Ushindi Daima
Member
- May 4, 2013
- 92
- 27
Salaam wana jamvi!
Naandika uzi huu wa kitafiti kama sehemu ya JAMII TALKS, nikiwa na furaha ya ushindi wa timu yangu Liverpool kutinga fainal ya CL kwa kishindo dhidi ya Barcelona.
Nirudi kwenye mada, last week nimetimiza miezi 4 toka nihamie Iringa kikazi nikiishi eneo la Mkimbizi, nimehamia Iringa nikitokea Mkoa wa Arusha.
Miezi 2 baada ya uenyeji nilianza kufuatilia siasa za Iringa Mjini na siku ya Jumamosi nilibahatika kwa mara ya kwanza kufuatilia mkutano wa Mbunge wa hapa Mheshimiwa Peter Msigwa uliofanyika kwenye uwanja wa Mwembetogwa.
Mkutano wa mbunge Msigwa ulikuwa na watu wengi na ulikaa kisiasa zaidi ingawa huyu Mchungaji sio wa kupuuzwa na kubezwa na CCM kama utafiti wangu unavyoonesha.
Kinywa cha Msigwa mina maneno ya kuudhi na kukera ambayo kwa wafuasi wake bado yanawapa morali na hamasa.
Jimbo la Iringa Mjini ni dogo lenye Kata 18 na Tarafa 1 pekee na limezungukwa na majimbo Kalenga,Kilolo na Isimani ambayo yote yapo CCM kwa Wabunge na Halmashauri.
Kwenye utafiti wangu ndipo nikakutane na jina la JESCA MSAMBATAVANGU almaafuru Madame Jesca.
Nikataka nimfahamu ni nani ndipo nikaanza kumfuatilia kupita maeneo mbalimbali ya wenye kunywa bia hadi ulanzi, wenye kula Mkate hadi Kande, wenye kukaa Uzunguni,Uhindini hadi Uswahilini, wenye kuangalia mpira hotelin hadi vibandaumiza.
Nikaona nafasi ya huyu Madame Jesca kama ndiye NYOKA WA SHABA kwa CCM hapa jimbo la Iringa Mjini.
Nimeambiwa huyu Mama amewahi kuwa Diwani wa kuchaguliwa Kata ya MIYOMBONI KITANZINI ambapo ndio Kata ya mjini aliingia mwaka 2012 kwenye uchaguzi mdogo na kuhudumu hadi mwaka 2015 alipochukua fomu ya kuomba ridhaa ya wana CCM kuwa mgombea Ubunge lakini hakufanikiwa.
Mwaka huo 2012 akachaguliwa kuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa na mwaka 2017 mwezi Machi alivuliwa uanachama wake na Kikao cha NEC kilichoketi Dodoma.
Madam Jesca alipata bahati ya kuwa mjumbe wa Bunge la Katiba 2014.
Kisiasa nje ya kuvuliwa uanachama wake inasemekana huyu Mama badi alibaki na imani yake ya Chama Cha Mapinduzi ingawa alikuwa hashiriki mikutano ya kisiasa lakini aliisemea pale CCM ilipokosolewa na kudhihakiwa na wapinzani.
Tarehe 18 Disemba,2018 Madam Jesca aliwekwa chini ya uangalizi maalum wa chama chini ya kikao cha NEC kilichoongozwa na JPM baada ya kuandika barua ya kuomba msamaha baada ya kuvuliwa uanachama na wenzake 12 wakiitwa Wasaliti.
Ila kwenye sherehe za miaka 42 ya kuzaliwa kwa CCM mlezi wao Mzee Mizengo Pinda alimtambulisha na kumpandisha mbele kuwasalimia wanachama wa CCM wa Iringa Mjini.
Wanachama walimshangilia sana na kumuomba mzee Pinda aseme kama chama wamemsamehe na kama bado wanamuombea msamaha kwa Mwenyekiti JPM.
Vijana wa Iringa mjini na Kina Mama ambao ndio wapiga kura wengi wanasema Madam Jesca anafikika kwa ukaribu na hujali sana shida za watu wanyonge, hajivuni na kipato chake zaidi ugawana na wahitaji.
Pia wanasema ni mtu wa kujichanganya kwenye shughuli za kijamii pasipo majivuno.
Nimebahatika zaidi kumfahamu Madame Jesca Msambatavangu mwenye umri wa miaka 43, mkulima na mjasiriamali mwenye shule ya msingi iliyopo Ipogolo na sekondari iliyopo Kitwiru zinajulikana kwa jina la STAR INTERNATIONAL SCHOOLS pia ana duka la kubadilishia fedha( Bureau de Change) ambayo ipo jengo la NSSF Iringa Mjini.
Analima ndani na nje ya Iringa kilimo biashara.
Huyu ndiye JESCA MSAMBATAVANGU ambaye CCM wanatakiwa kumfanya Nyoka wa shaba ili awavushe na kukomboa jimbo la Iringa Mjini.
Kwa utafiti wangu sijaona mwingine zaidi yake ingawa wapo wanaosemwa.
Alipata ajali ya kisiasa ila amesimama imara.
Wasalaam,
Dk Julius Nnko
Hospital ya Rufaa Iringa
Mkimbizi.