Jicho letu ndani ya habari - Star Tv

Jicho letu ndani ya habari - Star Tv

Kurunzi

Platinum Member
Joined
Jul 31, 2009
Posts
10,196
Reaction score
11,624
Kipindi cha jicho la habari naona kimeanza, wachambuzi watatupia macho mambo yaliyojitokeza kwenye habari wiki hii huku kikubwa ni suala la Gesi Mtwara kauli za Rais, na Waziri na wanasiasa wengine.

Naona hiki kipindi kinakosa mvuto kadri siku zinapokwenda kwani Studio Dar hakuna wachambuzi na hata waliopo Mwanza sidhani kama wanaweza kutoa hoja za msingi.

Kama ulisoma maelezo ya Zitto kwenye mwananchi ilitegemea waziri Mhongo kuja kujibu hoja za zitto na lipumba na Mbatia. Star TV boresheni kipindi tuongee asubuhi.
 
Acha ushabiki, wewe ndio unaangalia tv, unashindwa nn kutaja waalikwa ni kina nani kwa dar na mwanza na wameanza kwa kuzungumza nini.usitake unachokitaka wewe ndio kizungumzwe.ndio mana hakuna wachangiaji apa wamekudharau
 
Nawasikiliza naona Odelo anataka uwazi wa sera lakini huyu mwingine kila akija hapa startv yeye anataka uandishi wa utafiti. Mi siwaelewi kabisa
 
Acha ushabiki, wewe ndio unaangalia tv, unashindwa nn kutaja waalikwa ni kina nani kwa dar na mwanza na wameanza kwa kuzungumza nini.usitake unachokitaka wewe ndio kizungumzwe.ndio mana hakuna wachangiaji apa wamekudharau

Mbona povu linakutoka mia, nimeanzisha post ili wadau wengine wachangie wano angalia Tv au wasioangalia.
 
huyu moses hata ukumuangalia uson unamuona fika ni mtu anayehubiri asichokiamini.
 
.........
Naona hiki kipindi kinakosa mvuto kadri siku zinapokwenda kwani Studio Dar hakuna wachambuzi na hata waliopo Mwanza sidhani kama wanaweza kutoa hoja za msingi.
...............

Pale Mwanza yupo Mchambuzi mmoja (ODERO) tu ambaye anaweza kutoa uchambuzi unaoeleweka kwani anaweza kujibu kwa ufasaha maswali anayoulizwa na mtangazaji (Dotto). Huyu mwingine (MOSES) anashindwa kwenda sawa na speed ya mjadala/anashidwa kujibu hoja za mtangazaji kwa ufasaha kwani "emotions" zinatawala sana majibu yake. Mara nyingine Moses apigwe msasa namna ya kushiriki mijadala kwa ufasaha kabla ya kushiriki.
 
Lugha ni muhimu sana katika maendele ya nchi yoyoye. Naomba waandishi na wataalamu watumie lugha yetu ya kiswahili

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Naona Deus (Godless Lema wa Dodoma kwamujibu wa Lukuvu) kapiga simu na kuwe wazi yeye si Lema kama lukuvu alivyodai baili ni mtoto wa seremala anaishi Dodoma
 
  • Thanks
Reactions: PSM
Kesho George Simba Chawene atakuwa studio kujibu hoja zilizojitokeza katika sakata la gesi
 
Pale Mwanza yupo Mchambuzi mmoja (ODERO) tu ambaye anaweza kutoa uchambuzi unaoeleweka kwani anaweza kujibu kwa ufasaha maswali anayoulizwa na mtangazaji (Dotto). Huyu mwingine (MOSES) anashindwa kwenda sawa na speed ya mjadala/anashidwa kujibu hoja za mtangazaji kwa ufasaha kwani "emotions" zinatawala sana majibu yake. Mara nyingine Moses apigwe msasa namna ya kushiriki mijadala kwa ufasaha kabla ya kushiriki.

Kipindi kama kipindi ni kizuri kwani hakina tofauti na kile cha This week in perspective cha TBC1 ambacho ndicho kipindi pekee ninachokiangalia katika kituo hicho! Ila tatizo ninaloliona kwa star TV wanakosa human resource, sipendi saana ninapoona kila week analysts walewale say Odero + Moses wakijitahidi sana kutakuwa na Dr Kitima (mwalimu wa Odero) inafanya kipindi kinakosa uhondo kwa kweli. Na hata huko dar napo hawatuletei watu wa kueleweka. kumsikiliza mtu mmoja au hata wawili kila mara ni kufanyika wanafunzi wake kitu ambacho sio lengo la kipindi. Imefika mahali huwa nauliza leo ni Odero na nani? Ni wito wangu kwa hosts wa kipindi hiki sasa kuanza mwaka huu kwa kuikakabili changamoto hii!

With regards.

Nkunya
 
Mualikwa Moses bure kabisa......

Mkuu,

Mbona huyo hajawahi kuwa kitu. Mie imefika hatua ya kumuona tu kwenye kipindi nabadilisha channel. In fact hana tofauti na Mwigulu Nchemba, pumba tupu! Samahani kwa wananchi wa Nchemba.

Kwa moses kwanza hata habishani kwa hoja anapandisha mori tuu. Haheshimu mwenyekiti wala nini, kama isingekuwa huwa anaalikwa ningesema ni namna ya kuhujumu kipindi hiki. Lakini ni mwalikwa sasa tusemeje?
 
...star tv tuliwapenda sana lakini magamba yamewapenda zaidi..."MPUMZIKE KWA AMANI"...
 
Kipindi cha jicho la habari naona kimeanza, wachambuzi watatupia macho mambo yaliyojitokeza kwenye habari wiki hii huku kikubwa ni suala la Gesi Mtwara kauli za Rais, na Waziri na wanasiasa wengine.

Naona hiki kipindi kinakosa mvuto kadri siku zinapokwenda kwani Studio Dar hakuna wachambuzi na hata waliopo Mwanza sidhani kama wanaweza kutoa hoja za msingi.

Kama ulisoma maelezo ya Zitto kwenye mwananchi ilitegemea waziri Mhongo kuja kujibu hoja za zitto na lipumba na Mbatia. Star TV boresheni kipindi tuongee asubuhi.

Mvuto gani unaoutaka? Taja basi waliopo studio siyo kulalamika tu.
 
Kipindi kama kipindi ni kizuri kwani hakina tofauti na kile cha This week in perspective cha TBC1 ambacho ndicho kipindi pekee ninachokiangalia katika kituo hicho! Ila tatizo ninaloliona kwa star TV wanakosa human resource, sipendi saana ninapoona kila week analysts walewale say Odero + Moses wakijitahidi sana kutakuwa na
Dr Kitine (mwalimu wa Odero) inafanya kipindi kinakosa uhondo kwa kweli. Na hata huko dar napo hawatuletei watu wa kueleweka. kumsikiliza mtu mmoja au hata wawili kila mara ni kufanyika wanafunzi wake kitu ambacho sio lengo la kipindi. Imefika mahali huwa nauliza leo ni Odero na nani? Ni wito wangu kwa hosts wa kipindi hiki sasa kuanza mwaka huu kwa kuikakabili changamoto hii!

With regards.

-Nkunya
Hapo kwenye red kwa vyovyote vile ulitaka kusema Dr. Kitima na si kitine huyu ni mtu mwingine
 
Pale Mwanza yupo Mchambuzi mmoja (ODERO) tu ambaye anaweza kutoa uchambuzi unaoeleweka kwani anaweza kujibu kwa ufasaha maswali anayoulizwa na mtangazaji (Dotto). Huyu mwingine (MOSES) anashindwa kwenda sawa na speed ya mjadala/anashidwa kujibu hoja za mtangazaji kwa ufasaha kwani "emotions" zinatawala sana majibu yake. Mara nyingine Moses apigwe msasa namna ya kushiriki mijadala kwa ufasaha kabla ya kushiriki.

Huyo MOSES mara zote yuko off point hata hajui anachokisema maana anarudiarudia tu yale ambayo alishayasema zamani. Nadhani ana maslahi ama ndani ya serikali au chama tawala maana uchangiaji wake always una walakini. Pengine anaogopa kuonekana yuko critical au la. Simwelewi kabisa! Kijana kama yeye halafu awe na mawazo mgando ni jambo la ajabu kabisa!
 
Kipindi kama kipindi ni kizuri kwani hakina tofauti na kile cha This week in perspective cha TBC1 ambacho ndicho kipindi pekee ninachokiangalia katika kituo hicho! Ila tatizo ninaloliona kwa star TV wanakosa human resource, sipendi saana ninapoona kila week analysts walewale say Odero + Moses wakijitahidi sana kutakuwa na Dr Kitima (mwalimu wa Odero) inafanya kipindi kinakosa uhondo kwa kweli. Na hata huko dar napo hawatuletei watu wa kueleweka. kumsikiliza mtu mmoja au hata wawili kila mara ni kufanyika wanafunzi wake kitu ambacho sio lengo la kipindi. Imefika mahali huwa nauliza leo ni Odero na nani? Ni wito wangu kwa hosts wa kipindi hiki sasa kuanza mwaka huu kwa kuikakabili changamoto hii!

With regards.

Nkunya

Wana JF,

Kwanza tu natoa pongezi zangu za dhati kuwa Star Tv wanajitahidi sana na ndio twakubali wote ingawa kuna mapungufu yet wanajitahidi kuliko TBC1 Tv ya Taifa ikiwa inatuonyeshaga uozo mtupu na kuitetea serikali kila kukicha.

Wana JF wenzangu kimsingi ndio Dotto nae anakumbwa na changamoto nyingi sana ila najua pia nae anapenda makubwa zaidi pia nasi tunayo yahitaji Star TV watupe mfano ni changamoto ya kuwa na TV base za Star tv iwepo Arusha, Mbeya, Dodoma, na Dar ingawa sijui siku hizi kuna kuwa na tatizo la mawasiliano au mitambo inatakiwa kuboreshwa ili kuwepo na wachangiaji mahali pengi kama tunavyo ona kipindi cha SHAKA Sali VOA kina deal na African Politics.

Na mbali na hilo Kipindi cha leo kilikuwa ni kizuri sana Odero anajitahidi sana ila moses nadhani itikadi zake kwakeli ni ngumu sana yeye huwa yuko mlengo tofauti ila ukimbana maswali sijui huwa anajitambua kuwa anarudi pale pale na akasupport mada. Mada ya leo ili kuwa ni kweli kutaka kujua ufahamu na uelewa wa waandishi wetu waendapo kwa Press conference je huwa wamejiandaa au wanaenda chukuwa posho, Prof: Muhogo alipaswa ulizwa maswali machache sana, Gesi hajatungiwa sheria utekelezaji umeisha anza, Unapo wapa watu majibu ya ki geography yanayo kinzana wakati kwenye karatasi Mtwala ndio mwaitaja Gesi inapatikana prof hakutoa mwangaza unao eleweka kabisa ju ya geography ya maeneo yeye badala ya kujibu hoja yeye anakimbilia kuwajibu wana siasa hapo ukiangalia upeo sasa wa viongozi wetu kitaaruma ni mzuri sasa naona anataka kuchangaya siasa na uwajibikji ndipo atakapo kwenda mlama sasa.

Madhumuni makubwa ya waandishi wa habari walipaswa kumweka kati Prof Muhogo atupe ufafanuzi kamili, kile alicho kisema kuwa Dar inachangia pato 80% katika Taifa, me natakuwa na maswali mengi ya kuiuliza serikali.
Mfano tu Serikali mpaka sasa inashindwa hamia Dododma kwanini? nalo watasema Dodoma haichangii pato Taifa ndio maana hatuwezi endeleza miundombinu pale Dodoma ili tuamie au? Wajua Ufinyo wa mawazo na kuto kuwa na akiri ya ufumbuzi wam mambo ili tuendelee ndio huu wa viongozi wetu tulio wapa madaraka.

Hapa ni kumaanisha Dar ndio TANZANIA period. na hii ndio inavigezo vyake kwani mfano tu huo wa prof Muhogo wa kudai Dar inachangia pato kwa taifa 80%, pili Madaktari walipo goma last year wengine si walihamishiwa mikoani na hwa kwenda kwanini hakuan vitendea kazi kwahiyo Muhimbili ndipo kuna vitendea kazi wakati walitajaa pia hakuna vitendea kazi sasa ukichanganya mambo hapo utagundua tu kwanini watu wana lazimishia kuhamia Dar si mtu katokea rudewa tandahima nyambiti nyamongo ifakara wote wanataka kuja Dar hii ni kuonyesha jinsi gani serikali yetu hajiwezi kujipanga kabisa katika kukuza na kuendeleza mikoa huku wanaendelea kuongeza mikoa yaaani ni shida tupu.

My Take:
Waaandishi wa habari twaaombeni sana kuweni walimu pia katika taifa letu pia mtupe muhimu kweli yatakayo tukwamua tuliko na kuachana na ushabiki wa kuuza magazeti au kuwa kweze viongozi hawa tulio nao.

Star TV mjitahidi kuongeza TV stations nyingi Nchini ambako mnaweza mkarusha matangazo yenu Live pia.

Back
Top Bottom