Jerry Silaa: Nimetoa siku saba ghorofa liwe limebomolewa

Jerry Silaa: Nimetoa siku saba ghorofa liwe limebomolewa

Ng'wamapalala

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2011
Posts
6,811
Reaction score
6,506
Dar es Salaam. Halmashauri ya Manispaa ya Ilala imetoa notisi ya siku saba kwa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) pamoja na mmiliki wa jengo la ghorofa 16 lililopo Mtaa wa Indira Gandhi mkabala na Msikiti wa Shia Ithnasheri kulibomoa ndani ya kipindi hicho.

Ghorofa hilo linalomikiwa na mfanyabiashara maarufu nchini Ally Raza linabomolewa baada ya kuanguka kwa jengo pacha la aina hiyo Machi 29 mwaka huu na kusababisha vifo vya watu 36, kujeruhi 18 na uharibifu wa mali.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini jana, Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa alisema kuwa, notisi hiyo imeanza Mei 27 hadi Juni 3 mwaka huu.

“Tayari tumewakabidhi NHC na Ally Raza mmiliki wa jengo la ghorofa 16 notisi ya siku saba ya kumtaka kubomoa jengo hilo ndani ya siku saba na asipotekeleza hatua zaidi za kisheria zitachukuliwa,” alisema Silaa.

‘‘Kwa mujibu wa sheria ya mipango miji, mmiliki halali wa kiwanja hicho ni NHC, na wao ndiyo waliomuuzia Raza eneo hilo ili aweze kujenga ghorofa’’ alisema.

Kwa mujibu wa Silaa, kutokana na ramani iliyotolewa na mipango miji, maeneo yote ya Kisutu yanatakiwa kujengwa ghorofa 10 na si vinginevyo, lakini cha kushangaza, Mhandisi kutoka Bodi ya Wahandisi, msanifu majengo na makandarasi wameweza kusimamia ujenzi wa ghorofa 16 kinyume na taratibu.

Alisema, kitendo cha Manispaa hiyo kuingia kwenye lawama ambazo pia zinawahusu NHC, wahandisi, wasanifu majengo na wakandarasi kwa kuidhinisha ujenzi wa ghorofa 16 wakati eneo hilo linaruhusiwa kujengwa ghorofa 10 ni sawa na kutowatendea haki.Alisema kutokana na hali hiyo kila mmoja anapaswa kuwajibika kulingana na nafasi yake ili siku nyingine waweze kufuata sheria na taratibu zilizopo wakati wa kuidhinisha majengo nchini.

Alisema, kutokana na hali hiyo wameiomba tume iliyoundwa kwa ajili ya kuchunguza ghorofa hiyo kutoa ripoti mapema ili waweze kuijadili na kutoa mapendekezo yao.

Hali hiyo inatokewa wakati Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Profesa Anna Tibaijuka juzi wakati wa kuwasilisha makadirio ya bajeti ya Wizara yake, alizitaka Manispaa ya Ilala, NHC na mmiliki wa ghorofa hilo kulibomoa ghorofa hilo.

Kwa hisani ya Mwananchi.
 
Who is the boss?.

How many 'Formal statement', Orders and Ultimatum are needed to take the GHOST SHIT out of place.

I can't see the sense in issuing order while awaiting 'report' from recycled decision.

From The Minister for Human Settlements, Housing and Urban Affairs to
Parliament committe for Lands, Natural Resources and Environments and now, ILALA Municipal Mayor, Jerry Silaa.

Rushwa inapokomaa katika jamii au taasisi huwa inakuwa na tabia ya kutokuona aibu kwa lolote ile lililoko mbele yake.

Mojawapo ya mbolea ya Rushwa ni jamii au viongozi wake kuwa legelege katika maamuzi na utendaji.

Uzuri au ubaya wa rushwa haionekani kwa macho bali huwa inajidhihirisha katika matendo.

Matendo ya viongozi wetu katika swala hili yanadhihirisha kuwepo kwa rushwa ambayo imefikia kiwango cha kutokuona aibu.

This is embarrassing kwa Anna Tibaijuka Mb.
 
mgamba hakuna kitu zaidi ya kujikosha; je wahanga wamepata fidia kiasi gani
 
i don't expect anything new under this(upepo utapita)goverment.
 
Hapa nnachookiona ni mmiliki kulipwa Mabilioni ya Shilingi tu !

•Anakibali halali cha ujenzi
•Ubora wa jengo haupimwi kwa macho
•Waliompatia kibali cha kujenga zaidi wapo chini ya Mamlaka ya Mama Anna Tibaijuka, Amewasaka ?
•Badala ya kutoa matamko angesaidiana na mamlaka husika kusafisha Uozo wa kutoa vibali " blindly " katika Bodi yake ya Ukandarasi
 
Hii nchi bwana, huyu jamaa alipewa siku nne na kamati ya bunge, sasa miezi mitatu imepita. Atamsikiliza meya kweki!
 
Hizi ni kauli za kisiasa ili naye asikike alisema.
 
Naona kama ndugu meya anakurupuka.

Ndugu Meya kuwa makini na siasa hizi kaa chini na wataalam wa majengo na muangalie pia uwezekanao wa kisheria kwanza msije kukurupuka kama lile ghorofa la masaki lilivyo wa cost hadi sasa mjengo bado upo.
 
Even if he (the owner- Mr Raza) is going to be paid a 'huge' compensation, it's better than sitting on the danger hill! Wabomoe tu hilo jengo, jengo dogo sana lile kwa upana na ni refu sana!. Maamuzi magumu muhimu!
 
"gasho" mzee wa kujichubua,nae ana kauli? Kuishi kwingi kuona mengi
 
wanatishana tu hao, hakuna lolote hapo, ebu tusubiri toune siku 7 si nyingi....
 
Dar es Salaam. Halmashauri ya Manispaa ya Ilala imetoa notisi ya siku saba kwa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) pamoja na mmiliki wa jengo la ghorofa 16 lililopo Mtaa wa Indira Gandhi mkabala na Msikiti wa Shia Ithnasheri kulibomoa ndani ya kipindi hicho.

Ghorofa hilo linalomikiwa na mfanyabiashara maarufu nchini Ally Raza linabomolewa baada ya kuanguka kwa jengo pacha la aina hiyo Machi 29 mwaka huu na kusababisha vifo vya watu 36, kujeruhi 18 na uharibifu wa mali.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini jana, Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa alisema kuwa, notisi hiyo imeanza Mei 27 hadi Juni 3 mwaka huu.

“Tayari tumewakabidhi NHC na Ally Raza mmiliki wa jengo la ghorofa 16 notisi ya siku saba ya kumtaka kubomoa jengo hilo ndani ya siku saba na asipotekeleza hatua zaidi za kisheria zitachukuliwa,” alisema Silaa.

‘‘Kwa mujibu wa sheria ya mipango miji, mmiliki halali wa kiwanja hicho ni NHC, na wao ndiyo waliomuuzia Raza eneo hilo ili aweze kujenga ghorofa’’ alisema.

Kwa mujibu wa Silaa, kutokana na ramani iliyotolewa na mipango miji, maeneo yote ya Kisutu yanatakiwa kujengwa ghorofa 10 na si vinginevyo, lakini cha kushangaza, Mhandisi kutoka Bodi ya Wahandisi, msanifu majengo na makandarasi wameweza kusimamia ujenzi wa ghorofa 16 kinyume na taratibu.

Alisema, kitendo cha Manispaa hiyo kuingia kwenye lawama ambazo pia zinawahusu NHC, wahandisi, wasanifu majengo na wakandarasi kwa kuidhinisha ujenzi wa ghorofa 16 wakati eneo hilo linaruhusiwa kujengwa ghorofa 10 ni sawa na kutowatendea haki.Alisema kutokana na hali hiyo kila mmoja anapaswa kuwajibika kulingana na nafasi yake ili siku nyingine waweze kufuata sheria na taratibu zilizopo wakati wa kuidhinisha majengo nchini.

Alisema, kutokana na hali hiyo wameiomba tume iliyoundwa kwa ajili ya kuchunguza ghorofa hiyo kutoa ripoti mapema ili waweze kuijadili na kutoa mapendekezo yao.

Hali hiyo inatokewa wakati Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Profesa Anna Tibaijuka juzi wakati wa kuwasilisha makadirio ya bajeti ya Wizara yake, alizitaka Manispaa ya Ilala, NHC na mmiliki wa ghorofa hilo kulibomoa ghorofa hilo.

Kwa hisani ya Mwananchi.

jery jery jery siku 7 siyo miaka 7.kijana mwenzetu angalia,nape alitoa siku 90 mafisadi kuwafukuza ccm,haa mbaka leo,mkivunja jengo hilo mimi nakuja kuchukua kadi ya ccm.
 
Angalia tu mheshimiwa meya isije ikawa 7+7=14 mara 14+14=28 mara kimyaa
 
Sasa inakuwa kama mikwara ya MNYAMA MLINZI WA NYUMBANI KOKO!! Maana huyu ni kiongozi wa PILI kutamka rasmi juu ya kutakiwa kuvunjwa kwa hili jengo!!! Mimi niliamini Mh wa kwanza NI BIGGER kuliko huyu wa Pili na hivyo tungetarajia ORDER yake itekelezwe MARA MOJA!!!!! Sasa hadi inarudiwa (kama mwangwi) na Meya............Ni aibu kwa serikali kuwa KIBOGOYO (meno-less) kiasi hiki!!!
 
Back
Top Bottom