Jeshi La Polisi Lichunguzwe

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,201
219
KUKAMATA MACHANGUDOA

Kamanda wa kanda maalumu ya Dar es salaam alipoingia kwa mara ya kwanza alianza kwa kukamata Wakina dada na wanaume wanaojiuza mitaani , wanawake hawa na wanaume hawa wengine walionyeshwa mpaka katika tv na radio , watu hawakujua kwamba wale wanaoonyeshwa pale ni wale wa bei rahisi na ni rahisi kukamatika wale wasio na pesa au nguvu zozote za ziada wengi wao wanaokotwa sehemu kama za magomeni na barabara ya morogoro , wakina dada hawa wanakamatwa inapofikia wakati wa kupelekwa mahakamani wanaongea na maaskari na kuwapa kitu kidogo kisha askari hao wanawapeleka mahakama Fulani huko kariakoo wanasomewa mashitaka na kutolewa kwa dhamana , kesho yake wanarudi tena mitaani na kuendelea na shuguli zao kama kawaida , wakati mwingine tena hawa hawa wataenda kukamatwa wanakuja kuonyeshwa katika tv wanapelekwa mahakamani wanatoa hongo wako nje .

USALAMA NDANI YA RUMANDE


Mahabusu karibu zote Tanzania zinawekwa luva maalumu za marumaru ukutani na katika sakafu , hii ni jitihada nzuri lazima tulipongeze jeshi la polisi kwa kazi hii , ila baadhi ya mahabusu kama ile ya kituo cha kati central vyumba vingi marumaru zake zimevunjika na zingine zinazendelea kuvunjia hata mtu akishika kuigusa kidogo zinavunjika , hii maana yake sikumoja wahalifu waliowekwa mule ndani wanaweza kutumia ncha za marumaru hizi kujeruhi wengine au wengine hata kujijerui wao wenyewe , lakini mimi bado nashangaa yule kamanda anayezunguka katika vyumba vyote kila siku ya jumapili asubuhi anakagua watu pekee au hata mazingira wanayoishi hao watu ? huu ni mfano hao wa wakandarasi wabovu katika suala la ujenzi .

WAHAMIAJI WAMEKUWA DILI

Ukienda kariakoo na baadhi ya maeneo ya jiji wachina ni wengi sana wengi wamekuja kwa ajili ya shuguli zao haswa biashara na mambo mengine ya kazi wanazojua wao wenyewe , pamoja na hayo kuna baadhi ya watu ambao wanashugulika na kutengeneza mipango feki ya kusafirisha watu hawa pamoja na wengine kuwaleta nchini , wakishafikishwa nchini wanawekwa sehemu wanazojua wao halafu hawa watu huwapa taarifa polisi kwamba kuna huyu na yule anaishi sehemu Fulani wako na hati bandia na wako nchini sivyo kihalali , polisi wanaenda kubeba hawa watu wanawaweka ndani nao polisi wanataka kitu kidogo huu ni mradi mkubwa tu kwa baadhi ya askari na hawa wanaojiita watafutia watu kazi .

KUMBE WANACHAGUA KAZI

Wiki 2 zilizopita banki ya NBC iliibiwa bila kuvunjwa , katika wizi huo hata office ya jirani ambaye alikuwa ni mwanasheria napo kulivunjwa na nyaraka kuibiwa , hii haikutangazwa sana katika vyombo vya habari , wakati huo mimi nilikuwa pale polisi , basi bwana kuna askari alipewa kazi hii ya kuchunguza tukio lile yule askari akasema asipewe yeye kwasababu haina ulaji , NBC si mali ya ummah ? nani akupe hela za kufanya mambo yako ? kwahiyo hakuna mtu kwenda

KAZI KWAKO MWANANCHI KUTOKANA NA MAMBO HAYO HAPO WATU WAAMUE TULIFANYE NINI JESHI LA POLISI , NINI KINAENDELEA KATIKA VIJANA HAWA AMBAO TUNATEGEMEA WAWE MFANO MZURI KWAO WENYEWE NA JAMII ?

KAZI IPO
 
Back
Top Bottom