Hivi sheria gani mnayotumia kukusanya michango kwa wafanyabiashara mjini babati. Ninavyofaham mm kama ilivyo kwa majeshi mengine, Jeshi la zimamoto ni kikosi halali kilicho chini ya wizara ya mambo ya ndani kama police nk. Kitendo cha wananchi/wafanyabiasha kuchangia jeshi hili ni cha nchi nzima? Je serikari imeshindwa kuhudumia kikosi hiki? Tunachangishwa pesa hizi kwa lazima na wakati mwingine wanasema watawapeleka mahakamani wale wote wasiochanga pesa hizo. Wanatumia kigezo cha watanzania wengi kutokujua sheria na woga wa mahakama na vurugu/vita. Wanachangisha pesa hizi na kisha wanatoa certificate tena zenye expire date na yaonesha hili zoeli ni endelevu. LEO TUNACHANGIA ZIMAMOTO, KESHO WAKIJA JWTZ NA SHERIA YAO TUTAGOMA? MSAADA KWENU MJUAO SHERIA. Hii cert mimi ninayo tena kwa jina langu.