Jeshi la Polisi lafanikiwa kuwaua majambazi wanne na kurejesha baadhi ya silaha zilizoporwa

Wameshindwa kuwakamata mpaka wakawauwa?
Au ndicho walichofundishwa ukikamata jambazi mtoe uhai.

Polisi ya viwanda bana!!!
Hawajawakamata na hawajawaua. Kwa kawaida ya polisi tungeshaonyeshwa silala zilizorejeshwa na miili ya majambazi hao. Kana wamesema wamewapata na kuwaua ni kwa sababu hayo ndo maneno yanayopendeza masikioni mwa mkuu.
 
Safi sana jeshi letu la polisi kwa kazi nzuri.
Mwenyezi MUNGU azidi kuwasimamia
Ya kwa kweli wanafanya kazi nzuri ya kulinda wananchi na mali zao. Kilichobaki wawatafute majambazi wawapate na kutupa taarifa inayoeleweka siyo hiziboropaganda za akina ruta!
 
Majambazi sio wajinga kama watu wanavyodhani.
Kwamba walikuwepo tu wanawasubili pilisi waje kupambana?

Ni jambo ambalo haliwezekani hata maramoja.

Kwanza inawezwkana kikosi cha operation kiliwaacha wahusika wa uhalifu huko dar

Na wanao gongwa ni wengine kabisaaa
 
Ya kwa kweli wanafanya kazi nzuri ya kulinda wananchi na mali zao. Kilichobaki wawatafute majambazi wawapate na kutupa taarifa inayoeleweka siyo hiziboropaganda za akina ruta!
Tuwape muda mkuu. Naamini taarifa zikikamilika jeshi letu halitasita kutujulisha
 
Punguza hasiraaa Watanzania wote hatuwezi kwenda ila si Kuna TV na na Magazeti na Mitandao.
sasa una panic nini bro
TV NA MAGAZETI YAMEANDIKA SILAHA ZILIZOPATAINA NA MAJAMBAZI WALIOUAWA WEWE UNASEMA NI UWONGO SASA BORA TWENDE WOTE 53 MIL HAPO MKURANGA AU HUKUELEWA NIMEKASIRISHWA NA NINI HAYO NDIYO YALIKUWA MAJIBU YANGU KWAKE.
 
Hiyo taarifa nina mashaka nayo hasa kutoka kwa Nsato Marijani CP. Ningetamani wauwawe wote lakini taarifa niliyoipata from field ni tofauti haitakiwi kuitoa kwa usalama wa Polisi wetu. Ngoja tuendelee kusikilizia movie..namuomba Mungu abariki waatikane hao madhalimu wapelekwe kwenye haki..
Mi pia nilisikia tofauti ila tusubir tuone
 
Wasalaam wana jamvi.

Kwanza nianze kuwapa pole watanzania wote kwa kuondokewa na askari wetu wapendwa ambao wamekuwa wakifanya kazi kubwa kulinda raia na mali zao.. Pia ni mpe pole Mh Rais, IGP na waziri wa mambo ya ndani kwa msiba huu mzito ulio lipata taifa...

Wana jamvi kupitia BBC swahili leo jioni kamisishana operation na mafunzo kutoka jeshi la polisi amesema kuwa baada ya kutokea tukio la jana wameendelea na operation maalum wakishilikiana na kikosi maalum kutoka vyombo vyote vya usalama toka jana na hadi sasa wamefanikiwa kuwauwa majambazi wanne na kupata silaha nne kati ya zilizo porwa eneo la tukio,wahusika wa tukio la jana na operation hii kali kabisa itendelea mkuranga nzima na kibiti na amewahakikishia wananchi kuwa lazima wahusika washughulikiwe kwa nguvu zote na lazima wapatikane.

Pia ameweka wazi kuwa eneo la mkuranga wamiliki wa pikipiki na boda boda hawataruhusiwa kuendelea kuendesha vyombo hivyo baada ya saa kumi na mbili jioni... kwa hiyo kama wanofanya biashara ya boda boda wataifanya hadi saa 12 jioni...tuu

Pia ameeleza kuwa askari wetu walivamiwa kiasi kwamba ilikuwa ni vigumu sana kujiami na lengo la wahalifu hao ilikuwa ni kuchua silaha hizo na ameweka wazi kuwa tukio hili ni ujambazi na wala si ugaidi na wahusika watashughulikiwa ipasavyo.

Mungu libariki jeshi la polisi.
Mungu ibariki Tanzania..
Kwahiyo kuuwa ndio mwisho wa intelejensia yetu au?

Sent from my Z5 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom