Jeshi la Polisi lijitathimini na namna ya kukabiliana mambo

Anyisile Obheli

JF-Expert Member
Dec 13, 2009
3,399
320
Katika kumbukumbu zangu

Iliwahi kutokea hii mnamo mwaka 1999 Mkoani Mbeya pale shule za Meta na Sangu zote kwa pamoja wanafunzi waliandamana mpaka kwa Mkuu wa Mkoa wakipinga shule hizo kubadirishana wakuu wa shule Sangu wakitaka Mwl Mwankinga abaki pale pale na Meta pia hawakutaka mkuu wao aondoke

Lakini polisi walikwepo na kuweka mazingira safi ya maandamano wakitulinda wanafunzi na kuhakikisha tunaandamana salama na kusikilizwa

Benjami W Mkapa alikuwa ndiye rais wakati ule nafikiri kwa kiasi kikubwa Polisi walikuwa na weledi mkubwa sana na kazi wakiruhusu akili, busara na maarifa vitumike sana kuliko nguvu

Tujitathimini ipo migogoro haihitaji sana mabavu na miguvu, wakati mwingine tutumie busara kutatua haya mambo katika jamii zetu kuepuka kupanda fitina na chuki baina yetu

Kuwa FFU hakumaanishi kwamba katika kila jambo tu appy heavy power to solve our problem, yaani kwamba eti "yai" tulivunje kwa nyundo
 
Colonial mentality bado yawaongoza polisi , wamesahau zama zimebadilika now polisi kazi yake ni kumlinda raia, kua rafiki kwake pia
 
Tunaambiwa wale wa Bariadi walianza kwa kuwarushia Polisi mawe.
 
Back
Top Bottom