Jeshi la polisi muwe na msemaji moja ;itapendeza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jeshi la polisi muwe na msemaji moja ;itapendeza

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pdidy, Jun 3, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Jun 3, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,595
  Likes Received: 5,776
  Trophy Points: 280
  Wabunge waionya Polisi ajali ya Mwakyembe
  Tuesday, 02 June 2009 16:33
  Na Edmund Mihale

  KAMATI ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama ya Bunge imelikata Jeshi la Polisi kuwa na msemaji mmoja katika taarifa linazotoa kuhusu matukio yanayogusa jamii na jeshi hilo.

  Hatua hiyo imekuja kutokana na taarifa zenye utata zilizotolewa na jeshi hilo, baada ya timu iliyoundwa kukagua mazingira ya ajali ya Mbunge wa Kyela, Dkt. Harrison kukataliwa na jeshi hilo kwa maelezo kwamba haikuwa sahihi.

  Taarifa ya ajali hiyo iliyotokea Mei 21 mwaka huu katika eneo la Ifunda, Iringa na kusababishia kuharibika vibaya gari na majeraha kwa Mbunge huyo machachari wa Chama cha Mapinduzi (CCM), imeibua pia imeibua hisia tofauti kwa wananchi na makundi mbalimbali ndani jamii.

  Akijibu swali la waandishi waliotaka kujua ni hatua gani zimechuliwa na Kamati yake kuhusu taarifa hizo tata za Jeshi la Polisi,Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Bw. Wilson Masilingi, alisema wametoa magizo kwa jeshi hilo kuweka utaratibu wa msemaji mmoja katika mambo yanayohusu taarifa za Jeshi hilo.

  "Tumewambia waache utaratibu kusema ovyo na wawe na msemaji ili wananchi wawaelewe, sasa ona katika taarifa hii mwingine ametoa taarifa, mwingine anasema taarifa hiyo si sahihi taarifa sahihi anayo IGP Mwema (Said) sasa wananchi wamuamini nani katika hili? alisema Bw.Masilingi.

  Alisema pamoja na kusemwa mambo mengi juu ya ajali za wabunge zilizotokea hivi karibuni ambapo pia Mbunge mwingine, Bw. Aloyce Kimaro wa Vunjo alipata ajali baada ya watu wasijulikana kutega mawe barabarani, Bw. Masilingi, alisema anaamini kuwa ajali hizo ni za kawaida na hazihusiani na mambo ya kisiasa kama inavyotafsiriwa na wengi.

  Akizungumzia ajali ya Dkt Mwakyembe, mhadhuiri wa Sheria Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt. Sengondo Mvungi, alisema taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi inatia shaka kutokana na mazingira ya ajali hiyo.

  Alisema hadi sasa anashanga ni kwanini jeshi hilo limeshindwa kulikamata gari lilosababisha ajali hiyo na kutoa taarifa inayoegemea upande mmoja bila kuhusisha dereva wa gari jingine.

  "Nimeisoma taarifa hiyo lakini inatia shaka sidhani kama taarifa hiyo imeandaliwa na wataalamu kutoka katika jeshi letu ambalo tunaamini kuwa ndilo lenye dhamana ya kulinda usalama wetu na mali zetu alisema, Dkt. Mvungi.

  Alisema kiutaratibu askari wa usalaama barabarani walitakiwa kuwauliza wenyeji walishuhudia ajali, madereva wote na kupima eneo la ajali, kisha kutoa maamuzi kutokana na mazingira ya maelezo ya mashuhuda na vipimo, lakini taarifa hiyo haioneshi kumhoji dereva wa gari la pili.

  Alisema haamini kama kweli jeshi hilo lilishindwa kulikamata gari hilo baada ya tukio kwani kutoka na uwezo wa jeshi hilo, lingesingeweza kufika hata umbali wa kilomita 20 kutoka eneo la tukio.

  Alisema kimsingi taarifa hiyo haikukamilika kwa kuwa haikueleza 'upande mwingine wa shilingi' na kumtaka IGP Said Mwema kupanga vizuri askari wake ili wasilitie aibu jeshi hilo.
   
 2. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #2
  Jun 3, 2009
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Polisi wetu wengi ni form four leavers na middle school, kwenye kujieleza ni std 7.
   
 3. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #3
  Jun 3, 2009
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,214
  Likes Received: 316
  Trophy Points: 180
  Unatutakia mabaya! Kupunguza wasemaji ni kurahisisha udanganyifu na kutunyima habari.

  Kuongeza urasimu kutapunguza UWAZI.

  Kwa sasa RPC ndio wasemaji. Ungetaka ikitokea ajali mtaa fulani Sumbawanga kuweko ukimya mpaka makao makuu Dar waseme? Miye nadhani ingefaa hata OCD wawe wasemaji halali wa Polisi.
   
Loading...