Jeshi la polisi limfukuze kazi askari huyu mara moja!

jeshi la sasa limekua tu na tabia ya kuonea wasio kua na makosa wenye makosa wanawaogopa jaman police ndo kazi yenu uonevu mkikaa vituon mnataman tu rushwa kazi yenu nn sehemu ikitokea uhalifu ukiripoti huja mwisho wa tukio wahalifu wameondoka etii wanakamata wasio husika kwa uchunguzi kwa nn msiwahi kuja mkamate wahalifu waonevu sana nyie askari mnavitambi kukimbia hamuwezi kurusha ngumi shida ndo maana kuna sehemu nyingine wananchi wanachukia wana wapiga kwa ajili tu ya uzembe
 

Attachments

  • 1431085436473.jpg
    35.2 KB · Views: 711
Last edited by a moderator:

Kubebwa mgongoni kuna raha yake bhana,hadi askari wanaamua kukiuka maadili ya taaluma yao.si mchezo.
 
Hata Mimi limenistajabisha sana hilo.
Ila kwa jinsi ninavyowaona polisi hawana maana ningelikuwa mimi ningezama naye ndani ya maji huyo kwa kuchukulia kama bahati mbaya ili hali ni makusudi.
 
Kupanda daladala bure kulipitishwa na bunge la tisa, hivyo ni sheria inayotambulika. Kusihusihwe na kubebwa mdebwedo kama alivyo huyu makamasi.

spade4spade;
Huu ni wivu tu unawasumbua watu. Kwani mbona wengi tu wanabebwa? Angevaa kiraia ka askari kanzu nani angepiga kelele? Uzito hapo ni mabuti au mkanda?
Kama mnaamini alipanda bure, mkamateni atozwe jero au buku ka wengine. Na mbebaji tumsachi huenda ana msokoto au gomba mfukoni si bure
 
Mkuu nikuhakikishie tu kuwa ingekuwa ni kwenye nchi zinazoelewa ni nini maana ya jeshi huyu angekuwa kizuizini muda huu! Hiyo ni fedheha kubwa kwa neno 'jeshi'

Kwani jeshi maana yake ni kuloa...!!!! Pale wanajeshi, polisi, madaktari, usalama wa taifa na wengine unaowafahamu waliovushwa ni wengi mno. Sema yeye kavaa sare. Lakini yeye kuwa polisi hakumuondolei ile hali ya kuogopa mvua. Amefundishwa kulinda raia na mali zetu na hakufundishwa kuloa mvua. Na kama unaona hawezi kufanya kazi kwa kuwa kabebwa mgongoni basi vunja sheria halafu tumtume aje kwako ili tuone kama bado atakuwa mkakamavu ama atakuwa na hali ile ya kubebwa bebwa....!!!!!
 
Kumbe ni wale wale BAK MANI
Elli kama unaunga mkono afukuzwe basis mie napendekeza yule askari aliyetumia mbinu za kikomandoo kumficha Makonda kwapani pale Ubungo na kuokoa maisha yake asidhuriwe Apandishwe cheo. Pia Makonda apewe tuzo LA uvumilivu kwani pamoja na joto LA Dar aliweza kuweka pua yake kwenye kwapa LA Afande kwa dakika kadhaa tena kwa utulivu uliotukuka.
 
Last edited by a moderator:
Mafunzo ya Jeshi, kuna mahali pa kutumia Nguvu na Mahali pa kutumia Akili, sasa hapo huyo Askari katumia AKILI sio NGUVU
 
Kiukweli huyu askari hana kosa hata nukta, kamkuta mjasiriamali alieamua kuvusha watu kwa mgongo wake kwa ujira kidogo! Sasa kosa liko wapi ambalo huyo askari amelifanya!!!??

Lingalikuwa kosa kama alimlazimisha huyo RAIA amvuushe bure, lakini kama kailipia hiyo huduma mimi sioni tatizo lolote! Na tukumbuke askari au Jeshi wote ni binaadamu tu na wala sio malaika.
 
Ha ha haaa. Uliza ya Gongolamboto walivyotimua na kuwaacha wake na watoto.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…