Wadau muda huu kwenye star Tv kuna kipindi cha jicho letu ndani ya habari...na wameanza kujadili kichwa cha habari cha gazeti moja kilichosema"CCM inakufa" pia watajadili ujio wa Kibanda......
Ni kweli kabisa CCM inakufa maana mambo yayotokea sasa inadhibitisha kabisa kuwa CCM inakufa,na ikfa haitanyanyuka tena maana wanainchi wamechoka na AHADI hewa za viongozi wa chama hicho
STAR TV walishajiondoa kwenye cable system hiyo usikose kutupa update mkuu, ila kwa awali tu ni kwamba hicho kichwa cha habari kilichoandika "CCM INAKUFA" kimeenda kwenye mantiki moja kwa moja!
CCM haitafuti huruma kwa wanachi kwa kuwa inaonyesha kitu halisia. CDM ndio wanatafuya huruma kwa wananchi kwa kukimbilia kuitisha maandamano hata mambo yaliyoshindwa kwa hoja kama bungeni, mahakamani n.k huko ndiko kutafuta huruma. Mtu mzima huwezi kukimbilia mahakamani kwa mambo ambayo mengine hutatuliwa kwa njia ya kisheria.
Star tv is doing good job....km kuna uwezekano kwenye katiba mpya, watanzania tupendekeze hii tv iwe ndo chombo cha taifa maana tbc ishakuw mali ya ccm.
Star Tv wenyewe naona wanataka watu wote tununue ving'amuzi vyao wamejitoa hawaonekani ving'amuzi
vingine,na sisi watanzania tumeghairi kujaza maving'amuzi mengi ndani so tupe up date
Kipindi ni kizuri na nafikiri hawa Star TV walitaka kufanya kitu kama LISTENING POST cha aljazeera lakini nafikiri huyo mtangazaji bado mchanga sana katika fani ya habari,taarifa ni kuwa anasoma SAUT na kila kipindi ni lazima wawepo wakufunzi wa hapo na wanafunzi ambao kimsingi hawajui hali halisi ya utendaji wa media za tanazania,wao wanajadili hoja kwa kutumia notice za chuoni,
Kiukweli Doto anajitahidi sana, anajua jinsi ya kuwabana wageni wake kwa maswali, sema mgeni wa leo (moses) alikua na jazba sana alipoulizwa kuhusu kichwa cha habari "CCM inakufa". hiki ni kipindi pekee sipendi kukosa statv, vinginevyo jamaa hawana vipindi vizuri.
Uwekezaji wanaoufanya wa kujiunga DSTV uendane sanjari na kutafuta wanahabari makini na weledi. Jamani tujaribu hata kujifunza kwa jirani zetu Kenya, media zao zinaleta mvuto kuzitazama.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.