Kama alifanya yeye kweli ulitaka aseme alifanya na nani? Acha wivu husio na mashiko. Hoja yako ingekuwa na mshiko kama ungeonesha wapi alisema nilifanya wakati walifanya wengi, otherwise ni majungu na siasa za maji taka!
Siku akiiba yeye na akisema sisi tuliiba utakubali??????? kama amefanya yeye ni haki yake kusema mimi. Hawezi kusema sisi wakati ni yeye kwakuwa hata siku atakapoiba atakuwa ni mimi na sio sisi.
hata usemeje, umimi ni udhaifu mkubwa sana. A Y A T O L L A H Zitto ana ubinafsi, majivuno, na kiburi. Ndio maana anaona kila kitu ni yeye tu!!!siku nyingine utakuja na "kwa nini zito anaenda chooni?", au "kwa nini zito amenilia vyangu?".
Mimi ndio Mbunge pekee kijani niliyeiangusha Serikali mara 4, mimi ndiye Mbunge pekee niliyeweza kuwasilisha hoja binafsi zikaitikisa Serikali, mimi ndio mbunge pekee niliyefukuzwa na kupora chama cha watu, nikabadili katiba, nikajipa Cheo ninachotaka ndani ya siku 7.
Thibitisha mkuu!!
Sifa mojawapo ya kiongozi mbinafsi ni hiyo, matokeo chanya ya team hupenda kuona ni yeye ndio aliyasababisha; angalia kwa mfano Jerry Muro tokea ameondoka ITV bado kile kipindi cha report maalumu kinaendelea ingawa ndicho kilicho mpa umaarufu! Sina hakika kama Jerry Muro ameisha wahi kua kiongozi sehemu but with his age, siku 1 atakua so hili na liwe darasa kwake!
Jerry amesema anataka ubunge na alikuwa anasema sifa zake ambazo
hakuna anaeweza kuzi verify
mfano ni lini alitangazwa kuwa ni 'mwanahabari wa mfano'?
alitangazwa na nani?
ni kweli ni mwanahabari mchapakazi ..lakini titles na masifa angeacha wengine waseme
na wala hizo title na masifa hazim halalishi kuwa mbunge
Zitto the same..ni kweli alisababisha baraza la mawaziri livunjwe but hakusaidiwa?
hizo sign 70 zote hazina maana kwake?
angepungua nini kama angesema 'tulisababisha baraza la mawaziri kuvunjwa'?
Malkia Elizabeth anaposema 'we' unafikiri kuna malkia wangapi UK?
lugha ya uongozi ni sisi na we
Jana niliona mahojiano kidogo ya Jerry Muro kwenye kipindi cha MKASI EATV ambacho kikubwa nilichokiona kwa Jerry Muro ni 'entitlement feelings' alizo nazo
Ingawa kiukweli anaonekana ni mzalendo na anaipenda nchi yake na pengine anastahili
kupewa nafasi zaidi lakini kila anapofungua mdomo utamsikia akisema 'mimi nilifanya hivi' 'mimi nilifanya vile'.
Kuna kipindi alisema 'mimi nilikuwa mwanahabari wa mfano Tanzania' nikabaki najiuliza hiyo status alipewa na nani? ni lini alitangazwa wa mfano?
Nafikiri tatizo la Jerry Muro ni hilo....'kutwa anasema 'mimi' 'mimi'
Siku ile Zitto anatangaza kujiunga na ACT-Wazalendo kutwa alikuwa anasema 'mimi nilisababisha baraza la mawaziri livunjwe' 'mimi nilisababisha hiki na kile.
Ingawa yote aliyoyasema naamini yana kitu chenye ukweli but kumsikia kiongozi kutwa akisema 'mimi lilifanya hivi' 'mimi nilifanya vile' it is so irritating...
Lugha ya uongozi ni 'we' ....'sisi'
Naamini humu kuna washauri wengi wa Zitto na Jerry Muro. Waambieni tu kama wanataka kufanikiwa waache sasa hiyo lugha ya 'mimi nilifanya hivi' na waanze leo kusema 'sisi' na kutumia 'we' badala ya 'i' kwenye matamshi yao.
Ni kitu kidogo sana lakini kikuubwa sana.