Jeshi la Polisi lapekua ofisi ya CHADEMA Makao Makuu!

HUYU ILUNGA KWA KUWA ANATAFUTA KUTOA UHAI WA WAKRISTO - MBELE YAKO WEWE NA VIONGOZI WA JESHI LA POLISI NA SERIKALI AMBAO WOTE NINYI MNAONGOZWA NAYE KIDINI mnasherehekea!...

Basi acha ili gaidi likione cha mtema kuni.
 
Nawe pia Mkuu Bukyanagandi.
nadhani polisi kwa hili wangesubiri kesho ndio wakafanya upekuzi
tusingekuwa na mashaka na kazi yao na tungeamini ushahidi wao ungekuwa mzuri kufahamu ukweli...
kwa walivokurupuka leo sijaelewa mantiki yao ni ipi......
kuna evidence nyingi tu police wana tabia ya kubambikizia watu kesi, who knows wakaenda na kamera iliochukua picha na kuiweka ofisini kwa chadema ili watuaminishe kuwa shughuli yao walifanya chadema?
hapa kuna benefit of doubt nyingi tu.....why today and not tomorrow?


Heshima yako mkuu Lokissa, Taifa letu tusipo kuwa makini tunavyo ji-conduct tutakuja kuhabika kimataifa siku si nyingi zijazo!!
 

Kuna mtazamo mwingine wa hili sakata la video ya Lwakatare, mtazamo ambao nasdhindwa kuunganisha dots.. Naomba msaada

1. Kuna thread moja iliwekwa jana ikionyesha akina Michuzi wakipongezana kutokana na Usalama wa Taifa (TISS) ‘kuleta kitu hiki’ na kwamba ni ‘kete kubwa kwetu’ – bila shaka kete kubwa dhidi ya Chadema. Katika thread hiyo kulizuka tatizo la kutafsiri (yaani kulikuwapo ambiguity) kuhusu maneno (intepretation) ya pongezi hizo kwa TISS ni kwa ajili ya nini hasa – yaani kwa jitihada halali za TISS kuchunguza na hatimaye kupatikana hiyo video; au pongezi zililenga kwa wao TISS ‘kuipika’ hiyo videoa kwa ajili ya kubambikizia CDM?

2. Sasa hata tuchukue hiyo tafsiri ya kwanza – kwamba TISS ndiyo walifanikisha kuchunguza na kupatikana hiyo video ambayo bila shaka itakuwa ni ‘ushahidi’ mkubwa wa kesi dhidi ya Lwakatare na pengine CDM pia, jee hii ndiyo njia sahihi kwa TISS, au tuseme ndiyo utaratibu wao wa kuuweka kwanza ushahidi huu muhimu mtandaoni kabla ya sualakupelekwa mahakamani? Nasema hivi iwapo video hiyo ni kutokana na jitihada zao za halali wenyewe TISS yaani wao ndiyo exclusive owner wa hiyo video kama jinsi akina Michuzi walitaka sis tuamini. Inakuwaje waitumbukize kwanza mtandaoni? Ndivy utaratibu siku hizi?

3. Kwa nini TISS wasingekaa nayo kimya kimya tu halafu kuishtukizia mahakamani baada ya kumkamata Lwakatare? Ushahidi mkuu wa kesi unawekwa bayana kwa jamii kwa njia ya mtandaoni kabla ya kesi kuanza?

4. Lakini pengine TISS hawakuwa mmiliki pekee (exclusive owner) ya video hiyo yaani nao waliipata kutoka kwingine (labda from Mchemba?) lakini hata hivyo haikuwa sahihi kitaaluma za mambo ya upelelezi na mashitaka kuiweka kwanza mitandaoni – kwa lengo gani?

5. Na ndiyo sasa nakuja na tatizo langu kubwa kuhusu sakata zima hili: Yeyote yule (TISS au Mchemba) waliiweka video kwanza mtandaoni ili kupima joto ku-test waters) kuhusu uhalisia wake) na wameona kwamba video hiyo imejikuta inatobolewa matundu mengi tu (punched holes) hadi uhalisia wake kuonekana wa mashaka. Kweli TISS hufanya kazi kwa mtindo huu?

6. Mie nadhani ni Mchemba (aliyewahi kutangaza huko nyuma kwamba anayo video ‘inayoonyesha viongozi wa Chadema wakipanga mauaji’ lakini baadaye akajikuta video ina mapugufu mengi kuhusu alichokitangaza na ndiyo maana badala ya kuipeleka polisi (kama jinsi akina Dr Slaa walivyomtaka kuipeleka), au kuwapa TISS wai-deal nayo -- aliona ni vyema aiweke mtandaoni. Na sababu kubwa kufanya hivi ni kwamba iwapo itaonekana ni video ni bomu (yaani ya kughushi), basi isijulikane kama ni yeye ndiyo aliiweka mtandaoni na hivyo kukwepa lawama. Na ndiyo maana kumetokea ugumu wa kumpeleka Lwakatare mahakamani kwa haraka.


7. Video hiyo haimuunganishi moja kwa moja Lwakatare kuhusu kupigwa kwa Kibanda hivyo bila shaka waliokuwa nayo waliishikilia kwanza (was put on hold) hadi “tukio la Kibanda” litokee ndiyo ikawekwa mtandaoni. Hii bila shaka ilitakiwa jamii iwekwe kwanza kisaikolojia kuhusu yatakayofuata.”

8. Na yaliyofuata sasa tumeyaona – watu walipangwa ku-act nafasi zao kama ilivyotakiwa (according to the laid down script). Hawa wengine ni pamoja na Manyerere -- na hata huyo Ludovick na tukio lake lile la kutekwa ili kujitafutia alibi. Nahisi Ludovick atakuwa shahidi tu wa kujaribu kuakandamiza viongozi wengine wa CDM – ingawa hawatajwi katika video.
Mimi naona mpango mzima uliosukwa umekwenda kombo mahali fulani. Bado tISS wanakosa uweledi wa kufanya operations zao – kuanzia tukio la kuuwawa kwa Gen Amrani Kombe, Chacha Wangwe, tukio la tindikali la Kubenea, kutekwa kwa Ulimboka na pengine hili la kupigwa kwa Kibanda.


Naomba tujadili hili kwa kina.

Mkuu umeweza kuweka thread yenye weledi wa kutosha yote uliyoyauliza ukweli yanataka tafakuri ya nguvu.lnabidi sasa watanzania tuache kufikiri kiushabiki badala yake tuweke maslahi ya taifa mbele.Kweli hii cinema iliwekwa kwa aijli ya majaribio na nadhani imefeli na kama taasisi yetu ya usalama kama itakuwa imehusika basi nathubutu kusema hakuna usalama ktk nchi yetu mambo yanakwenda ndivyo sivyo, ivunjwe iundwe upya kama wadau wanavyojaribu kupendekeza,HAITUFAI KABISA.
Nawasilisha.
 
Makamanda fuatilieni hao mafia wasijebambikiza vitu ili kuhalalisha sinema yao. Mungu na aendelee kuwaumbua mafia hawa na jamii iwatambue na matendeo yao maovu.
 
Walitakiwa siku video imetoka wapekue kila sehemu, kwa SASA hata Kama Ni kweli kuna mipango Fulani basi ushahidi utakuwa umeishapotezwa.



tatizo huelewek, kuna mda unaongea vitu vya maana sana. Kwa hili umenena bt km kauli yako ipo neutral
 
Acha unyampafu weweee! Ilunga ana fuata nini hapa? Tuzungumze kuhusu iligaidi lenye kupanga mikakati ya kuwa sulubu wenzie

mkuu wangu.

sisi tunajadili ufanisi wa jeshi la tanzania katika kuchukuwa hatua inapotokea uvunjwaji wa sheria.

Wewe unalitazama jambo hili kwa mtazamo wako

Tuchoongelea hapa ni kwamba

1. Kamuhanda alisimamia mauwaji ya daudi mwangosi kule nyororo iringa je amechukuliwa hatuagani?

2. Uchochezi wa mkanda wa mauwaji, mwigulu amejitamba sana, je hatuagani zimechukuliwa kuona uwiano wowote katika hili?

3. Shehe Hassan Ilunga Amerikodi na kuto video za uchochezi zaidi ya miezi sita akizunguuka nchi zima polisi ilikuwa wapi?

4. Wezi wa Epa wameruhusiwa kurudisha fedha, hii ni sheria kifungu gani inayoruhusu mwizi kurejesha bila adhabu zaid?

5. Chenge na Rushwa ya Rada hakuna lolote

6. Kinana meri yake kusafirisha meno ya tembo sheria inasemaje? je meri hiyo imetaifishwa?

7. twiga wetu wamepandishwa katika ndege ya jeshi la nchi nyingine ndani ya nchi yetu nani alitoa kibali kuingia ndege hiyo?


8. Ulimboka ameteswa vibaya sana, mwanahalisi ametoa njia na vielelezo vya kumpata mtesaji Rama Ighondu wa ikulu, gazeti limefungiwa.

9. Kunamzee kauwawa mbeya, alikuwa usalama wa taifa huko nyuma, je nani kamuuwa mbona kimya?

10.

11.

12

Wewe unaingia na ushabiki wa mtu mmoja, usiangalie kabila, rangi wala dini ya mtu, tafakali kwa kuchangia kwa kuweka

utaifa kwanza. ukiweka ushabiki hata sikumoja hutaona ukweli wala ubaya wa mtu maana kwako kwanza ushabiki. Utaifa kwanza mengine baadaye. Jeshi la polisi limepwaya sana na limepoteza hadhi yake kwa kufanyakazi likiongozwa na uccm kwa manufaa ya watu wachache waliopo madarakani.
 
Excellent Point!! Na kama walishasema haziwahusu Chadema kama leo wameona zimewahusu ni lazima wawataarifu na waje na kibali cha kukagua na sio wakati wahusika hawapo..kwa jinsi Polisi-CCM walivyo vilaza wanaweza fanya hili[/QUOT
E]
Kwa kuwa habari hii ni tetesi tu, nadhani policcm hawajaenda kufany upuuzi huu kwenye ofisi za CDM.
 
Wakuu naomba kueleweshwa, kwani imeshabitika kweli jamaa wamevamia hiyo ofisi tunajadili tetesi?
 
magamba wajue hakuna marefu yasokuwa na ncha,na nyasi zikizeeka hupisha mpya,na mnyonyaji hatesi akifuruliza muda
 
Libaneni Hilo GAIDI mkimalizana nalo lipelekeni zanzibar FBI wlichukuwe waandoke nalo...Hatutaki UMAFIA hapa
 
kumekucha nini wewe mshamba mwenye tamaa ya tenda za TBS?

Huyu mtu wa kujipendekeza kwa ccm apewe tenda ya TBS alipewa?hivi haoni aibu kuendelea kujipendekeza kwenye mitandao?watanzania wa leo si wajinga wa kuthamini mamluki wa siasa hata kama ni binadamu
 
your wrong my brother.....
ofisi ni ya chadema, mkuu wa ofisi ni aidha dr slaa u mbowe.....
ni sawa na police kupekua nyumba bila wazazi kuwepo kwa kigezo yupo mtoto.
au kupekuwa ofisi ya serikali au binafsi bila boss kuwepo kwa kisingizio mfanyakazi yupo, hiyo haitoshi
ikumbukwe Lwakatare ni mshtakiwa kwa hili walitakiwa wawepo viongozi wa chadema...sheria zipo ndugu na lazima ujue kuzitafsiri sio kukurupuka tu.. still wamechemka...kwa walidhani hivo kama ulivoeleza wataumbuka...

My brother,
Nafikiri hujaielewa post yangu. Mimi nina maana wameenda kupekuwa kwenye ofisi ya Lwakatare ambayo iko kwenye jengo la ofisi ya CHADEMA. Sioni kosa lolote hapa.

Anyway, tukubali kutokubaliana.
 
Back
Top Bottom