Jide: Sijampiga kijembe Gadner

warumi

R I P
May 6, 2013
16,218
18,440
MKONGWE wa Bongo Fleva, Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ au Jide, amefunguka kuwa katika wimbo wake mpya wa Ndindindi, hajampiga kijembe aliyekuwa mumewe, Mtangazaji Gardner G. Habash kama wengi wanavyodhani.

[http://www]

Jide na aliyekuwa mumewe, Gardner

Akizungumza na mwanahabari wetu, Jide alisema wimbo huo ulitungwa na watu wake tofauti na yeye kuukamilisha hivyo kwa kuwa umebeba ujumbe mzito ni rahisi mtu kuhisi amemuimba mtu fulani kumbe yeye aliimba kwa ajili ya mashabiki wake wote.

“Sijampiga kijembe huyo wanayemsema (Gardner). Mimi nimetumia utunzi wangu kuwakilisha yale yanayotokea katika jamii mbalimbali sasa kama mtu anaona umemgusa fulani atakuwa amejiongeza tu lakini mimi sikumaanisha mtu mmoja bali ujumbe kwa mashabiki wangu wote,” alisema Jide.

Kwenye wimbo huo kuna sehemu Jide kaimba; “Niliwezaje kutoa vyote ili hali wewe ulininyima vyote” ambapo iliaminika amemzungumzia Gardner.
 
Attachments

  • 1459701081321.jpg
    1459701081321.jpg
    10.5 KB · Views: 105

Ni muhimu tukafahamu hiyo 'ndi ndi ndi' manake nini? Halafu hayo maneno “Niliwezaje kutoa vyote ili hali wewe ulininyima vyote” yanatia shaka angefafanua alitoa nini akanyimwa nini?
 
alimpa gadner upendo na mali zake but mwisho wa siku hakupata mapenzi , jide asitufanye sie matahira
 
Mi nimependa tu ubunifu , the ndi ndi ndi, dah jide mbaya nyie
 
alimpa gadner upendo na mali zake but mwisho wa siku hakupata mapenzi , jide asitufanye sie matahira
Huyo mama nae, kwani siku zooote walivyokuwa 'wakishow love' walikuwa manatuchuuza?
 
  • Thanks
Reactions: Lee
Kwani Yale manyimbo ya taarabu ambayo wamama wa uswazi upiga kwa sauti ya juu ili kuwakoga wenzao huwa ni kweli yametungwa kwa ajili ya hao kuwakoga wenzao?
Ni muhimu tukafahamu hiyo 'ndi ndi ndi' manake nini? Halafu hayo maneno “Niliwezaje kutoa vyote ili hali wewe ulininyima vyote” yanatia shaka angefafanua alitoa nini akanyimwa nini?
 
Mwanamke Sura, Tako na Kiuno ukikosa hivyo hata umiliki Dunia nzima Kidume chako lazima kika Pump hata kitaa kwa housegirl wa jirani!
 
Kwani Yale manyimbo ya taarabu ambayo wamama wa uswazi upiga kwa sauti ya juu ili kuwakoga wenzao huwa ni kweli yametungwa kwa ajili ya hao kuwakoga wenzao?
Mkuu hii ni bongo fleva sio taarabu, kama ingekuwa taarabu unafikiri tungeuliza, ingekuwa pouwa
 
Kwa mwanamuziki mkubwa kama Jd nilitegemea akiulizwa atajibu hivyo. Ni Ney wa mitego tu anaweza sema wimbo huu nimemuimba Wema kama anabisha niliyosema aje hapa uso kwa uso akatae..
 
Zote ni nyimbo tu tofauti ni miondoko, kwani wimbo wa Linex -Aifola ukimsikilizisha manzi wako mliyegombana anaweza kukupa jibu gani?
Mkuu hii ni bongo fleva sio taarabu, kama ingekuwa taarabu unafikiri tungeuliza, ingekuwa pouwa
 
Watu tunachoshindwa kuelewa kwamba kinachoifanya nyimbo yoyote iwe nzuri ni pale kila mtu anavyoitafsir na kuilewa kwa maana yake yy mwenyew alivyoilewa. Kamwe nyimbo haiwezi kuwa na maana moja. So wanaosema hiki na kile ni jinsi wao walivyouelewa. (Imao)
 
Ni muhimu tukafahamu hiyo 'ndi ndi ndi' manake nini? Halafu hayo maneno “Niliwezaje kutoa vyote ili hali wewe ulininyima vyote” yanatia shaka angefafanua alitoa nini akanyimwa nini?
Mkuu ongezea na, "Alitoa kwa nani na nani alimnyima vyote".
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom