Jeshi la polisi wanawasaka watuhumiwa wa mauaji ya mwenyekiti wa CHADEMA USA RIVER

Nadhani mafunzo ya Polisi siku hizi ni rasharasha, inawezekanaje askari akaporwa SMG na mhalifu? Polisi wajitafakari upya.
 
Hivi hawa makamanda na wasemaji wa jeshi la polisi wanapimwa akili kabla ya kupewa vyeo.Mbona wote wanashindwa kupangilia uongo.Je huyo askari alikuwa mwenyewe na je anadegedege au ndio anashindia viroba kupooza joto la kwenye zili nyumba zao

Kigezo kikubwa ni ukada kwa chama tawala na MAHABA Kwa watawala mkuu. Hapa zimeendelea kutumia mbinu zao na silaha zao wenyewe kujimaliza Mkuu.
 
Jeshi la polisi Mkoani Arusha inawasaka watuhumiwa wawili wa mauaji ya aliyekuwa mwenyekiti wa chadema kata ya usa river.

Watuhumiwa hao wawili walitoroka mahakama kuu kanda ya Arusha wakiwa chini ya ulinzi wa jeshi la polisi.

Akizungumza na waandishi wa habari, kamanda wa polisi mkoa wa Arusha ameeleza kuwa watuhumiwa hao walimsukuma askari, alipoanguka wakamnyang'anya silaha na kukimbia nayo.

Stay tuned! .............................. There is so much more to come!

this case rise more questions than answers.
 
Wamemtoa ili aendelee na kazi yake ya kuuwa maana waliobakia wameshindwa kazi hadi ikabidi CCM itumie Polisi kuuwa.
 
Danganya toto hii,wamewatorosha alafu wanazuga wanawatafuta.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums

Mtuhumiwa wa mauaji anapelekwa Mahakamani bila kufungwa pingu za mikono na miguu?! Lakini ikijulikana toka mwanzo kwamba mauaji yaliamriwa na mwekahazina wa CCM!
 
Jeshi la polisi Mkoani Arusha inawasaka watuhumiwa wawili wa mauaji ya aliyekuwa mwenyekiti wa chadema kata ya usa river.

Watuhumiwa hao wawili walitoroka mahakama kuu kanda ya Arusha wakiwa chini ya ulinzi wa jeshi la polisi.

Akizungumza na waandishi wa habari, kamanda wa polisi mkoa wa Arusha ameeleza kuwa watuhumiwa hao walimsukuma askari, alipoanguka wakamnyang'anya silaha na kukimbia nayo.

Stay tuned! .............................. There is so much more to come!

Duuh Bongo ni nomaaaa yaani huyu Kamanda na Ukamanda wake anasimama na kuongea ati yule jamaa alimsukuma Police akaanguka then akakimbia na bunduki hhahaha hahaha hahaha hii mbona ni Bongo Movie kabisa yaani hata mtoto wa darasa la kwanza hawezi kumuelewa huyu kamanda sasa kina Chagonja,Said Mwema si wajiuzulu tu kwa uzembe wao huu wa kuajili aaskari wajinga na wapumbavu.
Yaani Police wa Bongo wao wanajua kuua raia na kuiba mali za raia Lol yaani hata visimu vya Mchina wanaibia raia.Hii Bongo Movie kina Nepi,Said Mwema,kamanda wa Arusha,huyo Police kilaza aliyepokonywa silaha na Chagonja ndio walioicheza na Stering ni Kikwete Jakaya sasa ngoja tuone nani atakufa kwa hii Bongo movie maake pia Bongo Movies sometimes ziko so funny manake huwaga zinaisha kiaina.
 
Polisi kuwachunguza waliowalinda mahabusu waliotoroka
Na John Ngunge

Wakati polisi mkoani hapa ikiwachunguza wenzao waliokuwa wakiwalinda watuhumiwa wawili wa mauaji waliotoroka mikononi mwao, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, ametangaza donge la shilingi milioni tano kwa mtu au watu watakaofanikisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao.

Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Samwel Joseph Mtinange (26) au kwa jina maarufu Samu na Mohammed Shaban Limu (35) ambao pamoja na wenzao wanne Daud Lezire Mkumba (40), Mathias Kurwa (34), Said Florian Nkwera (26) na Swalihina Yohana (36) wote wakazi wa Usa, wilayani Arumeru, wanadaiwa kumuua aliyekuwa Mwenyekiti wa Tawi la Chadema Usa, Msafiri Johnson Mbwambo, Aprili 27 mwaka huu.

“Tunachunguza tukio zima la kutoroka kwa mahabusu hao, siwezi kusema polisi waliokuwa kwenye ulinzi kama wapo rumande au la, lakini tukio hilo linachunguzwa,” alisema wakati akizungumza na waandishi wa habari jana bila kutaja majina ya polisi waliokuwa wakifanya ulinzi huo.

Alieleza kuwa watuhumiwa hao walitoroka wakiwa wanatolewa mahabusu iliyopo mahakamani kupelekwa kwenye karandinga tayari kwa kurudishwa magereza.

Alisema katika tukio hilo askari polisi aliyekuwa amebeba bunduki alipigwa kikumbo na kuanguka.

Hata hivyo, Kamanda Sabas, alisema watuhumiwa hao hawakufanikiwa kutoroka na bunduki hiyo aina ya Sub Mashine Gun (SMG) ingawa habari zilisema baada ya kutoroka nayo waliitelekeza kwenye mto ulio jirani na mahakama hiyo.

Aliomba mtu yeyote atakayepata taarifa kuhusiana na watuhumiwa hao kutoa taarifa kwa polisi na kwamba zawadi ya Sh. milioni 2.5 itatolewa kwa kila mtuhumiwa atakayekamatwa.

CHANZO: NIPASHE
 
Polisi kuwachunguza waliowalinda mahabusu waliotoroka
Na John Ngunge

Wakati polisi mkoani hapa ikiwachunguza wenzao waliokuwa wakiwalinda watuhumiwa wawili wa mauaji waliotoroka mikononi mwao, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, ametangaza donge la shilingi milioni tano kwa mtu au watu watakaofanikisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao.

Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Samwel Joseph Mtinange (26) au kwa jina maarufu Samu na Mohammed Shaban Limu (35) ambao pamoja na wenzao wanne Daud Lezire Mkumba (40), Mathias Kurwa (34), Said Florian Nkwera (26) na Swalihina Yohana (36) wote wakazi wa Usa, wilayani Arumeru, wanadaiwa kumuua aliyekuwa Mwenyekiti wa Tawi la Chadema Usa, Msafiri Johnson Mbwambo, Aprili 27 mwaka huu.

"Tunachunguza tukio zima la kutoroka kwa mahabusu hao, siwezi kusema polisi waliokuwa kwenye ulinzi kama wapo rumande au la, lakini tukio hilo linachunguzwa," alisema wakati akizungumza na waandishi wa habari jana bila kutaja majina ya polisi waliokuwa wakifanya ulinzi huo.

Alieleza kuwa watuhumiwa hao walitoroka wakiwa wanatolewa mahabusu iliyopo mahakamani kupelekwa kwenye karandinga tayari kwa kurudishwa magereza.

Alisema katika tukio hilo askari polisi aliyekuwa amebeba bunduki alipigwa kikumbo na kuanguka.

Hata hivyo, Kamanda Sabas, alisema watuhumiwa hao hawakufanikiwa kutoroka na bunduki hiyo aina ya Sub Mashine Gun (SMG) ingawa habari zilisema baada ya kutoroka nayo waliitelekeza kwenye mto ulio jirani na mahakama hiyo.

Aliomba mtu yeyote atakayepata taarifa kuhusiana na watuhumiwa hao kutoa taarifa kwa polisi na kwamba zawadi ya Sh. milioni 2.5 itatolewa kwa kila mtuhumiwa atakayekamatwa.

CHANZO: NIPASHE
Hiyo ni moja kwa moja ni bonge la Movie! Baada ya ile muvi ya Kova ambayo ilipata umaarufu sana wakati wa utekwaji wa Dr Ulimboka, sasa IGP Mwema na RPC wa Arusha Sabas, wameamua kuiingiza sokoni hii muvi mpya ya muuaji wa kamanda wa CDM, Mbwambo wakijidai eti kampiga kumbo askari na kumpora SMG yake! Kwa akili za kawaida tu, hilo haliingii kichwani, kwa kuwa ninavyofahamu mimi mahakamani huwa kuna ulinzi mkubwa sana, hata kama huyo askari alizidiwa nguvu, huyo mhalifu asingeweza hata kwenda mita 100 bila kukamatwa na askari wengine wengi tu waliokuwepo hapo mahakamani! Kwa ushahidi wa mazingira, huo mpango utakuwa umesukwa na viongozi wa ngazi za juu wa magamba wakishirikiana na poliCCM. Sababu ya kufanya hivyo ni kutokana na kuelezwa kuwa huyo kamanda wa CDM aliyeuawa, yalikuwa maelekezo ya vigogo wa CCM. Sasa kwa kuwa inahofiwa kuwa huyo jamaa aliyetekeleza hayo mauaji, CCM walikuwa na wasiwasi naye kuwa angeweza kueleza ukweli wote na majina ya hao watu waliomtuma kutenda uhalifu huo!Kwa hiyo watawala wameona kwa kuwa umaarufu wa chama cha CCM unazidi kushuka kila kukicha, basi ni bora hii 'soo' ya mauaji ya Mbwambo waimalize kiaina kwa kumtorosha huyo mtuhumiwa!!
 
Back
Top Bottom