Jeshi Vs mfumuko wa bei

Rockabie

Member
Nov 25, 2011
26
13
Jana katika taarifa ya habari ya TBC1 saa 2usiku nilistaajabu kidogo kusikia Mkuu wa kikosi cha wanamaji Meja jenerali Omari akilijuza Taifa sababu za kupanda kwa bei ni uharamia katika bahari Hindi. Sijui mi ndo sjaelewa au?maana nilidhani taarifa hizi zingetolewa na BOT au waziri wa Fedha kama vyombo vyenye dhamana na huyo Afande atoe sababu za kushindwa kukabili maafa ktk mafuriko ya Dar kwa wakati.
 
Suala la nani alitakiwa kusema sijui ila ni kweli maharamia ni moja ya sababu za kupanda bei kwa baadhi ya bidhaa. Hii inatokana na bidhaa zinazopita eneo lile kulipiwa insurance kubwa na hivyo kusababisha gharama kuwa kubwa.
 
Du kweli maswala ya uchumi yanasemewa na mkuu wa kambi ya navy haaaaaaaa,kwa mkulo msimtegemee jimbo lake limemshinda ndo utasema uchumi wa nchi
 
Jana katika taarifa ya habari ya TBC1 saa 2usiku nilistaajabu kidogo kusikia Mkuu wa kikosi cha wanamaji Meja jenerali Omari akilijuza Taifa sababu za kupanda kwa bei ni uharamia katika bahari Hindi. Sijui mi ndo sjaelewa au?maana nilidhani taarifa hizi zingetolewa na BOT au waziri wa Fedha kama vyombo vyenye dhamana na huyo Afande atoe sababu za kushindwa kukabili maafa ktk mafuriko ya Dar kwa wakati.

Sidhani kukesha wakilinda baharini kama alivyojieleza ni dawa ya kudumu.Dawa ni kuvamia somalia na kuikalia milele kama koloni la Tanzania kama tumeshindwa tuwaombe wakenya wakishawatimua waweke serikali ya wajaluo na wakikuyu kule na wapandishe bendera ya kenya kule.Hawawezi kuusumbua uchumi wetu kiasi hicho tukaendelea kukaa kimya .Hapa ndipo huwa nawpenda marekani uchumi wao ungeathiriwa kama huu wetu na wasomali marekani saa hizi majenerali wao wangeshatua somalia kuwanyuka tofauti na sisi ambao badala ya kukimbilia somalia kumtandika msomali wanakimbilia TBC kuhutubia.
 
naona kila alieshika kitengo sasa ni msemaji mkuu waserikali..............what a drama!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Huu uchumi wa jeshi na maharamia mimi sijamuelewa. Kwa hiyo hata Umeme wa Tanzania ambao ndo chanzo kikubwa cha bidhaa kuwa ghali limesababishwa na maharamia?. Hili jeshi nalo bado la chama kimoja tu. Hiyo semina elekezi aliyopewa inawalakini.
 
Ndiyo .Hata umeme unahusika sababu mafuta ya kuendeshea mitambo ya Umeme na matransformer yanatoka nje na kuletwa na meli na kusababisha gharama kupanda za usafirishaji kwa ulinzi,bima n.k

Suala ambalo sikufurahi ni kuwa kwa Generali kutoa statement ile atakimbiza hata hizo meli chache zinazokuja alisema statement moja kuwa hata wengine wanakuja sababu wana ulinzi wao ila hao wengine wanaokuja ni kwa sababu anadhani labda wana vichwa vigumu.Hii sentensi sikuipenda.Inaonyesha kuwa hatari ni kubwa sana huko baharini kuwa hata hao wanaojitosa kuleta mizigo ni kwa sababu ya ugumu wa vichwa vyao hawakutakiwa kuja.Sijui kwa nini alisema vile nadhani ile sentensi yaweza kimbiza wenye meli.Sijaelewa ile statement wahusika waichukue ile Telecast Ya TBC waiskilize tena nadhani ni vizuri mambo makubwa kama hayo si vema yakawa yanatolewa matamko na watu wazito kama majenerali yaweza gharimu uchumi wetu.Generali ni mtu wa kuaminiwa mno akisema kuna hatari kubwa baharini kwa meli ni rahisi kuaminiwa na watu wakatimka wasilete mizigo Tanzania.
 
nilichogundua , kila mtendaji siku hizi awe TISS , POLICE, JESHI , MGAMBO, WAFANYAKAZI WAKAWAIDA WA SEKTA YA UMMA, wote , wote wanajidai ni wanasiasa, na hii huwasaidia kujenga taswira kama mkuu akipenda wanaweza kumsaidia mkuu kutulisha propaganda za maisha bora na ujinga sababu za kushuka kwa uchumi due to external factors, ni dalili kuwa mkuu anapenda kusikia hayo na wanampa anayoyapenda
 
Huu uchumi wa jeshi na maharamia mimi sijamuelewa. Kwa hiyo hata Umeme wa Tanzania ambao ndo chanzo kikubwa cha bidhaa kuwa ghali limesababishwa na maharamia?. Hili jeshi nalo bado la chama kimoja tu. Hiyo semina elekezi aliyopewa inawalakini.

Mkuu, kwa mujibu wa mkuu wa Tz Navy, ni kuwa maharamia walikunywa sana maji ya Tz ndo maana umeme ukawa shida!
 
Jiandaeni na uhaba wa mafuta..... Hoja ishaanza kujengwa mapema ili iwaandae ki-psychology!! Baada ya miaka 50 CCM wanatujua mbele na nyuma.
 
Jeshi letu kama limegundua kuwa maharamia wa Kisomali ndio chanzo cha shida zetu mbona serikali yetu haijatoa tamko lolote kuiunga mkono Kenya katika harakati zake huko Somalia? Kilichobaki ni wao kila wakisikia watu wanataka kuandamana wanazuia eti Alshabab watashambulia? Hivi Alshababu tayari wana kambi zao au ofisi hapa TZ?
 
Huyo Jamaa Mwanajeshi sasa atuambie kuna haja gani sisi kuendelea kupoteza pesa zetu kugharamia ulinzi wa JWTZ ilhali yeye ameshakiri kuwa Jeshi letu limewashindwa hawa maharamia?
 
Haya ndo matatizo ya kutegemea bidhaa za nje. Tumeshindwa kuzalisha vya ndani matokeo yake tunaanza kulalamika uharamia. Sasa sijui na malighafi zetu tunazopeleka nje tutazipandisha bei au la.
 
ni jambo la fedhea sana kusikia matamshi yakukatisha tamaa kama haya, hawa wasomalia wamepigana wenyewe kwa wenyewe for years inakuwaje washinde jeshi letu lenye vitendea kazi vyote, tena lenye kufanya mafunzo ya mara kwa mara na wanamaji kutoka marekani etc!

kuna tatizo kubwa, inamaana taifa letu halina ulinzi dhabiti, siasa safi wala elimu stahili yakutuwezesha kupambana na mazingira! kiini macho cha ombwe la utawala dhaifu usio na chembe ya ubunifu, kuongoza nchi kwa matukio yaliyopangwa mithili yakutumia ramli badala yakufuata sera na mikakati inayotekelezeka

nina amini v soon mafuta yatapanda sana bse hao wenye vichwa ngumu watakapochoka itakuwa taabu sana, bt jambo la ajabu ni hili, mafuta tunayo, natural gas tunayo etc nilitegemea nchi nyingine ndiyo zilalamike usalama wakutoa mafuta gas n mazao ya chakula kutoka tz kukatiza somalia and not vise verse !
 
Hahahaaa! Ukiwa c mchapakazi bac lazma uwe mwingi wa sababu-ukweli ni kwamba serikali imeshindwa kusimamia uzalishaji kwa kutokuwa na forecasting nzuri ya demand vs supply. Hii imefanya nchi isiweze hata kujitosheleza kwa chochote kiasi kwamba we are importing everthng trash! Semeni kweli jamani-maana hata tooth-stick zinatoka china! By then ivi iyo marine-pirates inflation inahusika na meli zinazokuja tz tu au? Na je nini suluhisho la jeshi letu ktk hili?
 
Sidhani kukesha wakilinda baharini kama alivyojieleza ni dawa ya kudumu.Dawa ni kuvamia somalia na kuikalia milele kama koloni la Tanzania kama tumeshindwa tuwaombe wakenya wakishawatimua waweke serikali ya wajaluo na wakikuyu kule na wapandishe bendera ya kenya kule.Hawawezi kuusumbua uchumi wetu kiasi hicho tukaendelea kukaa kimya .Hapa ndipo huwa nawpenda marekani uchumi wao ungeathiriwa kama huu wetu na wasomali marekani saa hizi majenerali wao wangeshatua somalia kuwanyuka tofauti na sisi ambao badala ya kukimbilia somalia kumtandika msomali wanakimbilia TBC kuhutubia.

teh teh teh teh mkuu umenivunja mbavu
 
Ni porojo tu!! Kwa nini mfumuko wa bei uwe kwa Tanzania tu? Ni Tanzania tu tunaotumia bahari ya Hindi? Kenya na Rwanda mbona hakuna mfumuko wa bei!
 
Hii ndo Tanzania bhana, wachache wanakula rasilimali za nchi wengi twaumia.
 
Back
Top Bottom