Kwanza swala la kujiuliza Wazanzibar ni kina nani, na wametoka wapi. Na ndipo swala la muungano litakuwa na ufumbuzi.
Katika swala zima la muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Jambo la kwanza la msingi ni kufahamu historia yako, pamoja
uhalali wa watu na uhasilia wao, mbali na upotoshwaji wa Waarabu, Wapershen na wahindi. Ambao wanataka kuirudisha
Zanzibar katika karne ya 16. Chini ya mikono ya watu wa Oman, in the way of " Conflict of interest " kwa sababu crud oil
inawasumbuwa vichwa vyao, na kuwaza tayari wameshakuwa matajiri wa haraka haraka. Kunako miaka 3,500 iliyopita
wafanya biashara na wavumbuzi wa wa Kiegyptian, wa Kichina, wa Kiroma, wa Kigiriki, wa Kipershen ambao ni wairan,
wa Kihindi na wa Kiarabu, waliitumia Zanzibar kama kituo kwa kusimama na kupumzika katika misafara yao.
Watu wa kwanza kwenda " Unguja " ni wabantu kutoka Bara la Afrika. Wandengeleko, Wamakonde, Wanyamwezi,
Wasukuma, Waha, Wanyarwanda na makabila mengine zaidi. na hiyo inakisiwa ilikuwa kwenye karne ya 4 A.D.
( 4th Century A. D. )
Katika mwaka 1698 wa Oman walidai rasmi kama kisiwa cha Zanzibar kipo chini ya utawala wao.
Katika mwaka 1840 Sultan Seyyid Said wa Oman aliondoa makao yake ya usultan kutoka Muscat, Oman na kuhamia Zanzibar.
Zanzibar ilibakia kuwa Capital ya Sultanate ya Oman mpaka hapo Sultan Seyyid Said alipofariki mwaka 1856.
Tokea muda wote huo mpaka kufikia mwaka 1964 yalifanyika mapinduzi ya kumuondoa Sultan katika madaraka.
mapinduzi yaliongozwa na Hayati Karume ambaye familia yake ilitokea Rwanda. " Unguja " ni jina la asili ya hapo, na
lilipokezwa na jina la Zanzibar kutoka kwa Waarabu, Zinj, in maana " Weusi, " na al - Bar, ina maana " Nchi ya. "
na hiyo ndio " ZANZIBAR " ina maana " Nchi ya Weusi " sasa basi ikiwa Sultan wa Kiarabu tokea mwaka 1698 anakutambua
kama wewe ndio mwenye kisiwa cha Unguja sasa kwa nini na wewe usijitambue na kuweka sawa hatma ya muungano.
Wote tuelewe kama civilization ndio imetufanya tuwe na status za muungano. Kiukweli hiyo ni sehemu asilia ya Bara kama
Kilwa na Mafia. mjielewe kama karne ya 4 mlitokea Bara wakati huo Tanzania inaitwa " Pwani ufukweni kwa wale watu wapole "
Kwa Kiarabu " SAWAHIL " " Pwani, Ufukweni au watu wa pwani " na hii lugha tuliyonayo ndio imezaliwa kutoka katika neno
ilo la Kiarabu. Kufikia mwaka 1885 - 1919 Tanzania yetu ilikuwa inaitwa " GERMAN EAST AFRICA " na jina ilo limetokana na
kampuni ya Kijerumani iliyokuwa ina colonized nchi yetu ukijumlisha Rwanda na Burundi. Jina la " TANGANYIKA " ni jina
asilia kutoka " Ziwa Tanganyika " na lilianza kutumiwa na Waingereza mwaka 1919. Baada ya Mjerumani kushindwa vita
vikuu vya kwanza, na nchi yetu kuwa chini ya udhamini wa umoja wa mataifa chini ya usimamizi wa mwingereza. na
wakati huo huo kupoteza majimbo mawili ambayo yalichukuliwa na Mfaransa na kufanywa nchi ya Rwanda na Burundi.
Si unaona sasa hapo Wzungu na Waarabu walivyotugawanyagawanya. Swala lingine bado amjajielewa la udini kuzarau
dini zingine ni makosa makubwa sana. Tuelewe kuwa Wamissionary ndio wliosimamisha utumwa Zanzibar. Na kumlazisha
Sultan Seyyid Barghash tarehe 6 june 1873 kuliondoa soko la watumwa. Na badala yake wakajenga Kanisa la Kikatoliki.
" JOSEPH CATHEDRAL. " Pale Stone Town, TUMETOKA MBALI NA TUELEWE KULE TUNAPOKWENDA. hii ni kwa ufupi
jihabarishe zaidi kuelewa tulipotoka.
Click Here:
Seton Hall | Law - About Zanzibar
Historical Sites of Zanzibar