JF Ladies....Arusha Wing...DINNER....

Status
Not open for further replies.
ila angalia kwenye mada kunasemaje kuhusu wanaume hamruhusiwi hapa
 
nimekubali best na nimekuelewa bestito
karibu
 
mngesema kwa member wote wa uku bila kuweka limit
 
mngesema kwa member wote wa uku bila kuweka limit

Mkuu.......wazo lako ni zuri.......ndio maana tukasema.......Arusha Wing.......ila na mikoa ya jirani wanakaribishwa..........sidhani.....japo inawezekana....... mtu wa Mtwara au Mbeya akasafiri kwa ajili ya one day dinner......
 
Nendeni dukani kwa mromboo ama daraja mbili kuna madhari mazuri sana yenye utulivu wa kutosha kwa nyie kujadili na kupata kubadili mawazo, mkitoka hapo muende Snake park ama kwenye maporomoko ya maji kule Oligilai.

Wazo tu!
 
ushauri wangu ni huu:

1. Ni vyema mkajikusanya na kujenga familia ya wanawake wa jf pamoja huko arusha na kuangalia uwezekano wa kusaidiana kwa wale ambao bado hawajafikia hatua ya azma zao.

2. Kubuni mbinu za kibiashara na kutafuta masoko nje ya arusha au nje ya Tanzania kiujumla.

3. Kusaidia kama kuna mmoja wenu hana cha kujishughulisha nyie mnamsaidia kwa kumwezesha mtaji wa kuanzia biashara yake atakayoweza kuifanya.

4. Kufungua saccos yenu ndogo ambayo itawawezesha kupata miikopo kwa wanachama wenu na kuweka akiba mbeleni

5. kingine kununua hisa au kuwekeza katika hisa hii nayo inalipa sana na inakufanya usiwe mwoga kwenye wimbi la biashara

6. Kuwaona wataalamu/ washauri wa mambo ya kibiashara ili wawape somo la biashara au semina ya biashara (mm mwenyewe naweza kuja kuwaelimisha kuhusu mambo ya biashara na ujasiriamali)

7. Kujua changamoto na mbinu za kukabiliana nazo wakati mnafungua biashara yenu au shughuli yoyote ile

8. Kuwaona wafadhili au nyie wenyewe kujifadhilisha ili kuinua kikundi chenu na kuleta maendeleo na sio kuwangoja akina baba wawasaidie au wawape fedha za matumizi, changamkeni kwani WANAWAKE TUNAWEZA.

9. Kuwasaidia wasichana wenye matatizo ya kifamilia au wale masikini kuwasomesha kwenye kikundi chenu mpaka na wao wafikie malengo kama yenu.

10. Kuwainua wasioojiweza hususani wamama watu wazima au wazee katika kuwapa mbinu za kijisiariamali na wao wakawa wanajiishughulisha mfano halisi ni KILIMO KWANZA kinalipa sana na hata nyie wenyewe mkianzisha shamba la hekari 10 - 50 mkawa mnakodisha vijana wa kuwalimia na kupanda mazao nanyi mnafanya kazi ya umwagiliaji tu baada ya msimu mwingine mnashangaa mmepata mazao ya kutosha kwenye shamba lenu na mkasaidiana kwa kile kiasi mpatacho kwenye hayo mazao.

Yangu ni hayo tu bestito Preta nikiwa na maoni mengine nitayaweka hapa

ciao
 
Last edited by a moderator:
mawazo swadakta ladyfurahia........na ningeomba basi uwepo ili tuweze kufaidika na upande huo wa ujasiriamali.......
 
Last edited by a moderator:
Halafu mkitoka hapo muanze kusengenyana...oh flani sijui 'weaving' lake liko hivi....mara 'ah yule naye anajidai'.....mara sijui nani ana shepu kama Betina...mara bibi mwafulani kakaa kama Zena.....
Haha'ha kweli maana wanawake tuna mambo,lakini naamin watu wa chuga hawana hzo makitu
 
me ntajitahd maana nipo moshi,naamin tutafanikiwa
 
na nyie kwa ubaguzi hamjambo ,,,,,

mara utasikia haki sawa.........

mara sijui WAMA............

mara sijui ustawi wa jamiii......

mara sijui viti maalumu...........

ilimradi tu muwe na kitu chenu binafsi........
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…