Jerusalem kwa mujibu wa BBC

Jerusalem kwa mujibu wa BBC

Slim5

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2014
Posts
28,374
Reaction score
38,248
Mji wa Jerusalem

Kumekuwa na mzozo wa muda mrefu kuhusu udhibiti wa mji wa Jerusalem kati ya Waisraeli na Wapalestina.
Mji huo kwa sasa huwa umegawanywa mara mbili, Jerusalem Mashariki na Jerusalem Magharibi.

Jerusalem ya Magharibi hutazamwa na Israel kama mji wake mkuu nayo Jerusalem Mashariki hutazamwa kuwa mji mkuu wa taifa la Wapalestina (litakapoundwa), ingawa eneo hilo bado kwa kiwango kikubwa limetawaliwa na Israel tangu vita vya 1967.

Tangu wakati wa vita hivyo, Israel imejengwa nyumba za walowezi wa Kiyahudi takriban 200,000 ambao huishi Jerusalem Mashariki, hatua iliyoshutumiwa na jamii ya kimataifa. Eneo hilo huishi Wapalestina takriban 370,000.

Israel ilitangaza 1980 Jerusalem yote kuwa mji wake mkuu wa milele, lakini nchi nyingi duniani hazikubali azimio hilo.

Hivyo basi, balozi za nchi za kigeni katika Israel ziko nje ya Jerusalem, katika mji wa Tel Aviv.
Mzozo huo umefufuliwa tena kutokana na hatua ya Rais Donald Trump wa Marekani kutarajiwa kuutambua mji huo kama mji mkuu wa Israel.

Mataifa mengi ya Kiarabu yameshutumu hatua hiyo ya Bw Trump na kusema itazidisha uhasama Mashariki ya Kati.
Lakini ni kwa nini mji huu huzozaniwa hivyo? Mwandishi wa BBC Erica Chernofsky anachambua.

Dini tatu
Mji huu huwa na umuhimu mkubwa kwa dini tatu kuu - Ukristo, Uislamu na Uyahudi. Dini zote tatu humuangazia Abraham anayetajwa kwenye Biblia na Koran kama mmoja wa waanzilishi au mababu wa imani.
Ni mji ambao umedhibitiwa na dini hizo kwa vipindi mbalimbali katika historia.

Kwa Kiebrania, mji wa Jerusalem hufahamika kama Yerushalayim na kwa Kiarabu al-Quds. Kwa Kiswahili, jina lake halisi ni Yerusalemu. Mji huo ni miongoni mwa miji ya kale zaidi ambayo ipo hadi sasa duniani.

Ni mji ambao umetekwa, ukabomolewa na kuharibiwa na kisha kujengwa tena.
Kila sehemu ya ardhi yake ukichimba kwenda chini hufichua enzi fulani katika historia yake.
Ingawa umekuwa chanzo cha ubishi na mzozano kati ya dini mbalimbali, dini zote huungana kwa pamoja kuungama kwamba ni eneo takatifu.

Ndani yake kuna Mji Mkongwe, ambao una njia nyembamba, vichochoro na nyumba za kale. Kuna maeneo manne makuu na kila eneo, majengo huwa tofauti. Kuna eneo la Wakristo, Waislamu, Wayahudi na Waarmenia. Eneo hilo huzungukwa na ukuta mkubwa wa mawe. Hapo, kunapatikana baadhi ya maeneo yanayoaminika kuwa matakatifu zaidi duniani.

Kila eneo kati ya maeneo hayo manne (unaweza kuyaita mitaa) huishi watu wa aina moja. Wakristo wana maeneo mawili, kwa sababu Waarmenia pia ni Wakristo. Eneo lililotengewa Waarmenia, ambalo ndilo ndogo zaidi kati ya hao manne, lina vituo vya kale zaidi vya Waarmenia duniani.
Jamii ya Waarmenia imehifadhi utamaduni wake wa kipekee ndani ya Kanisa la St James na nyumba kubwa ya utawala. Maeneo hayo mawili yamechukua sehemu kubwa ya mtaa huo wa Waarmenia.

Kanisa

Ndani ya mtaa wa Wakristo, kuna Kanisa Kuu la Kaburi na Ufufuo wa Yesu Kristo, ambalo ni muhimu sana kwa Wakristo kote duniani.
Hupatikana katika eneo ambalo lina umuhimu mkubwa katika kisa cha kusulubiwa, kufariki na kufufuka kwa Yesu.

Kwa mujibu wa utamaduni wa Kikristo, Yesu alisulubiwa hapo, katika Golgotha, au mlima wa Calvary. Kaburi lake linapatikana ndani ya kanisa hilo la kaburi na inaaminika kwamba hapo ndipo alipofufuka.
Kanisa takatifu lafunguliwa Israel
Chumba alimozikwa Yesu chafunguliwa tena Israel

Kanisa hilo husimamiwa kwa pamoja na madhehebu mbalimbali ya Kikristo.
Sana huwa ni wahudumu wa kanisa la Kiothodoksi la Ugiriki, watawawa na mapadri wa Francisca kutoka Kanisa Katoliki la Roma na wengine kutoka kanisa la Waarmenia.
Kuna pia wahuudmu kutoka kanisa la Waothodoksi kutoka Ethiopia, Coptic na Syria.

Ni eneo ambalo mamilioni ya mahujaji wa Kikristo husafiri kila mwaka kwenda kuliona kaburi wazi la Yesu na kutafuta ufunuo na kuomba katika eneo hilo.

Msikiti
Mtaa wa Waislamu ndio mkubwa zaidi kati ya maeneo hayo manne na ndani yake kunapatikana madhabahu ya Dome of Rock (Kuba ya Mwamba) na Msikiti wa al-Aqsa kwenye eneo linalofahamika na Waislamu kama Haram al-Sharif, au Mahali/Hekalu Patakatifu.
Msikiti huo ndio eneo la tatu kwa utakatifu katika dini ya Kiislamu na husimamiwa na wakfu wa Kiislamu ambao hufahamika kwa Kiarabu kama Waqf.

Waislamu huamini kwamba Mtume Muhammad alisafiri kutoka hapo hadi Mecca usiku na aliomba pamoja na roho za manabii wengine wote. Hatua chache kutoka hapo kunapatikana Dome of the Rock (Kuba ya Mwamba) ambapo kuna jiwe la msingi. Waislamu huamini kwamba ni kutoka hapo ambapo Mtume Muhammad alipaa mbinguni.
Waislamu hutembelea eneo hilo takatifu kila wakati katika mwaka, lakini kila Ijumaa wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhan, mamia ya malelfu ya Waislamu hufika kuomba kwenye msikiti huo.

Ukuta

Katika mtaa wa Wayahudi, kunapatikana Kotel, au Ukuta wa Magharibi ambao ni masalio ya ukuta wa nje uliozunguka lililokuwa Hekalu Takatifu.

Ndani ya hetalu hilo kulikuwa na Patakatifu pa Patakatifu, eneo takatifu zaidi katika dini ya Kiyahudi.
Wayahudi huamini kwamba hapo ndipo kulikuwa na jiwe la msingi ambapo kutoka kwake dunia iliumbwa.

Kadhalika, wanaamini ni hapo ambapo Abraham alikuwa amejiandaa kumtoa kafara mwanawe Isaac. Wayahudi wengi huamini kwamba Dome of the Rock ndipo lilipokuwa eneo takatifu zaidi ndani ya hekalu lililofahamika kama Patakatifu pa Pat

Leo hii, Ukuta wa Magharibi ndilo eneo la karibu zaidi ambalo Wayahudi wanaweza kufanya maombi yao.
Husimamiwa na Rabbi wa Ukuta wa Magharibi na kila mwaka hutembelewa na mamilioni ya mahujaji.

Wayahudi kutoka kila pembe ya dunia hutembelea eneo hilo kuomba na kukumbuka utamaduni wao, hasa nyakati za siku kuu za kidini.
Ukuta huo pia hufahamika kama Ukuta wa Maombolezo.

Chanzo BBC
 
Hivi Suleman alijenga huo msikiti?

Maana tunajua alijenga hekalu

Huo msikiti umejengwa karne za juzi tu

Why waislamu mnalazimisha yerusalemu uwe mji wenu?

Neno israeli lina maana yake kibiblia , ,nyie kwenye koran hamjui hata maana ya Israeli

Mnadanganya watu eti ibrahimu alikuwa muslim

Wakat uislamu umekuja juzi juzi na muhamad ,before hakuna hata chembe ya history kuwa kuliwahi kuwepo na kitu kinaitwa islamu ,
 
,HAYA TUFAHAMISHE SASA HUO MSIKITI ULIJENGWA JUZI NA KINA NANI??
Wewe unasema uislamu umekuja juzi tu
Haya naomba ANDIKO KATIKA KITABU CHAKO UNACHOKIAMINI LINAYOSEMA KUA KRISTO NI DINI
NIPE ANDIKO
Nikizama saana kidini saana saana huu uzi utafungiwa tu,
Huo msikiti wa Al-Aqsaa unaufahamu vizuri historia yake???hebu nenda kwanza ukaoge half ukaanze kuchota maji kisimani
Utaniharibia siku bure tu kuanza kulumbana na matoto
 
Wayahudi na Wakristo wala hawapingani juu ya umuhimu wa Jerusalem kwao. Wakristo wanaelewa kwamba Jerusalem ni ya Isreal. Wakienda kule wanakwenda kwa mantiki ya imani yao wala hawajawahi na hawawezi kung'ang'ania kuwafukuza Wayahudi kule eti sasa ni kwao kwa kuwa kuna chimbuko la imani yao!. Ridiculous!

Hawa waislam, kuna misingi gani ya Imani yao ya uislam katika Jerusalem?

Ndiko alikozaliwa mungu wao mohamed?

Kuna kaburi la mohamed?

Kuna nini cha imani yao katika Jerusalem?

Hawa watu ni wakorofi siku zote:-, hata ukiwapa Israel nzima haiwezi kuwapa amani kwa sababu amani yao huwa ni machafuko.

Waislam muoni haya.Oneni aibu kuwa watu wa kuanzisha machafuko na kusababisha umwagaji damu kila mnakokuwa na hata kwa majirani mnaopakana nao. Shame!
 
Hivi Suleman alijenga huo msikiti?

Maana tunajua alijenga hekalu

Huo msikiti umejengwa karne za juzi tu

Why waislamu mnalazimisha yerusalemu uwe mji wenu?

Neno israeli lina maana yake kibiblia , ,nyie kwenye koran hamjui hata maana ya Israeli

Mnadanganya watu eti ibrahimu alikuwa muslim

Wakat uislamu umekuja juzi juzi na muhamad ,before hakuna hata chembe ya history kuwa kuliwahi kuwepo na kitu kinaitwa islamu ,
Kumbe BBC ni waislamu!
 
Wayahudi au uyahudi wanawawekak wakiristo na waislam kundi moja tu, hawajawahi kumkubali Yesu kama mtume wao kamwe, na wakiristo wa Israel na mashariki ya kati wanaua hili , ndio maana juzi waliandamana na kutoa tamko kwamba Jerusalem ibaki kama City of peace kwa dini zote, tatizo humu watu sio wafuatiliaji wa mambo ..... wakristo wa Israel wanapata shida sawa na wenzao wailam juu ya mayahudi , mimi nilikutana na mkiristo mkimbizi wa kipalestine kule Iraq na ni mkimbizi kwa sababu ya hao hao, ila huku kwetu tunafikiri uyahudi ni ukiristo .... uyahudi ni dini tofauti kabisa na wale conservative wanamchukulia Yesu kama nabii wa uongo, ni uislam tu ndio wanamuamini Yesu katika dini zote zisizo za kikiristo
 
Naam umesema kweli kabisa ila walio wengi miongoni mwa wakristo hawafahamu hili
 
Hivi Suleman alijenga huo msikiti?

Maana tunajua alijenga hekalu

Huo msikiti umejengwa karne za juzi tu

Why waislamu mnalazimisha yerusalemu uwe mji wenu?

Neno israeli lina maana yake kibiblia , ,nyie kwenye koran hamjui hata maana ya Israeli

Mnadanganya watu eti ibrahimu alikuwa muslim

Wakat uislamu umekuja juzi juzi na muhamad ,before hakuna hata chembe ya history kuwa kuliwahi kuwepo na kitu kinaitwa islamu ,

Mkuu huwezi kusoma mavitabu ya ajabu ajabu alafu ukaelewa ukweli mbali na biblia takatifu,hiki ndicho kitabu bora zaidi kuliko vyote duniani,kwani kmeandikwa na watu tofauti tofauti,wenye taaluma tofauti tofauti,waliishi miaka tofauti tofauti lakini wote wameandika mambo yanayo fanana,hakika Mungu wa Israel ni wa ajabu.watu tofauti tofauti katika miaka tofauti tofauti wametabiri juu ya mji wa bwna wamajeshi yaani Yerusalem nahakuna unabii ambao hujatimia soma unabii wa yeremia,Ezekiel, isaya,Daniel, mika,zakaria,injiri na ufunuo wa Yohana wote hawa wametabiri habari za Israel na unabii mwingi kati ya huo umeisha timia na baadhi unakwenda kutia muda sii mrefu.
 
Hivi Suleman alijenga huo msikiti?

Maana tunajua alijenga hekalu

Huo msikiti umejengwa karne za juzi tu

Why waislamu mnalazimisha yerusalemu uwe mji wenu?

Neno israeli lina maana yake kibiblia , ,nyie kwenye koran hamjui hata maana ya Israeli

Mnadanganya watu eti ibrahimu alikuwa muslim

Wakat uislamu umekuja juzi juzi na muhamad ,before hakuna hata chembe ya history kuwa kuliwahi kuwepo na kitu kinaitwa islamu ,
Umeonyesha kiwango chako cha ujinga!…

Kasome uelewe,, dini sio sawa na kula au kupiga shoo kila mtu atajua! jinga
 
,HAYA TUFAHAMISHE SASA HUO MSIKITI ULIJENGWA JUZI NA KINA NANI??
Wewe unasema uislamu umekuja juzi tu
Haya naomba ANDIKO KATIKA KITABU CHAKO UNACHOKIAMINI LINAYOSEMA KUA KRISTO NI DINI
NIPE ANDIKO
Nikizama saana kidini saana saana huu uzi utafungiwa tu,
Huo msikiti wa Al-Aqsaa unaufahamu vizuri historia yake???hebu nenda kwanza ukaoge half ukaanze kuchota maji kisimani
Utaniharibia siku bure tu kuanza kulumbana na matoto

WE MUISLAM KELEEEE NA MWENZAKO MKRISTO ANYAMAZE KIMYAAAA wote nyinyi wa kuja huo mji ni wa wayahudi waislam na wakristo ondokeni hapo acheni ujinga wenu dini dini dini zenu zimewakuta watu wapo pale tokeni zenu..
 
Uhusiano uliopo ni kwamba kabla al kaaba(kibra) iliyopo sasa katika msikiti wa mecca ambapo waislam wanaenda kuhiji na ambapo ni eneo takatifu zaidi kaaba(kibra) ya mwanzo ilikuwa katika msikiti wa al aqsa huko Yerusalem.
hiyo Kibla nini nini? na kwanini ile Yerusalemi badala ya Madina na Macca ambapo ndo kwa Mohamad na kwa Waarabu.
 
WE MUISLAM KELEEEE NA MWENZAKO MKRISTO ANYAMAZE KIMYAAAA wote nyinyi wa kuja huo mji ni wa wayahudi waislam na wakristo ondokeni hapo acheni ujinga wenu dini dini dini zenu zimewakuta watu wapo pale tokeni zenu..

Mkuu kuna mitume waliotumwa kueneza dini ya kiislamu ni WAYAHUDI vilevile muhimu utambue na hilo
Kwa mfano Nabii Suleiman alikuwa myahudi lkn ndie aliewaamrisha viumbe waliokua chini yake kuujenga huo msikiti na nabii suleiman alikuja kabla ya nabii Issa(Yesu)
Na chanzo cha QIBLA ni hapo.kila muislam anaposali lazima aelekee kibla na chanzo chake ndio hapo hicho kibla
Hii ni dunia nzima wanalifahamu hilo
Quraan kareem haijaacha kitu.Yote yapo ndani yake
Zaburi-Alipewa nabii Dawood
Taurat-Alipewa nabii Musa
Injili (Biblia)-Alipewa nabii Issa (Yesu)
Quraan-Alipewa nabii muhammad s,a,w
Hicho kitabu cha mwisho ndio imeviunga vitabu vyote hivyo vya mwanzo.imetaja kila kitu
I hope utakua umenielewa mkuu
 
Uhusiano uliopo ni kwamba kabla al kaaba(kibra) iliyopo sasa katika msikiti wa mecca ambapo waislam wanaenda kuhiji na ambapo ni eneo takatifu zaidi kaaba(kibra) ya mwanzo ilikuwa katika msikiti wa al aqsa huko Yerusalem.

Hiyo kibra ya mwanzo ilijengwa na nani huko Jerusalem, ilikuwa mwaka gani, na huyo mjenzi kwa nini alikwenda kuijenga kule? Kama kibra ilihamishiwa mecca, nini kilisalia Jerusalem ambacho hakiwezi kuhamishwa?
 
Waislamu achen kung'ang'ania hekalu na mji wa watu

Hivi Suleman alijenga huo msikiti?

Maana tunajua alijenga hekalu

Huo msikiti umejengwa karne za juzi tu

Why waislamu mnalazimisha yerusalemu uwe mji wenu?

Neno israeli lina maana yake kibiblia , ,nyie kwenye koran hamjui hata maana ya Israeli ,mnaropoka tu

Mnadanganya watu eti ibrahimu alikuwa muslim

Wakat uislamu umekuja juzi juzi na muhamad ,before hakuna hata chembe ya history kuwa kuliwahi kuwepo na kitu kinaitwa islamu ,

Nyie nenden macca na madin huko mkacheze na majini na kurusha mawe
Wanashangaza sana kwakweli.
 
Mkuu kuna mitume waliotumwa kueneza dini ya kiislamu ni WAYAHUDI vilevile muhimu utambue na hilo
Kwa mfano Nabii Suleiman alikuwa myahudi lkn ndie aliewaamrisha viumbe waliokua chini yake kuujenga huo msikiti
Na chanzo cha QIBLA ni hapo.kila muislam anaposali lazima aelekee kibla na chanzo chake ndio hapo hicho kibla
Hii ni dunia nzima wanalifahamu hilo
nakuelewa ndugu sana sana na vizuri umenijulisha kuwa hao mitume ni wayahudi ndiyo maana nikasema hivyo ila lazima tujue mji sio dini ila dini ipo katika mji kabla ya ibrahim baba wa mababa wa dini zote uyahudi,uislam na ukristo palikuwa na watu hapo sasa tukitetea amani kwa kidini atuwezi kuipata coz imani ni roho huwezi tenga mwili na roho,hivyo udini ukishika kasi hapo tusitegemee amani ikapatikana pia kumbuka na myahudi atakwambia sulemani ni myahudi na daudi baba yake ndiyo aliwajengea huo mji na mkristo atakwmbia daudi baba yake sulemani ndiyo chanzo cha Yesu ndiyo maana anaitwa mwana wa daudi na jeruselem ndiyo mji wake unafikiri amani itapatikana hapo,nafikiri sisi tuliodandia wakristo na waislamu tukubali tu wayahudi ndiyo wenye haki asilimia mia.kwani dini zingine zimekuja na kuwakuta wayahudi.
 
Back
Top Bottom