Upo Firstlady ni hivi,
Nguo:napendelea kuvaa kuendana na umbo langu pia kutokana na occasion. Mf. nikiwa beach basi lazima niwe na vazi la ufukweni mana napenda sana kuogelea.Kazini kikazi zaidi.. Kwenye sherehe kadhalika vazi rasmi la mtoko kuangaliana na mazingira ya hiyo sherehe yani kama na washkaji au wazee wetu..Pia nashona vitenge kadhaa na hakika natafutaga rangi/muundo wa mshono unaoendana nami..Sipendi kuvaa nguo oversize au imenibana wee mpaka nashindwa kuhema/kukaa..
Viatu:napenda flat, sneakers na hata high-heels inategemea navaa kwenda wapi au nimevaa nini..
Nywele: huwa napenda kuzitengeneza saluni yani ku-relax na kuzipasi zinyooke mara nyingine nabana stlye mbalimbali ila sijawahi kuvaa weaving na kusuka ni mara chache sana...
Make-ups: kwakweli hii idara naona bado sijaiwezea..mafuta ya nivea au baby johnson ndiyo napaka sanasana naongezea powder. laa, lip-shiner/glow huwa siachi kupaka kwenye lips.
Handbags: naona hapa ndio kwenyewe, nina rangi mbalimbali ambazo namechisha na viatu tu..yani handbags nazobeba lazima ziendane na viatu kwa rangi..
Accesories: Saa muhimu mkononi, bracelets na kidani shingoni kutokana na nilichovaa..mkanda pia kama niko nguo yenye kuhitaji basi haikosekani..