Jeshi la Polisi Uganda laomba radhi kumpiga mwandishi. Hapa kwetu mwandishi anafunguliwa kesi

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
_103119571__103114720_fireafp.jpg

Mwanzoni mwa wiki hii waandamanaji waliingia katika mitaa ya Kampala kudai kuachiliwa kwa mbunge Bobi Wine.

Jeshi la Uganda limeomba msamaha ambao ni nadra sana kutokea baada ya askari wake kuonekana kwenye mkanda wa video wakimpiga mwandishi wa habari ambaye alikuwa akitimiza wajibu wake kwenye maandamano ya kushutumu kukamatwa kwa mbunge Bobi Wine mnamo Jumatatu .Katika tukio hilo waandishi wengine nao walipigwa walipokuwa wakiarifu jamii juu ya maandamano hayo kupitia vyombo vyao vya habari.

Taarifa iliyotolewa na jeshi la polisi, ilieleza kuwa kitendo hicho kilichofanywa na askari wake kuwa si cha weledi na kusema kuwa watakamatwa kwa muujibu wa sheria za jeshi nchini humo.

Kumekuwa na mvutano wa kisiasa nchini Uganda baada ya mbunge Bobi, na wabunge wanne wa upinzani, kukamatwa wiki iliyopita.

Bobi ni maarufu nchini Uganda awali kutokana na kujihusisha na tasnia ya muziki kabla ya kuchaguliwa kama mbunge mwaka jana, amefanikiwa kuteka umaa wa wana Uganda miongoni mwao vijana, na kuendesha harakati za kisiasa dhidi ya raisi Yoweri Kaguta Museveni anaarifu mwandishi wa BBC aliyeko mjini Kampala Catherine Byaruhanga.
_103119575__102984991_gettyimages-812671438.jpg

Bobi Wine alikishinda chama tawala katika jimbo alilogombea na kuwa mbunge

Vijana wengi walioko sasa nchini Uganda walikuwa hawajazaliwa wakati raisi Museveni alipotwaa madaraka mnamo mwaka 1986.

Mapema wiki hii chama cha kutetea haki za binaadamu kilichoko mjini New York, kimewataka polisi na jeshi nchini Uganda kusitisha mara moja mashambulizi yao dhidi ya vyombo vya habari na waandishi habari nchini humo na kuheshimu haki za waandamanaji.

Katika video iliyorushwa mtandaoni, mwandishi wa habari wa shirika la Reuters James Akena, anaonekana akipigwa kwa fimbo na askari wawili mtaani katika mji mkuu, wa Kampala.

Kipigo kiliendelea kumuangukia mwandishi Akena hata alipoamua kusalimu amri na kuweka mikono yake juu huku akiwa amepiga magoti.

Shirika hilo la kutetea haki za binadamu linasema kupigwa na kukamatwa kwa waandishi wa habari ni ushahidi tosha kuwa wa mamlaka nchini Uganda wanataka kuficha mwenendo wa vikosi vya usalama nchini humo.Katika taarifa yake, Jeshi limejitetea kuwa awali lina uhusiano mzuri baina yake na vyombo vya habari nchini humo.

Mbunge Bobi, ambaye jina lake kamili ni Robert Kyagulanyi, bado anaendelea kusalia kizuizini na kwamba anatarajiwa kufikishwa katika mahakama ya kijeshi siku ya Alhamisi kujibu mashtaka ya umili wa silaha kinyume cha sheria.

Familia ya mbunge huyo inadai kuwa alishambuliwa vikali, lakini jeshi, ambalo linamshikilia Mbunge huyo , limekana vikali madai hayo.

Naye raisi Yoweri Museven amekanusha taarifa kuwa Bobi Wine ameumia na kwamba ana majeraha mabaya, na kuziita taarifa hizo kuwa ni habari za kupikwa.
 
Dikteta Mseven kakubali sisi huku mwandishi kapewa kesi na kaambiwa yeye ndo kamkunja polisi
 
Pressure na maandamano pamoja na tukio hili kulaniwa dunia nzima ndio kumewafanya washituke otherwise wangekaa kimya.

Africa, hasa Afrika mashariki na kati, ni eneo lenye watawala ambao wengi wao hawajastaarabika kabisa..
Acha uwongo nenda MASHARIKI YA KATI AU VENEZUELA!
Acha hiyo kijana mdogo haipendezi kabisa walahi!
That’s all
 
Kuna kaupepo kanapita East Africa ....Ngoja tuone ni kama ule wa Misri,Libya na Tunisia

Sent using Jamii Forums mobile app
Inatia wasiwasi kwa kweli hata huko ilianza kama utani hapo ndio nchi inatakiwa kuwa na watu kuangalia haya sio tuko busy na chaguzi za diwani. kama nchi tukae tujuwe tumekosea wapi tuwe kitu kimoja na sheria iwe juu ya kila mtu. Haki inaleta amani bila kupigana. ikifika sehemu mtu hajui atapaka haki yake wape ndio haya yanatokea. Amani hailetwi na jeshi au polisi ni vitu vitatu muhimu sana katika amani na maendeleo. Serikali/Katiba/sheria/security na mahakama vikiwa imara na Mahakama kuwa kama refa kuleta haki ikiwa huru kabisa hatuwezi kuwa na tatizo kabisa. kugombana au kutofautiana sio tatizo kabisa ni muhimu sana ila sote tunakuwa chini ya sheria na mahakama. sheria zitungwe kwa uadilifu sio kivyama.
 
Back
Top Bottom