudi ambao ulikuwa unaoongezeka;

Wimbi la ugaidi wa Kiyahudi na hujuma dhidi ya Waingereza viliongezeka;

Mpango wa Umoja wa Mataifa wa kugawanya Palestina mwaka 1947 kuwa mataifa mawili tofauti: Wayahudi na Waarabu.
 
Baada ya 1948 Nakba ya Palestina na Diaspora / Taifa la Israeli

Vita na Nakba ya Wapalestina ya 1948 ilisababisha mauwaji ya Wapalestina (ethnic cleansing) kutoka kwenye nchi yao na kuanzishwa kwa Taifa la Israeli;

Takriban wananchi milioni moja wa Kipalestina wakawa wakimbizi katika nchi jirani za Kiarabu; zaidi ya miji na vijiji 500 viliondolewa wananchi wake na kuharibiwa;

Wapalestina waliosalia wakawa chini ya utawala wa kijeshi wa Israel; Sheria ikatungwa ya kumiliki mali za wale wa Palestine waliokimbia ilipofika mwaka 1950, ambapo ardhi ya wakimbizi wa Kipalestina ikawa mali ya taifa la Israeli;

Israeli ilipitisha Sheria ya Kurudi, ikimpa kila Myahudi haki ya kuishi Israeli/Palestina;

Pia haki ya kuishi kwenye ukingo wa Magharibi na Ukanda wa Gaza chini ya utawala wa Jordan na Misri,

Vuguvugu la Fateh(Fateh movement) lililoongozwa na Yasser Arafat lilianzishwa mwaka 1961;

Chama cha ukombozi wa Palestina PLO kilianzishwa mnamo 1964.
 
1982 Mauaji ya Sabra na Shatila

Azimio nambari 242 la Umoja wa Mataifa linatoa wito kwa Israel kujiondoa katika maeneo iliyoyakalia kwa nguvu;

Vita vya al-Karama mnamo 1968, ambapo Fatah ilizuia shambulio la Israeli;

Vita ya octoba 1973; Mkataba wa Camp David ulitiwa saini na Israel, Misri na Marekani;

Uvamizi wa Israel dhidi ya Lebanon, kuzingirwa kwa Beirut, kufukuzwa kwa PLO kutoka Lebanon na mauwaji ya wananchi wengi Sabra na Shatila mwaka 1982.
 
1987-1993 Intifada ya Kwanza na Makubaliano ya Oslo

Intifadha ya kwanza ya Wapalestina mwaka 1987 na kuanzishwa kwa Uongozi wa Umoja wa Intifadha;

Mkutano wa amani wa Madrid 1992;

Mikataba ya Oslo iliyotiwa saini kati ya Israel na PLO mwaka 1993;

Kuanzishwa kwa Mamlaka ya Kitaifa ya Palestina mnamo 1994;

Kuendelea kwa shughuli (settlements)za makazi ya wahamiaji wa Israeli;

Mgawanyo zaidi wa maeneo/makazi ya Palestina kuendelea kufanywa na Israel.
 
2000–sasa: Intifadha ya Pili hadi Maandamano Makuu ya Kurudi

Kuzuka kwa Intifadha ya Pili na kukaliwa tena kwa nguvu kwa maeneo ya Palestina yaliyokuwa chini ya udhibiti wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina mwaka 2002;

Wanajeshi wa Israel kumzingira Arafat kule Ramallah na kusababisha kifo chake mwaka 2004;

Kutambuliwa kwa Umoja wa Mataifa kwa Taifa la Palestina kama nchi isiyo mwanachama mnamo 2012;

The Great March for Return in 2018 ambapo wizi wa ardhi ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu kwa matumizi ya walowezi wa Kiyahudi wa Israel bado unaendelea na unaendelea licha ya kuwa unakiuka sheria za kimataifa.
 
Courtesy of Dr Mahmoud Hawari and Dr Ghada Karmi on “Palestinian History Tapestry”

Dr Mahmoud Hawari, formerly Director General of the Palestinian Museum in Birzeit, and Dr Ghada Karmi, Research Fellow at the Institute of Arab and Islamic Studies, Exeter University, are responsible for drawing up this chronology.
 
Back
Top Bottom