Siri ya sifuri
JF-Expert Member
- Sep 21, 2018
- 2,615
- 2,264
Nawasalimu ndugu zangu,jamaa zangu,rafiki zangu washirika wenzangu na hata adui zangu kama wapo, najivunia kuwa mwana Jf kwa maana yakuniondoa kwenye upweke na kuniunganisha na jamii, kunipatia marafiki,kunipatia fursa ya kuungana na watu wa kila aina, wakiwemo wasomi,wajinga,werevu, matajiri, maskini,wakubwa na wadogo, nakuweza kujaniliana nao juu ya kila jambo linalohisu maisha yangu ya kila siku nakuniongezea maarifa na ujasiri wa kukabiliana na kila gumu ninakokutana nalo maishani bila gharama yoyote. Shukrani ziwafikie wakuu waanzilishi wa Jf kwa ubunifu wako, wakuu washirika wenzangu wanatoa maoni na kuchangia kila hoja kadri ya uwezo wako. hakika Jf ni kiunganishi bora na SALAMA kwetu. Asante.