JF jikumbusheni matukio yenu mwaka huu wa 2011!!. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JF jikumbusheni matukio yenu mwaka huu wa 2011!!.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Maalim Jumar, Jun 7, 2011.

 1. Maalim Jumar

  Maalim Jumar JF-Expert Member

  #1
  Jun 7, 2011
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 1,443
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Habari zenu Greaters T.
  SI VIBAYA KWA WALE WANAOAMINI NA WAJUE MAMBO HAYA (KUJIKUMBUSHA)......


  MATUKIO YA KILA NYOTA 2011.
  MTABIRI: MAALIM ABALHASAN JUMAR.


  1-Kondoo(Aries) Machi 21-Aprili 20.
  Mwaka huu ni mzuri hasa kwenye mambo yanayohusu ilmu.Utapata nafasi ya kuongeza ujuzi ulionao.Mipango ya safari za mbali ni muda muwafaka.Namba yao ya bahati mwaka huu ni (10).
  KIPATO: Jitahidi uongeze ufanisi wako au ujuzi wako ili uimarishe kipato chako. Ajira utayoipata itakuongezea mafanikio makubwa sasa katika maisha yako. Hili iwapo huna mikosi(mabalaa).
  MAPENZI: Utadumu kwenye upendo wako au utapata ushirikiano hasa ukishirikishaa ndugu zako. Salaam mara kwa mara zitakuongezea upendo kwa umpendae. Fikra zako binafsi ndio zitanusuru uhusiano uliopo.
  AFYA:Utasumbuliwa zaidi meno,kichwa itasababishwa ajili ya kipato au ajira uliyo nayo.
  UADUI: Utaibiwa mara kwa mara hali hiyo itakuongezea hofu nyingi.Pia taarifa nyingi zitakutia hofu.

  2-Ng’ombe(Taurus) Aprili 21-Mei 21.
  Mwaka huu ni muda muafaka kuongeza ujuzi au kwenda kupata ujuzi zaidi.Utaandamwa kwa maneno/kesi zaidi.Kazi zitakunyanyua katika maisha yako.Namba yako ya bahati ni (11).
  KIPATO:Utapata kupitia rafiki zako.Mialiko mingi itakuongezea kipato chako.Taarifa nyingi ndio zitahatarisha kipato chako.Utatuzi wahitajika zaidi.
  MAPENZI: Zingatia ushauri wa wazazi wako kwenye mahusiano yako.Siri nyingi zitakuharibia matarajio yako kwenye mahusiano.Matatizo yataanzia hapo hapo ulipo.
  AFYA: Maradhi ya wasi wasi yatakuandama. Hutosikia vizuri,sauti kukwaruza mara kwa mara.
  UADUI:Utaharibiwa mipango yako au kuandamwa zaidi ajili ya mbinu zako katika maendeleo .

  3-Mapacha(Gemini) Mei 22- Juni 21.
  Mwaka huu utajazwa swifa nyingi za ukweli/uongo pia utasaidiwa. Hali hiyo itakuongezea raha.Muda muwafaka kupata hifadhi kwa kila kitu chako. Walio karibu nawe watasafiri mbali nawe!.Namba yako ya bahati ni 21.
  KIPATO: Subira yahitajika kwenye kipato chako.Utadanganywa hali ambayo itakuharibia mambo yako.Utafanyiwa kila hila(ujanja) ili uharibikiwe.
  MAPENZI: Utaempata ndie anae kufaa maishani . Hali itayojitokeza ni vizuri uwe mwenye subira ili usizae nje ya ndoa!.Utapoanzisha uchumba haraka utakubalika.Shida zahitajika utatuzi.
  AFYA: Maradhi yatakua chanzo kwa kutofanikisha mipango yako ya makazi.Utasumbuliwa zaidi kupumua/mikononi maumivu/kuwashwa.
  UADUI: Migogoro itaanzia kwenye kazi /biashara zako.Hali hii itaendelea hata kukuingiza kwenye mashauri yasio makini.

  4-Kaa (Cancer) Juni 22- Julai 23.
  Mwaka huu maradhi yatazidi kukuandama.Utazidi kua mnyonge…utasengenywa(kutetwa).utakua kwenye wakti wa kujikatia tamaa.unahitaji kupewa ushauri na kupatiwa utatuzi zaidi.Namba yako ya bahati mwaka huu ni 22.
  KIPATO:Utakachokianzisha kitaleta faida/kuendelea japo kiduchu.Ndugu/marafiki zako watakua ni wenye msaada kwako.Uheshimu zaidi mawazo yao.
  MAPENZI:Uhusiano wako utakumbwa na migogoro/mizozo ya mara kwa mara. Hali hiyo itadumu na itakua tatizo endelevu.Unaweza kujitahidi na uwe mwanye ustahamilivu ili kutengana kusitokee.Kwa hili utatuzi wahitajika haraka.
  AFYA:Usiendekeze starehe zaidi kwa kua humo itakuharibia swiha yako.Mazingatio ya swiha ndio itakuwekw hali iwe vzuri au mbaya.Akina mama mtasumbuliwa maeneo ya uzazi. Maumivu ya kifua ni wanaume na wanawake.
  UADUI: Misaada utayoipokea ndio itakua chanzo kukuharibia mipangilio yako.Uwe karibu yao marafiki zako hata ukigundua mabaya yao..wewe usiwaoneshe chuki. Tahadhari zako ziwe za rohoni(usiri).

  5-Simba (Leo) Julai 24-Agosti 23.
  Mwaka huu ni mwafaka kujihudumia kwenye afya au kujichunguza hali ya mwili wako/akili(mawazo)yako.unayo nafasi kuanzisha biashara/uchumba/kujenga…yatatimia ukiwa huna mikosi(mabalaa).Namba yako ya bahati mwaka huu ni 23.
  MAPENZI:Mahusiano yataendelea.Ulienae atazidisha migogoro/magomvi.Wanaotafuta mahusiano utaekutana nae anafaa zaidi.Ajili ya mahusiano yako vitu vingi vitapotea!.
  KIPATO:Muda muafaka kuifuatilia ajira .Waliopo kwenye vyanzo vya mapato yao ni muda muafaka kutekeleza yote yalio muhimu ili kuepuka majuto.Epuka matumiziyasio muhimu(starehe).
  AFYA: Utasumbuliwa zaidi maradhi ya manjano(Jaundice) moyo(Bp) hali hiyo itakukosesha utulivu. Pia utaongeza ukorofi…jitahidi upate utatuzi wa hayo.
  UADUI: Maneno mengi utayosikia au kuambiwa vizuri ufanye subira ili usifikwe na matatizo makubwa.Hali hii itakua inajirudia mara kwa mara.

  6-Mashuke (Virgo) Agosti 24- Sept 23.
  Mwaka huu huzuni zilizopita ujitahidi na unaweza kujiandaa kujiweka vizuri..hali hii itafanikisha iwapo huna mikosi.Mipango ya mali/kipato itaimarika. Yote uliohitaji kununua ni vyema ukatekeleza haraka. Ubakhili wako si vzuri /si suluhisho.Namba yako ya bahati mwaka huu ni 3,6,9.
  KIPATO: Endelea kufuatilia mikataba yako au ahadi zako hasa za kuongeza kipato.Yote hayo vizuriuwe mwangalifu.Kudanganywa au kuzidiwa kutajitokeza.Mipango na utimilifu wa ahadi iwapo huna mikosi.
  MAPENZI: Utadanganywa katika mahusiano yako na hali hiyo itajitokeza zaidi.Hofu zitaongezeka hali hiyo itamshitua mkeo/mumeo/umpendae.Ukweli ni kidogo kwenye mahusiano ni vizuri uwe mwenye subiri.
  AFYA: Umpendae vizuri umchunguze tabia(Afya) yaake.Mizozo iepuke ili ugonjwa wa shinikizo la damu lisikusumbue!.
  Mawazo yatakusumbua vidonda vya tumbo(Ulcer).
  UADUI: Uchijunge mwenyewe hizo misifa (Majigambo) ndio itakua sababu ya kuandamwa na kufanyiwa vitimbi.

  7-Mizani (Libra) sept 24-Okt 23.
  Mwaka huu misaada itahitajika kwa ndugu zako au watoto wao. Ni vizuri uwasaidie haraka watapohitaji. Upendo utaongezeka juu yako. Ndoto nyingi zitakusumbua mawazo yako.Mikataba ifuatilie kwa umakini zaidi.Namba ya bahati mwaka huu ni 7.
  KIPATO: Miradi yako au makampuni yako yataendelea vizuri. Mambo mengi yataendelea vzuri iwapo huna mikosi(mabalaa).Yote uliokuwa wayasubiri utayafahamu.
  MAPENZI: Mpenzi wako atakua mbali nawe! Vizuri uwafuate na kuzidisha mawasiliano nae.Utayohisi kwenye mahusiano mara nyingi yatakua yenye usahihi.Mahusiano yasasa ni chanzo cha mafanikio yako.Hili nalo iwapo huna mikosi.
  AFYA: Utasumbuliwa zaidi viungo au kichwa au mgongo hali hii itakuzidishia wasi wasinkwako. Jitahidi kutafuta tiba .
  UADUI: Utazidi kuandamwa kwa sababu ya kipato chako ili uharibikiwe.Unaweza kutafuta utatuzi pia!.

  8-Nge (Scorpio) Okt 24-Nov 22.
  Mwaka huu siri zako nyingi zitafichuka.Mambo muhimu kwako uyatekeleze ni kujenga/kununua kiwanja au shamba ikiwa unao uwezo.Hifadhi akiba zako.Ulilokua hujalifaham khatma yake sasa utalijua.Namba yako ya bahati mwaka huu ni 17.
  KIPATO: Kitaendelea kua chenye furaha.Matanuzi yako au starehe zako ni muda muwafaka. Vizuri upunguze hayo matumizi yako.Kipato chako kitakuinua zaidi mwaka huu.Wasaidie rafiki zako shida zao!.
  MAPENZI: Utafanikisha mahusiano mengi kupitia cheo ulicho nacho au nafasi utayokua nayo.Kutajitokeza mashauri ambayo yatakusumbua.Utatuzi wahitajika!.
  AFYA: Jitahidi ufuate utatuzi tatizo ulilo nalo Jitahidi uombewe du’aa kwa ajili ya afya yako ya kiakili.Ugonjwa wa haja ndogo na viungo vya uzazi vitasumbua.
  UADUI: Utaandamwa kwa ajili ya ukaribu uliopo.Hata hizo safariutazozifanikiwa itakua sababu ya kuhasidiwa.

  9-Mshale (Sagittarius) Nov 23-Des 21.
  Mwaka huu ni muda mwafaka kuwazidishia furaha watoto wako hasa kwenye majukumu uliyo nayo.Pia kwa watoto wa ndugu zako na jamaa zako.Starehe ni nyigi ambazo zitakuvutia hata utajisahau kwenye mambo muhimu.Mazoezi ya mwili ni muhimu kwa afya yako yafanyike mara kwa mara.Namba za bahati mwaka huu ni 3,6,9.
  KIPATO: Kitatetereka zaidi ajili ya afya yako au matatizo yatayokufika.KItu muhimu utakikosa pia itakuharibia mambo yako kwenye kipato.Muda mwafaka kutafuta kazi au shughuli bora zaidi.
  MAPENZI: Yataendelea kwa upendo.Misaada mingi itapatikana kutoka kwa mpenzi wako.Pia marafiki zako watakusaidia kudumisha haya mahusiano yako.Vizuri kujua kama huna mikosi …kama mikosi unayo hayo hayatotimia.
  AFYA: Inshaallah! Kwa sasa utawezeshwa kupata tiba sahihi katika haya maradhi yako.Maradhi yatayokusumbua zaidi ni mapaja,makalio.
  UADUI: Makazi au maeneo unayoishi itakua chanzo cha matatizo.Vizuri uwe mwenye subira na kujitahidi kutatua hali hiyo kwa uangalifu na umakini.

  10-Mbuzi (Capricorn) Des 22-Jan 20.
  Mwaka huu maradhi yatakusumbua mara kwa mara. Maradhi ya kuwashwa,majipuna maumivu ya mgongo.Mambo mengi hayatokuwa sawa.Utatelekezwa au kususiwa hata kufukuzwa kwenye mambo muhimu.Utatuzi muhimu wahitajika.Namba ya bahati kwako mwaka huu ni moja.
  KIPATO:Utadhulumiwa na kupoteza.Mizozo itajitokeza mara kwa mara kwenye kipato.Utafanyiwa vimbwanga ili uharibikiwe.HIli linahitaji utatuzi haraka.
  MAPENZI: Katika uhusiano huu hakuna ukweli kabisa!.Vizuri uwe mwenye subira kwa yote utayoyaona au kusikia …japo kwakoitakua ugumu wa kuamini…ni vizuri utilize hasira zako.
  AFYA: Magonjwa yatayokusumbua zaidi ni (gout) maumivu makali ya mgongoni.
  UADUI: Mipango yako ambayo itayokuletea mizozo ni ile utayojishughulisha kuhusu maisha yakosaidia kuliko kuleta ushindani. Ukiendekeza ushindani utaharibikiwa mambo yako muhimu.

  11-Ndoo (Aquarius) Jan 21-Feb 19.
  Mwaka ni mzuri kwenu hasa wenye kuhitaji wapenzi wa uhakika na wakweli.Mliopo kweye mahusiano mizozo itakua ni mingi…pia yahitaji uvumilivu ili kudumisha mahusiano yenu ya upendo.Mwaka huu jitahada ni nyingi kwenye hili(Growing spiritual).Namba yako ya bahati ni (11).
  KIPATO: Uhakika si mkubwa kwa kua wasiwasi nimwingi.Vizuri kuyalipa madeni yako bila kuhofia kipato chako ukifanya hivi itakuongezea bahati zaidi au baraka.Utapoteza sana kwenye mali zako au vitu vyako.Utatuzi wahitajika.
  MAPENZI: Unao wahitaji wengi waondio utaokutana nao.Vizuri utoe maamuzi kwa haraka kutekeleza azma yako.Mapenzi yatakua yenye faraja katika maisha yako ya sasa.Vizuri kuangalia afya zenu kabla ya kulianzisha penzi.Au ni vzuri kuangalia chochote kitacho husu yeye.
  AFYA: Macho yako hayatoona vizuri.Moyo utakua unashituka mara kwa mara.Yatayokua yanakusumbua jitahidi uyapuuze na upumzike zaidi.
  UADUI: Utatishwa zaidi na kususiwa kwenye mambo yako yatayokuletea faida.Hali hiyo itakuongezea unyonge.Si vizuri kuwaonesha au kuwadhihirishia chuki wote walio karibu yako.( Almighty Allah saves you).

  12-Samaki (Pisces) Feb 20-Machi 20.
  Mwaka huu mashaka ni mengi kwenye mipango yako.Ahadi nyingi hazitotimia.Mipango mingi haitotekelezwa.Utaibiwa na kupeteza zaidi.Unaoshirikiana nao kwenye shughuli zako nao watakuongezea mashaka zaidi.Namba yako ya bahati ni 30.
  KIPATO: Utayoyapangilia yatakuletea faida na kukuzidishia bahati. Safari ndefu au za mbali ndio zitakua chanzo kukuongezea mali.
  MAPENZI:Unao pendana nao ni chanzo cha kuzidi huu upendo.Mizozo itahusu mali(kipato). au cheo chako.Hali yeyote itayo jitokeza inahitajika uwe mvumilivu.Utatuzi wahitajika!.
  AFYA: Mafua yatkusumbua zaidi pia shinikizola damu. Na huo mgongo . Haya maradhi yatakua chanzo cha maumivu mengi mwilini.Maeneo ya kifua na magotini yatasumbua.
  UADUI: Mizozo kwenye uhusiano ndio sababu kubwa itayokuongezea huzuni.Lipa madeni yako ili uepuka uadui na unyonge.  Mawasilano na mtabiri: MAALIM ABALHASAN JUMAR.
  Phone; 0713-351781.
  e-mail: mahjur45@yahoo.com
  Facebook: maalim.jumar

   
 2. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #2
  Jun 7, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  siamini kwenye nyota.
   
 3. Maalim Jumar

  Maalim Jumar JF-Expert Member

  #3
  Jun 7, 2011
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 1,443
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  kwanini usiamini?
   
 4. Maalim Jumar

  Maalim Jumar JF-Expert Member

  #4
  Jun 7, 2011
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 1,443
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  WATU WENGI HUA HAWAAMINI KITU CHOCHOTE IWAPO KUNA UBABAISHWAJI...
  HATA KWENYE MAPENZI HUA HIVYO HIVYO...SI KWAMBA MAPENZI NI MABAYA SWEETLADY!
  :smiling::poa
   
Loading...