Jerry Silaa amesahaulika ama ni upepo?

Ukonga tulimkataa tukamchagua Mwita Waitara.

Ukonga hatupendi ujinga sisi
 
Jerry kasoma Electronics udsm, kamaliza 2005. Dogo hawezi kwenda sawa na Magu maana ni mpigaji sana, na upigaji kaanzia chuo wakat akiwa waziri daruso. Anaijua hela.He is very bright,very smart though.

Pia ikumbukwe wamewahi kukwaruzana na mkuu kuhusu mabango ya barabarani na dogo akapiga kibesi akichallenge uamuzi wake.

Kuna lawama zingine mnampa presdaa mnamuonea tu. Ndo maana kazi kama ya urais inahitaji moyo sana, unaowahangaikia wanakupiga majungu na lawama bila sababu.
 
Jerry nilimsikia wakati anahojiwa na chombo kimoja cha habri, kijana anahekima na busara... anaweza kuongea na lika lote katika jamii!!!

ni wachache watamlinganisha Jerry na Makonda.... Makonda acha abaki bavicha, Jerry ni wa kuwekwa kundi moja na kina Mwigulu, Bashe na kingwangala... ana reasoning ya kutosha kutatua matatizo katika jamii. Hasa Dar es salaam kwa vile alikuwa meya wakati uliopita [HASHTAG]#TunajengaNchiMoja[/HASHTAG]
 
Acheni mambo ya kinafiki ya kizamani yaliyopelekea chama chenu CCM kupoteza ushawishi. Sio lazima Jerry apewe nafasi na mkuu. Mwambie atumie elimu yake kujiajiri na kuajiri watu, alishapewa nafasi akiwa mdogo alitakiwa sasa yeye awe na mtaji wa fedha na network ya watu prominent atumie resource hizo kujiajiri na kuajiri vijana ambao wametoka kuhitimu chuo na hawajapata fursa kama zake.
 
Mtoto wa Marehemu Captain Silaa aliyefariki dunia akiwa na lulu ya Kitanzania Mh Deo Filikunjombe (RIP),
Mara chache napitaga pale kwenywe bar yao maeneo ya Lawate wilayani Siha kujipatia moja baridi,moja moto.

Dogo anajitahidi sana sema tu CHADEMA walimzidi nguvu. Ajipange upya 2020 ajitwike tena mzigoni.
 
huyo kijana abaki hukohuko mitini. alipata laana baada ya kuonyesha hadharani dharau kwa fikra na itikadi ya baba wa taifa mwalimu nyerere. baada ya kupigapiga dili akawa tajiri akaona ajipendekeze kwa mabwanyenye na kudharau watu maskini huku anapenda uongozi.
 
Sisiyemu hakuna msafi
 
Ana MKIA kwanza au hana😵😵
Nilidhani angesema ana Master's degree au PhD. Kumbe post graduate diploma ya practical legal training pale Law School. Huyu si msomi wa kupewa attention. Ndo maana anadai attention. Kuna gapes bado kitaaluma. Kuna watu tuna post graduate diploma,Master's degree mbili, PhD on progress, tena zote ktk fani ya sheria,lakini hatuna kazi. Who is he?
 
Akiwa Meyaaaa alimjibu ovyooo waiziri dhamana wa madaraja ati haongei na mbwa anaongea na mwenye mbwaaaa
Wacha aisome namba
Busara na hekima ni kitu kizuri sana katika maisha yetu ya kila siku
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…