Hivi serikali na chama wamekosa wanastratejia? Au ni hujuma kwa serikali na chama chake?
Sidhani kwa wakati huu ambapo kuna wingu zito dhidi ya utendaji wa serikali (taarifa ya CAG na kura ya kutokuwa na imani na WM), utata juu ya hukumu ya Lema, kushindwa kwa CCM huko Arumeru, kushindwa kwa CCM kwenye udiwani muhimu, Kuhama kwa kada muhimu wa UVCCM na wimbi la kuhama kwa wanaCCM, ukweli kwamba wabunge wawili walijeruhiwa siku ya mkesha wa uchaguzi - tena ni uchaguzi wa udiwani. Polisi wanaibuka na kutoa kauli tata kiasi hiki?
Wake up serikali. Mnachezea moto kwenye nyika wakati wa kiangazi. Moto ukilipuka hamtaweza kuuzima. Siyo muda muafaka kwa sasa. Serikali inahitaji kupumua na wala siyo kuendelea kuibua vitu visivyokuwa na msingi na kuacha mambo mazito yanayosumbua nchi.