JF Imekufanyia nini katika maisha Yako?

JF imenisaidia kupata ushauri wa kisheria ktk Jukwaa la Sheria. Baba mzazi leo hii angekuwa lupango kama si kudra za Mungu kupitia JF!
Mkuu hii kama ni kweli Mshukuru Mungu na ishukuru JF halafu mkuu ichangie kidogo hata ka hamsini tu...
 
Nimekuwa raibu (addicted) na JF kiasi kwamba kila siku lazima niipitie kupata habari muhimu kabla azijamwagwa kwenye vyombo vingine vya habari hapa tz! Pia nimeunganishwa na JF Saccos.
Mkuu ni kweli hata mm now ni addicted....na hili la Saccos natamani na mm nijiunge...
 
nimeelimika na kuelimisha,
nimehabishwa na kuabarishwa,
nimeburudika na kuburudisha.
Hakika jf ni noma.
Tatitizo nimeathirika nayo, kila wakati nataka niwe jf.
 
Ni mengi mno nimejifunza JF. Sina cha kuwalipa kwa uhuru huu wa habari. Nikitaka kujua details za habari yoyote Tanzania ambayo inarushwa kwa kutafunatafuna na wengine basi napata details hapa Jamvini. Ni kisima cha habari. Nimekuwa kimawazo. Huko mitaani naitwa mzee wa Breaking news!! Kumbe nimezipata JF. Ha ha ha.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom