Jeshi la Polisi lawakamata wahamiaji haramu 81 Bagamoyo Mkoani Pwani

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
Jeshi la Polisi Bagamoyo mkoani Pwani limekamata wahamiaji haramu 81 waliokuwa wakitokea Mombasa nchini Kenya kuelekea Afrika Kusini baada ya kutelekezwa porini katika kijiji cha Kingani Bagamoyo na baadaye kujitokeza pembezoni mwa bahari ya Hindi katika harakati za kutafuta chakula baada ya kushikwa na njaa.

Chanzo: ITV
 
Kwaiyo polisi watawafanyaje? Maana kuwarudisha Kenya ni gharama kwa mtanzania.
 
Eti bwana! Watu hawajajenga makao ila wanajipitia tu unawaita wahamiaji haramu!?Nashindwa kuuelewa huu msemo wa polisi.Wahamiaji haramu wa kweli wapo lakini hawaguswi!
Maana yake hawana vibali vya kuhama nchi, mbona nyie wagumu kuelewa
 
Hao ndiyo wataeleza vizuri kwa nini waliwatupa wenzao sita kwenye mto Ruvu badala ya kuwazika kistaarabu
 
Hao jamaa wako on transit so kuwaita ni wahamiaji haramu sio sawa labda sijui maana ya uhamiaji haramu, their intention ain't settling in tanzania!
 
hao walipaswa kukamatwa maeneo ya mpakani mwa nchi...

wangekuwa alshabab wangeshafanya kitu mbaya kama west gate
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…