Leak
JF-Expert Member
- Feb 22, 2012
- 52,844
- 43,316
Wasalaam wana jamvi.
Kwanza nianze kuwapa pole watanzania wote kwa kuondokewa na askari wetu wapendwa ambao wamekuwa wakifanya kazi kubwa kulinda raia na mali zao.. Pia ni mpe pole Mh Rais, IGP na waziri wa mambo ya ndani kwa msiba huu mzito ulio lipata taifa...
Wana jamvi kupitia BBC swahili leo jioni kamisishana operation na mafunzo kutoka jeshi la polisi amesema kuwa baada ya kutokea tukio la jana wameendelea na operation maalum wakishilikiana na kikosi maalum kutoka vyombo vyote vya usalama toka jana na hadi sasa wamefanikiwa kuwauwa majambazi wanne na kupata silaha nne kati ya zilizo porwa eneo la tukio,wahusika wa tukio la jana na operation hii kali kabisa itendelea mkuranga nzima na kibiti na amewahakikishia wananchi kuwa lazima wahusika washughulikiwe kwa nguvu zote na lazima wapatikane.
Pia ameweka wazi kuwa eneo la mkuranga wamiliki wa pikipiki na boda boda hawataruhusiwa kuendelea kuendesha vyombo hivyo baada ya saa kumi na mbili jioni... kwa hiyo kama wanofanya biashara ya boda boda wataifanya hadi saa 12 jioni...tuu
Pia ameeleza kuwa askari wetu walivamiwa kiasi kwamba ilikuwa ni vigumu sana kujiami na lengo la wahalifu hao ilikuwa ni kuchua silaha hizo na ameweka wazi kuwa tukio hili ni ujambazi na wala si ugaidi na wahusika watashughulikiwa ipasavyo.
Mungu libariki jeshi la polisi.
Mungu ibariki Tanzania..