JF Hip-hop frestyle battle

MMU inafundisha maisha/ bila hata ya kuficha/ kwa pamoja jamii inawakilisha/ na kwa wale wanaojifunza inaleta picha/ kwamba kuna mambo yanatisha/kuanzia mapenzi na kwenye maisha/

Madomo zege inawasaidia/ kupata wachumba kwa kujitangazia/ kila mmoja anaitumia/ great thinker na makapuku pia/

MMU inaleta raha/ sijawai ingia nikapata karaha/ inatoa ushauri na nasaha/
 
Mahusiano,mapenzi na urafiki,
Ndo jukwaa liongozalo kwa kiki,
Mada za ajabu mbaka unaogopa kulike,
Ukija kwenye koment basi zote zakinafiki,
Kuna wanaume wanajifanya mashost,
Hao ndio huongoza kwa kupost,
Ukigombana nao lazima itakukost,
Mana lazima waitane na kukufungia boost,
Kwa mada za kitandani hapa ndo mahala pake,
Ukitaka umaarufu we wasifie wanawake,


Nawasaidia wenye mada mana naona wanazingua tu.......
 
Yeah ah,kama dawa kama kawa
Nashiriki kamanda kuwawasha kama chawa,wadwanzi wote wanapagawa
Nipo kwenye list lakini sio shame
Ile fake iliyowapa sifa marehemu
Keti kwenye kiti ,shika biki
Chora jina langu leo nadhibiti
Nikitambaa kwenye biti ,kama nyani juu ya miti,walahi matozi wote leo hamnipati
Jf inanipa raha kinamna hii,nitawaburudisha jata nisipoifunza jamii
 
Labda wanaogopana ngoja wamalize kuandika maana najua wanaandika mimi.hahaha
Sijawao shindwa kwenye battle/ nikianza washa huu moto/ unanipambanisha na watoto/
ambao wanatumwa wakoleze moto/
mistari inatiririka kama maji kwenye mto/ nasubiri nani yuko tayar nimchape na fito/[emoji12] [emoji12] [emoji12] [emoji15]
 
Unakuja kwa njia ya kutaka kiki/ hiki kipaji hakiambiliki/ MMU iko moyoni akilini haielezeki/ jukwaa langu pendwa mdomoni halitoki/ sitaki like wala makofi/ nitasimama kuwaangusha mafisi/ wanaokuka kwa njia ya manesi/ na nishawastukia sasa nakuvalisha nepi
 
kiranga sikusomi keyon nasikia unamatatizo kila sehemu haupo stable kwa flow

leo nadeal nawewe ninja mimi brain yako haiko level your capacity ipo so low


again n again usiji 4c ku writ verse hii ni free style bwana mdogo leo umekutana na kisiki kamwe hauwezi toka drow

upo mwepesi sana hauna misingi unavamia kambi ushafel kwenye attacking rule today utaisoma show


am not your level first ask to daby i think u feel hard jipange wewe ni mtoto mchanga unahitaji mafunzo mengi ili ugrow
 
Hahahhaha kijana pole/ unajifanya mlokole/MMU imekushinda nenda kalale/ kule hatusimulianagi misukule/ ni mapenzi tu kwa kwenda mbele/ MMU siyo ya watoto wale wa babu tale/ kule tumejaa watu wazima tena tele
 
Hii battle adimu ka' mkwanja,
Usije kwa stim za ganja,
Take care Mc utakimbia uwanja,
Nawapanga kwa stanza mi kiranja,

Njoo nizuri, danger!!
 
Wakuu sijui kwanini tumeshindwa kunogesha huu mchezo. Kila mtu akichana kivyake sio mzuka. Ishu wajitokeze watu wa battle twende kwa mtoano au mchujo mpaka mshindi apatikane. Shida mara mtu kapotea hewani mara karudi. Please kama unataka battle kwasasa na upo free sema ijulikane.
 
Kwanza salam tena, usienijua unifahamu

Nilianza kuchana, toka enzi za jambo forum


Hadi leo nipo, nakita na mikito

Haikua easy, kwahiyo usichukulie simpo

Shujaa kama Ben sanane, We miss you bro

Sina Story kama @Bold kwangu ni flow flow

Wakongwe wananipa tittle bila noma wala zengwe

Flow zina target kaa sawa nikulenge
 
Hii battle adimu ka' mkwanja,
Usije kwa stim za ganja,
Take care Mc utakimbia uwanja,
Nawapanga kwa stanza mi kiranja,

Njoo nizuri, danger!!
Inajulikana, mtengwa real ni mmoja

Kwa hiyo mwana, kaa mbali we wakuja

Mnaiga hadi Id, Mnacopy kama surname

Wivu na mna hii,Mungu akurehemu

Nikikudiss sitafanya vyema

Nakuacha uSEPE TU, we madame WEMA
 
Nilianza zamani long kama Thursday kwenye TBT

Sio wewe new comer me old kama TVT

Nasambaza injili kama kanisa la E.A.G.T

Hata tuki battle wawili me ndo B.E.S.T
 
Inajulikana, mtengwa real ni mmoja

Kwa hiyo mwana, kaa mbali we wakuja

Mnaiga hadi Id, Mnacopy kama surname

Wivu na mna hii,Mungu akurehemu

Nikikudiss sitafanya vyema

Nakuacha uSEPE TU, we madame WEMA
Hata mtengwa wewe ni shit, vina vimepinda kama my morning piss/

Flow shit kama za mbwa koko, mwenzio sepetu wewe wa baikoko/

You are so local, your btch basic come have a coco/

Una flow umbuzi na utoto, njia nzima maboko/

Natumaini sijakukera acha ninawe mikono/
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…