Kumepambazuka ndio anataka kudanganya watu...wakati wa umeya wake Ilala haijawahi huwa chafu kama sasa. Alijimilikisha makampuni ya takataka tukawa hatuwezi kuyahoji, Barabara mashimo matupu, aliingia taa za barabarani zinawaka, leo zote zimekia miti tu isiyo matunda.
Ameshindwa kubuni njia bora za kuondoa adha ya foleni, amekuwa akianzisha miradi ya kupata fedha ya kuweka matufali kwenye pembe za barabara zenye mashimo... yaani barabara yenyewe haipo lakini pembeni anaweka matofali ..wizi mtupu. Ameanzisha na watu wa fire ati kila nyumba ilipe fire, badala ya kutuambia tununue vifaa vya moto yeye tutoe tozo
Hilo soko atalojenga ni pia ubadhirifu na wizi ameuza kiwanja hicho ili waendedhe matajiri ...yatakuwa kama soko la machinga Ilala mpaka leo lipo tupu.. wewe unafikiri muuza nyanya ataweza kulipa kodi kwa investor anayetaka kurejesha fedha zake? Wamepeana tenda za parking, fedha hazijulikani zinafanya kazi gani.
Fedha za billbords na mabango ni mabilioni kwa mabilioni, hazijulikani zinakwenda wapi. Huyu jamaa kumrejesha tena kwenye uongozi basi tutakuwa wendawazimu... nadhani ndio maana kaenda Ukonga huko... labda watu watamchagua kwa u handsome