JF imenifanya nikose hamu ya kufanya mapenzi

JF imenifanya nikose hamu ya kufanya mapenzi

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
23,707
Reaction score
57,211
Wakuu nisaidieni Ushauri wa kimawazo mdogo/rafiki wenu nimekuwa na mapenzi ya kupitiliza na simu yaani Sasa imekuwa too much.

Haipiti dakika tano sijachungulia simu yangu kuona nini kinaendelea hasa humu JF.Whatsap sio sana lakini JF ndo imenifanya nimekuwa mtumwa na sijui ni lini nitakuwa huru maana mambo ndo yanazidi kuwa mengi humu ndani.

Nikiamka asubuhi cha kwanza simu naingia JF Kucheki notification Kisha unread post.

Nikiwa nakula natafuta mada JF ya kusoma soma. Nikiwa kituoni nasubiri gari napitia pitia Jf nikiingia kwenye daladala hata Kama sijapata seat ya kukaa utakuta nakomaa na Jf hapo nimesimama tumebanana na abiria lakini lazima nitoe simu Kucheki JF.

Nikiwa kazini ndo usiseme yaani simu muda wote IPO kwenye chaji kisa JF.nimekuwa busy na Jf kiasi Cha kwamba Sina hata hamu ya kufanya mapenzi kwa Sasa yaani naona mwanamke wangu Ni JF.

Hivi hii Jf imewezaje kunikamata namna hii naandika kwa masikitiko makubwa naombeni mnipe ushauri wa kimawazo ili niepukane na matatizo Zaidi ya kisaiokolijia.

Lakini kwa wakati huohuo Jf pia imenisaidia Sana hasa kuniepusha na Mambo maovu Mambo mabaya mabaya.

Kwa mfano stori zikinogaga humu ndani nasahau kabisa hata kwenda bar au kwenda maeneo hatarishi.najikuta na enjoy tu humu ndani

Ndo hivyo wakuu Faida zipo Ila hasara Nako zinaninyemelea Kama nilivyoainisha hapo juu.

Yaani imefikia wakati nimekuwa mvivu mpaka kwenda Kusali msikitini kwa sababu ya Jf.MWENYEZIMungu nisaidie mja wako niweze kujiwekea ratiba nzuri ya kuchungulia JF.

NYONGEZA: MELLO NAOMBA KAMA KUNA NAFASI YA AJIRA HAPO OFISINI NIWE HATA MOD HII ITANISAIDIA SI NITAKUWA NATUMIA JF HUKU NIKIJUA NIPO KAZINI KWANGU.
 
uko mkoa gani mkuu... maana kila mkoa na wanawake wa tofauti kiuzur na maumbile.?
 
Ndege wote huwa hawana hamu ya kufanya mapenzi...
 
Tafuna "binjira" mbegu za maboga,kula tende na maziwa...kunywa maji mengi...
 
HII ADDICTION HAUKO NAYO PEKE AKO..NILIKUA NAIELEWA INSTA KWA KUSOMA VITU VINGI SANA ILA SIKU HIZI HUNAMBII KITU KWENYE JF

MOJA KATI YA ADDICTION MBAYA SANA NAMSHUKURU MUNGU SINA SMART PHONE MAANA SIPATI PICHA NINGEKUA TEJA WA AINA GANI.
 
Kama hujaajiriwa na Chama, basi mkuu una moyo. Ulifaa kabisa nafasi ya Pole Pole maana una jitihada binafsi za kutetea serikali ya Pombe hata kwa madudu ambayo hata chekechekea anaweza kutambua.


Pole kwa uraibu mkuu.
 
Kama hujaajiriwa na Chama, basi mkuu una moyo. Ulifaa kabisa nafasi ya Pole Pole maana una jitihada binafsi za kutetea serikali ya Pombe hata kwa madudu ambayo hata chekechekea anaweza kutambua.


Pole kwa uraibu mkuu.

Ilikua nikushauri ila kwa uzi huu mood imeniisha
 
Back
Top Bottom