Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,897
- 6,933
Wakuu, heshima mbele,
Najuta sana kumtafuta partner humu JF yani pamejaa usanii hapa usipokuwa mjanja kama mimi unalizwa hivi hivi unajiona.
Kipindi kile nilikuja na swala la kutafuta mchumba hapa, kweli huyo aliyejidai mchumba alipatikana bada ya kuchuja chuja na kufanya trial and error. kumbe mchumba hakuwa mchumba bali tapeli wa mapenzi tu. mkasa ulikuwa hivi....... jamaa alisema yuko single na mara ya mwisho kuwa na msichana ni mwaka mmoja uliopita.baada ya kuchat sana kupitia mtandao huu wa JF na email ilibidi tupeane mawasiliano ya simu, na majina ya facebook account. Ukweli mawasiliano yalikuwa hot sana. Simu zilikuwa hazikauki, meseji ndo dahhh siwezi sema, kutwa kuchwa ni kuchat na kupena meseji za mahaba. Ila kwenye facebook friend list yake ilikuwa imefungwa huwezi ona nani ni rafiki yake na huwezi post kwenye wall yake pia.
Basi, sisi tukiwa kwenye mapenzi motomoto na kuliwazana (ila sikuwa mwepesi kutoa tundi ndio ninachoshukuru na kujivunia) kumbe jamaa ana girlfriend wake wa long mie sikujua, basi siku moja niliona friend request ya mdada mmoja hata simjui ameni-add mie bila hiyana kabla ya kumu-accept nikawa natumiana nae inbox kujua ni nani na ni wawapi.....bi dada akaniambia nimuadd kwa faida yangu, ila akawa anadadisi sana kuhusu mahusiano yangu ya kimapenzi, sikuwa muwazi sana hadi aliponitajia jina la facebook la huyu kiumbe tulokutana JF. Huyu binti alisema yeye na huyu fisadi wa mapenzi ni wachumba wa long time ila yeye anafanya kazi mkoani huwa anakuja dsm mara chache sana. Nilimuuliza kuhusu uthibitisho ili niamini maneno yake then alinitumia hadi ushahidi wa pics ambazo sio za kawaida yani za mitego mitego ya kimapenzi zinazoonesha wako na mahusiano live (picha zilionesha hata dates za muda wa karibuni), kuforwad emails za huyu kiumbe wanazotumiana kila leo za kimapenzi n.k.
Ukweli baada ya hayo yote hasira zilinipanda ila nikazituliza nikapata ujasiri wa kumuomba kijana anipishe tugawane ustaarabu. kijana alisita huku akisistiza nimwambie why, mie nikamwambia nimeona siwezi match nae, yeye akawa anasisitiza bado ni mapema mie ku conclude hivyo. Nilipoona anasisitiza nikamwambia live kwamba ana msichana mwingine hivyo ni bora nimpe nafasi ili apumue vizuri! Kijana alibisha hadi leo hii.., pamoja na kumforwadia emails zake lakini wapi bado anakataa.
Hili tukio nimeona nililete ili kuwaasa wasichana wenzangu na hata kaka zangu ambao nao wako kwenye process ya kuisaka ndoa wawe makini sana. mimi kwa hili naweza sema ni Mungu ameniokoa kwani nilikuwa ninaelekea mbali na kuzamia kabisa! huwa nimefikiria ilikuwaje huyu dada akanijua kupitia facebook? au alipewa password na hyu kaka? hapana Mungu aliamua kunionesha na kuniokoa.
Wanawake wenzangu na kaka zangu tumuombe sana Mungu ili atupatie wanaume na wanawake wa ukweli na sio matapeli.
Mbarkiwe sana.
Nimepitia maoni yenu wote, kwa mlionipa pole ninawashukuru sana. Ninaomba pia niweke wazi mambo yafuatayo
1. kuhusu kuonana live tulishaonana na alionekana ni innocent na mcha Mungu kwa maneno yake, pia kwa muonekano sio mtu mbaya au anayeonesha kuwa na tabia mbaya
2. Kwa waliokazia kuhusu ulaji wa tunda, sina haja ya kumdanganya mtu nisiye mjua na asiyenijua ukweli ni huo kwamba kamwe hakuwahi kuuona utupu wangu na kwa hilo siko na sikuwa mrahisi kwa yoyote yule. Kwahiyo kama wewe unalazimisha kuamini hivyo wewe amini tu upendavyo ila tunda ni langu na halikuliwa.
3. Watu hukutana popote na kufanikiwa kuwa na mahusiano yenye manufaa tu, hivyo kukutana na mtu online, street, kanisani au kwingineko hakucount ila ni aina ya mtu uliyekutana naye ndio inacount.
4. Hata kama ingekuwaje, bado ingekuwa vigumu kwa mimi kujua mambo ya mahusiano yake kwani mpenzi wake yuko mkoani kama nilivyokwisha elezea kwenye post yeye ndiye anayejua wanawasiliana lini na kwa namna gani.
5. Hii post iko hapa ili kuwapa somo wengine ambao kwa njia moja au nyingine wana mpango wa kuanzisha mahusiano ili wawe makini na kutojirahisisha kabla ya kujuana kwa undani iwe online, street n.k.
Otherwise michango yenu wote kwa upande mmoja au mwingine inajenga kutegemeana na nini unaamini as far as relationship is concerned.
msichana ukishamchoma na kumuacha anakuwa mkali huyo dah!. atakusema hadi ujute kwanini umemchoma. utasikia ooh..umeniharibia maisha, kumbe maisha yaliharibika kabla hata hamjaonana. mapenzi si mchezo aisee. unaweza ukafa au ukawa tahila. mi ndo maana huwa sitongozi.
Hata wanawake nao hivyo hivyo wengi wao unakuta mwanamke anawanaume zaidi ya mmoja na anawapanga kama foleni ya ATM za NMB na hawajuani
...........aisee..:ballchain:Ngoja nikitafute.
hahahaaaaaaaaaaaaaa.... sasa hii si avatar tu ajamni??Pole Nakadori, mitandao hasa hii ya kijamii haifai, hebu cheki hii video Clip uone jamaa alivyokutana na Jini mtandaoni
duh nimebaki naduwaa.....huyo dada amejuaje kuwa unataka kuanzisha mahusiano na huyo kaka mpaka akufuate???.......lol pole lakini....mie nahisi ungemtaja humu tumjue...NAME AND SHAME HIM????????????????........kazi kuvizia tu humu hana haya loh,ukute kashawadanganya kibao kwa gia ya ndoa....mmmmmmnh......
Nakubali kabisa wapo wanaume matapeli lakini huu ushahidi aliotoa mtoa mada haudhibitishi kama kweli amedanganywa kwani ana uhakika gani kuwa alieyemletea email ni mwanamke fake na kwamba huyo ndiye aliyemzidi maarifa kwa kumdanganya ni wachumba. nasema hivi kwa sababu mazingira amabayo huyu dada amemfahamu mtoa mada hayako wazi na kuna kila dalili kuwa amezidiwa maarifa na mwanamke mwenzake.
Mkome kutafuta wachumba kwenye mitandao kwani mtaani hamuonekani???
Humu ni usanii tu
Chunga sana, kuna kisa kililetwa juzijuzi na mwana JF wa zamani kuhusu haya mapenzi ya kwenye mtandao kumbe mtu alikuwa unausambaza UKIMWI makusudi kabisa. Pole.
the only advice to men and women.... Be careful, most of social network love is just nothing more than a waste