JF EXCLUSIVE: DOWANS vs TANESCO, the saga continues!

Mkuu ni kweli alisema, na hoja yake ni kutafuta sababu tu. Miaka yote ya utumishi kati ngazi ya uwaziri hakuwahi kugundua hili? Mwanasheria mkuu ambaye ni mshauri wake hakuliona hilo na alimshauri nini. Kwanini asianze na kutafuta mwanasheria mkuu (AG) kutoka nje. Kesi ilipounguruma si walijua kuwa tuna wanasheria dhaifu (kama ni kweli) ilikuwaje wakamtuma yule wa Tanesco kwenye kesi kubwa kama ile ikiwa walijua kuna udhaifu.
Mambo yote yanajadiliwa katika baraza la mawaziri, je hawakuona udhaifu huo.

Kwa kujua hatuna wataalamu kulikuwa na shida gani kutafuta kutoka nje? mbona wao wakiugua wanakwenda kutibiwa na wataalam nje ya nchi.
Kuhusu copy and paste, mkuu sio kama walifanya hivyo kwa bahati mbaya, walijua kabisa lakini 10% ilishatembea. Tunakumbuka Dr Mwakyembe alisema hata mwanafunzi wake angeshinda kesi,ipo namna si kuwa hawakujua walifanya nini.

Kama wataalamu wa sheria wana walakini, je wanasiasa wanaofanya maamuzi ni competent? Rais katika kamati kuu alisema lazima walipwe, alipokwenda kuonana na wabunge akasema hawalipwi! sasa hapa ametumia wanasheria kumshauri, na kama yeye anayumba kiasi hicho tutegmee nini inapofikia hapa.

Mkataba uliohamishwa kutoka Richmond kwenda Dowans, hivi kweli ni jambo linalohitaji mwanasheria kutambua makosa! Rais alishajua kuwa kampuni haikuwepo hapo alihitajika elimu gani kubwa kiasi hicho cha kutambua kuwa yapo matatizo.
Nani amewajibika kwa suala hili kisheria. Kama tatizo ni wanasheria mbona upuuzi huo umejirudia TRL ingawa ni kwa namna tofauti.

Nakubaliana nawe kuwa wapi ambapo katika mikataba yetu tumeona wataalamu waliobobea kama maprofesa wakishirikishwa?

Kinacholiumiza taifa ni rushwa ya hali ya juu kwa viongozi wa serikali, na hakukuwa na dhamira ya kulimaliza suala hili kwa manufaa ya taifa.
Huwezi kuliongelea jambo hili bila kuwahusisha mapacha, baraza la mawaziri ambalo kiongozi wake ni Rais.Kwa mchanganyiko huo nani atamfunga paka kengele! na kwanini tuwalaumu wanasheria kwa makosa ya siasa yaliyosabababishwa na uingiliaji.
 
Reactions: EMT
The facts is: CCM refused to reveal who real brought DOWANS to Tanzania and nani alicheza hii deal na kutaka ku-blame the whole country on this. This is not going happen in our watch. Aliye-sign huu mkataba ni nani? Aliyekuwa mshahuri wa Tanesco/serikali kuingia huu mkataba ni nani?

Majibu mengi yapo na tunajua kwa upande wa Rostam yeye alikubali kama ni consultant wa DOWANS Tanzania wakati huo huo akiwa mbunge wa Taifa. How come CCM ina wabunge waliochaguliwa (fake as we know) na badala ya kufanya kazi kutetea Taifa ili lisijiingize kwenye hii mishimo ya debt crisis wao wakwanza kuleta deals mbovu ili lolote likitokea wananchi waishie kulipa? Facts zipo Rostam ali-lobby hii deal ofisi ya raisi mpaka ikapita na sasa tutaona sababu kubwa zilizomfanya aondoke na kujitoa ktk ubunge.

This isn't the end until Kikwete na serikali yake waje mbele ya nchi na kuonyesha record zote za deals za dowans na serikali ya Tanzania. Tunajua zipo deals nyingi sana Tanzania kama hizi...
 
Habari zilizopatikana zinadai kwamba mawakili wa Matrix ya Uingereza walidai kulipwa fedha za utangulizi kutoka Tanesco kiasi cha Paundi 500,000 za Uingereza zaidi ya Sh1 bilioni na kwamba fedha hizo zilikuwa katika mchakato wa kulipwa.

Source: Mwananchi
 
Hili la kukataa kusema nani anahusika sasa limekuwa utamduni.
  • Marehemu Daudi Bilal amefariki bila kujua alikuwa na nini moyoni. Tukafichwa hadi tulipoambiwa kafariki. Kila kitu kilikuwa ni siri, EPA ikafikia kikomo na hatutajua nini kimetokea.
  • ShailesheiVithlani yupo duniani kila wakiulizwa wanasema interpol inamtafuta lakini anajulikana yupo wapi anafanya nini.
  • Serikali ya Kikwete imesema haijui Kagoda ni nini na wameiba nini, ingawa haihitaji interpol na nyaraka na wahusika wapo.
  • Richmond haijulikani ni nini na ilidhuru vipi serikali na wananchi wa Tanzania. Hakuna anayejua ingawaje PM alijiudhulu.
  • Gire ameshinda kesi isiyohusiana na Richmond na hiyo imepita.
  • Merememeta ni siri ya jeshi na hatutajua nini kimefanyika.
  • DOWANS ni kama hapo juu, hatutajua nani amehusika hata kama wapo. Rostam alikana hana uhusiano na Dowans halafu akakubali.
  • Haya yote na mengine ni chini ya uongozi wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete.
Mwisho wake tunatafuta mawakili kwa pesa za walipa kodi, yaani tulipe wanasheria ili tushinde kesi ya wezi. Kwa maneno mengine tunawawekea wezi mawakili,wezi wakiwa wameshachukua chao na wanatumia pesa hizo hizo kununua maekari ya mashamba kutoka kwa masikini wale wale waliolipa ada ya wanasheria kwa kesi zao. Haya yote ni chini ya Uongozi wa Rais JK. Kikwete.

Tunakopa pesa na madeni kwa watoto wetu kwa umeme wa dharura, tunapindishiwa bei za umeme kwa makosa yasiyo yetu na ya makusudi.
Rais wa nchi yupo pembeni utadhani yanatokea India au Singapore.
Kama hatutasimama na kuzitetea nafsi zetu tukisubiri wabunge wa CCM basi wataendelea kuimaliza nchi yetu tunaona.
Mwisho tutalipa kodi ili zilipe mafao yao mazuri sana wakishamiliza miaka 10 ili wajazie 10%. Maisha ya vizazi vyao yanaimarika na kupendeza

Tudumishe amani na utulivu uliodumu kwa miaka mingi. Wajibu wetu ni kulipa kodi.
 
Old stories hakuna jipya ...wanataka ku-deviates attention yenu kwenye mambo haya..
 
Mkuu mi hayo maungwini ya kisheria huwa yananipa headache kweli. Hebu niambie kwa kifupi, ni nini kinaendelea kuhusu hii kitu ya DOWANS na TANESCO?
 
Hili ni bandiko la mwaka 2011, miaka 11 iliyopita, kuna kitu nilikisema, leo nimekithibisha, nilisema dawa ya deni ni kulipa!. Serikali Awamu ya 6, imelipa hili deni, na sasa mitambo ya Simbion ni Mali yetu.

Uthibitisho umepatikana from chanzo mamlaka.

Wewe as mwana JF, be the first to know, tozo ya Dowans tumelipa every cent, mtambo sasa ni mali yetu.
P
 
Watu wamelipwa, na kufanya acquisition ya mgodi wa madini ya thamani kuliko madini yote!.
Hili neno!. This is the role of the vibrant media kufanya IJ, kwanza aliyelipwa tozo ya Dowans ni nani, waliotufikisha hapa wamefanywa nini?.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…