Jerry Muro usipokee Tuzo ya Mwandishi Bora 2009

Kamura

JF-Expert Member
Apr 26, 2011
506
52
Ninamshauri Jerry Muro asipokee tuzo ya Mwandishi Bora wa Mwaka 2009 aliyopokwa na Baraza la Habari Tanzania (MCT) kwa sababu walimhukumu kabla ya hukumu ya Mahakama jambo ambalo ni udhalilishaji wa hali ya juu.
 
tunamsubiri aje na riporti yake kuhusu ufisadi bagamoyo,halmashauri zingine kama kilosa,tanroads,air tanzania nk.Kisheria anatakiwa kurudi kazini na kulipwa mshahara wake wote tangu aliposhtakiwa akiwa TBC lau tido mhando atampeleka aljazeera.
 
Oh, mshahara! Hivi alikua anapewa japo nusu au ndo ilikua 'kahukumiwa' kimoja?
 
dah but the guy amekiri kuwasamehe wote mbele za mwenyezi Mungu,nadhani apokee tu..na aendelee kuwaombea msamaha kwa mwenyezi Mungu maana malipo ni apa apa duniani.
 
Apokee, nyie vipi, mtu akatae mihela kibao kisa kazira au ndio nini, tuzo sio cheti tuu cha sifa, kinakwenda na mihela kibao. Anahitaji hela kwa ajili yake na familia, kumbuka alivyokopa hela ya kukombolea gari, ilimsumbua kurejesha kama nini.
 
Ninamshauri Jerry Muro asipokee tuzo ya Mwandishi Bora wa Mwaka 2009 aliyopokwa na Baraza la Habari Tanzania (MCT) kwa sababu walimhukumu kabla ya hukumu ya Mahakama jambo ambalo ni udhalilishaji wa hali ya juu.
]#

hawakumhukumu,Muro alikuwa mtuhumiwa, sasa imethibitika kuwa tuhuma hazikuwa za kweli. MCT hawana kosa. na muro akikataa atakuwa na matatizo yake, hakushitakiwa na MCT. lakini kutuhumiwa kwake, ilikuwa ni kasoro ktk maadili ya uandishi wa habari, sasa angepewaje wakati mwenendo wake kwa wakati ule ulikuwa wa mashaka?
 
Back
Top Bottom