NAREI
JF-Expert Member
- Mar 10, 2017
- 1,730
- 1,665
pamoja na kazi kubwa waliyonayo ya kulinda RAIA na Mali zao lakini kuna jambo ambalo najiuliza mpaka kesho...!!
Iko hivi
Mnamo mwaka 2014 nikiwa chuo mkoani Mwanza, kijana niliyemwajiri kunifanyia kazi ya pikipiki kwa mkataba.( Boda Boda) kwa mkataba wa mwaka mmoja alitoroka na chombo changu na kuelekea maeneo ya mkoa wa Mara ( shirati). Baada ya kuwa hapatikani kwenye mawasiliano nikaamua kufuatilia ndipo nilipoambia na vijana wenzake wa stand kuwa muhusika karudi kwao na aliwadanganya kamaliza mkataba ilhali pikipiki ikiwa bado ni mpya ( approximately ilikua na miezi mi 3 hivi).
Baada ya hapo ilibidi nitafute kijana wa mwenyeji wa maeneo hayo ili niende nae. Safari ilianza toka Mwanza mpaka SHIRATI ( kwa wasiopafaham vizuri ni rorya kwa mbele) tulipofika nikaripoti kituo cha polisi SHIRATI.
Nikaaendelea na zoezi la kumtafuta mtuhumiwa ( kumbuka hapo hakuna hata saport ya vyombo vya usalama)
Nilihangaika kwenda Boda ya Kenya (GIBENI) na kurudi shirati zaidi ya Mara 2 au 3 kwa siku, ( hii ni kutokana na kupata taarifa kuwa pikipiki yangu pamoja na mtuhumiwa huwa anafanyia KAZI ya kubeba samaki kutoka sehem moja kwenda nyingine.
Nikifanikiwa kumkamata kwa ushirikiano mkubwa na wenyeji (WAJALUO) Mara baada ya kumkamata ilitakiwa nimsafirishe mtuhumiwa mpaka nyakato Mwanza ( ndipo nilipofungulia kesi) jambo la kushangaza nikaambiwa natakiwa nitoe laki mbili na thelathini ( 230,000) ili pikipiki yangu pamoja na mtuhumiwa tuende Mwanza kwa msaada wa mgambo kuhakikisha usalama wa mtuhumiwa. Nilishangaa kwanin nitoe pesa yote hiyo ilhali nilitumia nguvu zangu na za wanakijiji kumpata mtuhumiwa. (N.b pia nikaambiwa nikichelewa kufanya haraka ndugu zake wanauza ng'ombe watakuja kumtoa ni bora nitoe laki mbili na thelathini ili asafirishwe tena kwa gharama zangu kuanzia mtuhumiwa, mgambo,pikipiki na Mimi mwenyewe).
Ni bora ukipata tatizo la kupotelewa na Mali ukamaliza kwa namna nyingine lakini si kwenda kwa hawa jamaa. Nilitumia takriban laki 4 na 80 na mtuhumiwa baada ya kumfikisha Mwanza akaachiwa juu kwa juu baada ya ndugu zao waliouza ng'ombe kuja.
Hivi hawa jamaa wako kimaslahi au kutumikia raia???
Sent using Jamii Forums mobile app