Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,812
- 11,987
Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Ulinzi ya China imesema, Jeshi la Ukombozi la Watu la China limetoa misaada ya vifaa vya kukabiliana na maambukizi ya virusi vya Corona kwa majeshi ya nchi 20 zikiwemo Ethiopia, Msumbiji, Tunisia, Angola, Misri, Morocco, Tanzania, Jamhuri ya Watu wa Kongo, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Guinea Ikweta, Sierra Leone, Zimbabwe, Zambia, Cameroon, Rwanda, Argentina, Laos, Cambodia, Saudi Arabia na Bengal.
Taarifa hiyo inasema, binadamu ni jumuiya yenye hatma ya pamoja, na mshikamano na ushirikiano ni silaha yenye nguvu zaidi ya kupambana na virusi vya Corona.
Jeshi la China litaendelea kuimarisha ushirikiano wa kimataifa ili kulinda usalama wa afya duniani.