Jeshi la Polisi laagizwa kuwashughulikia askari wala rushwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jeshi la Polisi laagizwa kuwashughulikia askari wala rushwa

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by MziziMkavu, Oct 2, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Oct 2, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,608
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Laurance Masha  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Laurance Masha, ameliagiza Jeshi la Polisi kuwachukulia hatua polisi wote watakaobainika kujihusisha na vitendo vya rushwa katika maeneo yao ya kazi.
  Akizungumza katika mahafali ya polisi waliomaliza mafunzo ya Ukaguzi Usaidizi katika Cho cha Polisi cha jijini Dar es Salaam jana, Waziri Masha alisema kuna baadhi ya polisi wanajihusisha na vitendo vya rushwa kiasi cha kulipaka matope jeshi hilo, tabia ambayo ambao alieleza kuwa inatakiwa kukomeshwa kwa nguvu zote.
  Alimwagiza Kaimu wa Mkuu wa Jeshi hilo, Kamishna Glodwig Mtweve, kutowaonea haya watu hao na badala yake wawachukulie hatua ya kinidhamu pindi itakapobainika amehusika na tukio hilo.
  “Rushwa ni kitu ambacho tunakipiga vita, naomba ndugu zangu tusijiingize katika vitendo hivi vya rushwa ili raia waweze kuwa na imani na jeshi letu, naagiza kama kuna watu wa aina hii wachukuliwa hatua za kinidhamu,” alisema.
  Hata hivyo, alisema katika kipindi cha miaka miwili ajali za barabarani zimeongezeka na akawataka polisi wa usalama wa barabarani kuwachukulia hatua kali madereva watakaobainika kupuuza sheria na kanuni.
  Katika maadhimisho hayo, jumla ya wahitimu 454 walimaliza mafunzo hayo yaliyodumu kwa kipindi cha miezi mitano, ambapo wawili walishindwa kumaliza baada ya kuumia wakati wakifanya mazoezi.
  CHANZO: NIPASHE
   
Loading...