Jerry Muro na Zitto Kabwe, Something familiar

Jerry Muro na Zitto Kabwe, Something familiar

The Boss

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2009
Posts
49,320
Reaction score
117,613
Jana niliona mahojiano kidogo ya Jerry Muro kwenye kipindi cha MKASI EATV ambacho kikubwa nilichokiona kwa Jerry Muro ni 'entitlement feelings' alizo nazo

Ingawa kiukweli anaonekana ni mzalendo na anaipenda nchi yake na pengine anastahili
kupewa nafasi zaidi lakini kila anapofungua mdomo utamsikia akisema 'mimi nilifanya hivi' 'mimi nilifanya vile'.

Kuna kipindi alisema 'mimi nilikuwa mwanahabari wa mfano Tanzania' nikabaki najiuliza hiyo status alipewa na nani? ni lini alitangazwa wa mfano?

Nafikiri tatizo la Jerry Muro ni hilo....'kutwa anasema 'mimi' 'mimi'

Siku ile Zitto anatangaza kujiunga na ACT-Wazalendo kutwa alikuwa anasema 'mimi nilisababisha baraza la mawaziri livunjwe' 'mimi nilisababisha hiki na kile.

Ingawa yote aliyoyasema naamini yana kitu chenye ukweli but kumsikia kiongozi kutwa akisema 'mimi lilifanya hivi' 'mimi nilifanya vile' it is so irritating...

Lugha ya uongozi ni 'we' ....'sisi'

Naamini humu kuna washauri wengi wa Zitto na Jerry Muro. Waambieni tu kama wanataka kufanikiwa waache sasa hiyo lugha ya 'mimi nilifanya hivi' na waanze leo kusema 'sisi' na kutumia 'we' badala ya 'i' kwenye matamshi yao.

Ni kitu kidogo sana lakini kikuubwa sana.
 
Kiongozi mwenye nia njema utamjua tu. Hata Nyerere ktk hotuba nyingi huwezi kumsikia akisema kwa mfano "sikuwa na mchezo na rushwa " bali atasema "hatukuwa na mchezo na rushwa "
Kuna watu wanapenda kuona wakionwa "wao" tu hata wakizungumza muda wote neno kuu ni "mimi "
 
Nadhani ni wivu tu, lkn kiukweli ukiona mtu anasema mimi nilifanya hili kimsingi analo, na ukiona mtu yuko kimya fahamu kwamba hana jema la kusema ndio maana anafanya hila kukemea wengine wasiseme mazuri yao, ndio maana hata nyerere alikuwa akitolea mfano mambo kadhaa yaliyofanywa na serikali yake.
 
Hata mi nilimsikiliza mwanzo mwisho yaani hawana tofauti kwakweli wote ni wabinafsi,wangemuuliza Lyatonga mrema umimi uliopitiliza ulikomfikisha sasa.wangepata la kujifunza.
 
mambo ya kutumia "Sisi" wakati ulikuwa peke yako ni lugha za kisiasa zenye uongo mkubwa ndani yake

Baada yakuwa maarufu kule kwenye jukwaa la Mapenzi sasa umeona uje huku kutafuta umaarufu kupitia Zitto!!!q He kweli zitto kiboko yao,acha chadema wahahe nchi nzima kusafisha hali ya hewa lol!!!!!!!!Mpaka ww mwana MMU unakuja siasan!!!!!!

Nadhani ni wivu tu, lkn kiukweli ukiona mtu anasema mimi nilifanya hili kimsingi analo, na ukiona mtu yuko kimya fahamu kwamba hana jema la kusema ndio maana anafanya hila kukemea wengine wasiseme mazuri yao, ndio maana hata nyerere alikuwa akitolea mfano mambo kadhaa yaliyofanywa na serikali yake.

kama hata hili lililoandikwa kwa lugha rahisi hamjaelewa, basi tena
 
Sasa kama alikuwa anahojiwa JERRY yeye kam yeye sasa atazungumziaje nafsi za watu wengine???ni kukosa kujiamini na atakuwa mnafiki akisema neno"sisi"wakati ni yeye peke yake anazungumza.

Kuhusu Zitto nahisi unataka uzi wako uwe mrefu tu maana sijaona mantiki ya wewe kumuingiza zitto kwa mada ya jerry
 
Naona kumbe watu wengi wanaliona hili. Zitto na umimi wake tuliugundua zamani tu... enzi zile alivyokuwa chuo. Na huyo Muro itapendeza akijiunga na ACT!?
 
mambo ya kutumia "Sisi" wakati ulikuwa peke yako ni lugha za kisiasa zenye uongo mkubwa ndani yake

Kutenda peke yako kwa ni msalani kujisaidia? Hakuna alifanyalo mwanasiasa akiwa pekee bila kushirikiana na wenzie. Hata kama ni wazo lazima lipate uungwaji Mkono was wenzie
 
Sasa kama alikuwa anahojiwa JERRY yeye kam yeye sasa atazungumziaje nafsi za watu wengine???ni kukosa kujiamini na atakuwa mnafiki akisema neno"sisi"wakati ni yeye peke yake anazungumza.

Kuhusu Zitto nahisi unataka uzi wako uwe mrefu tu maana sijaona mantiki ya wewe kumuingiza zitto kwa mada ya jerry

Jerry amesema anataka ubunge na alikuwa anasema sifa zake ambazo
hakuna anaeweza kuzi verify
mfano ni lini alitangazwa kuwa ni 'mwanahabari wa mfano'?
alitangazwa na nani?

ni kweli ni mwanahabari mchapakazi ..lakini titles na masifa angeacha wengine waseme

na wala hizo title na masifa hazim halalishi kuwa mbunge

Zitto the same..ni kweli alisababisha baraza la mawaziri livunjwe but hakusaidiwa?
hizo sign 70 zote hazina maana kwake?
angepungua nini kama angesema 'tulisababisha baraza la mawaziri kuvunjwa'?

Malkia Elizabeth anaposema 'we' unafikiri kuna malkia wangapi UK?
lugha ya uongozi ni sisi na we
 
Back
Top Bottom